Kada wa CHADEMA
JF-Expert Member
- Feb 27, 2016
- 289
- 615
Imeniuma na imenisikitisha sana. CHADEMA sasa tumekubuhu kwa kuibaka Demokrasia na sasa tunaibaka waziwazi bila ya kificho.
Mtakumbuka kuwa Wabunge walioteuliwa na chama chetu kwenye abunge la Afrika ya Mashariki, Wenje na Masha walikataliwa Bungeni kwa kupigiwa kura za hapana. Hali hiyo imelazimu chama chetu kuanza mchakato wa kupata wagombea watakaopigiwa kura Bungeni ili kukiwakilisha chama chetu Ubunge wa Afrika ya Mashariki.
Jana Jumamosi, tarehe 29 Aprili 2017, Msemaji wa CHAMA bwana Makene ametoa Tangazo la kuwatangazia wanachama kote nchini kwenda kwenye ofisi za chama kujaza fomu za kuomba kuteuliwa na kwenye bunge la EALA. Mbaya zaidi tangazo lenyewe ni la kibaguzi kwa vile limewalenga wanawake tu.
Kinachonishangaza ni muda uliotolewa. Kwa mujibu wa Tangazo hilo, mwisho wa kurejesha fomu ni Mei Mosi na Mei 2 watakaoteuliwa wanapaswa kuwepo Dar es Dalaam kwa ajili ya kukamilisha taratibu za uhamiaji na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Najiuliza, je kwa mtu wa Kasulu, Namtumbo, Nanyamba, Sumbawanga nk ataweza masharti hayo? Arudishe fomu Mei Mosi na Mei 2 awepo Dar es Salaam, inawezekana? Hili ni changa la macho. Taarifa nilizonazo tayari Majina yameshaandaliwa na kinachofanyika kwa sasa ni kuwaghilibu wanachama na wananchi ili ionekane demokrasia imefanyika ndani ya chama. Hakuna.
Badala ya mchakato kuanza upya ndani ya chama, Mbowe ameelekeza kuwa Wenje na Masha wawepo kwenye orodha mpya eti kwa maelezo kuwa wakiondolewa ni kuwapa ushindi CCM. Pia Mbowe ameshaandaa majina ya wanawake ambao watajumuishwa kwenye orodha hiyo. Majina yaliyoandaliwa ni yale yenye ukakasi kwa CCM ili kuwapa wakati mgumu wakati wa kupiga kura. Pia majina hayo ni yale yenye mahusiano mema na ama Chairman ama mmiliki wa CHADEMA, Lowasa. Time will tell.
Unachofanya Mbowe ni dhihaka na dharau kwa chama chetu. Kwa mwendo huu kwa kweli hatutafika