Mbowe ana kesi 9 za uchochezi, lakini bado anapambana 'mpaka kieleweke'! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe ana kesi 9 za uchochezi, lakini bado anapambana 'mpaka kieleweke'!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bhikola, Jun 2, 2012.

 1. bhikola

  bhikola JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 457
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Sehemu ya maneno ya Mbowe wakati yuko kwenye mikutano Tandahimba (mikoa ya Kusini)


  Kuhusu kesi zake: “Hadi sasa mimi ninakesi tisa za uchochezi, sitanyamaza hata wakiniongezea nyingine, nitaendelea kusema ukweli kuhusu masuala ya ukombozi wa wananchi,wakitika wanifunge na hata nikifa wakati wa mapambano wanamageuzi wote wekeni maiti yangu pembeni songeni mbele,ukombozi utaletwa na wanawake na wanaume, ” alisemaMbowe.

  Kuhusu vurugu za moto katika soko la Tandahimba: "Serikali lazima itoea tamko, hatua gani wamechukuliwa watu waliochoma maduka ya wananchi na mali zao. Chadema haiwezi kukubali na mimi niko tayari kufunguliwa kesi zaidi za uchochezi na hata kufungwa jela, lakini sitaacha kuelimashi wananchi juu ya haki zao na ninawamba muunge mkono Chadema ichukue dola mwaka 2015 ili mpate ukombozi wa kweli,”alisema.

  Kuhusu kuingia ikulu: "Chadema hakipo kwa ajili ya kuwania udiwani na uenyekiti wa serikali za mitaa bali ni kuingia Ikulu kuongoza dola na kuleta utetezi wa kweli wa rasimali za watanznaia zikiwamo madini gesi na mafuta kuwanufaisha pia wakazi wa maeneo zinakotoka. Dhamira ya Chadema ni kuondoa serikali ya CCM katika uchaguzi wa 2015 na wakazi wa mikoa ya kusini msiyumbishwe na propaganda za udini,ukabila ukanda. Kwa hiyo wakazi wote wa kusini chagueni chama chenye mlengo wa kuwakomboa bila kujali ni chama gani".

  Mbowe ametoa msimamo huo wa chama ikiwa ni muda mfupi baada ya Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willbrod Slaa kueleza dhamira ya chama hicho kuwa ni kuhakikisha inawatetea kwa nguvu zote wakazi wa Tandahimba walioharibiwa mali zao na kwamba chama hicho kimemkabidhi jukumu hilo Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni .
   
 2. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Sasa itabidi mbunge wa Tandahimba afunguke bungeni vinginevyo akiwaachia wakina Mbowe wamsemee habari yake itakuwa imemalizika kabla 2015
   
 3. mutabilwa

  mutabilwa JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Now it's the time we need people like Mbowe, mm ninafuata nyayo zake ww je?
   
 4. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Mbunge wa tandahimba Juma Njwayo hamna ki2,alimuibia kura KATANI AHMED wa Cuf ila itabdi ktani Ahmed aangalie mstakabali wake coz CUF ipo taaban baada ya m4c kusini.walikuwa wanapategemea sana tandahimba
   
 5. bhikola

  bhikola JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 457
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  inabidi kumshauri katani ahmed ahamie chandimu
   
 6. asrams

  asrams JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 4,016
  Likes Received: 1,387
  Trophy Points: 280
  Mie sipendi siasa lakini Mbowe ana points za maana kweli, japokua wananchi bado ni viziwi.


  Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
   
 7. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Mbona kesi anayodaiwa na NSSF ya kampuni yake ya bilicans kutoweka malipo ya watumihi wake haisemi!? Kabunja sheria naye ni munga sheria!
   
 8. bhikola

  bhikola JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 457
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Mkuu usikurupuke, jifunze biashara kaka,
  1. Hakuna kambpuni ambayo haina madeni, na kama ipo basi "liquidity" yake ni "questionable"
  2. Lazima utenganishe biashara, na mmiliki wa biashara (business and business owner(s) are two different entities)
  3. Kampuni mbele ya sheria ni sawa na mtu (a company is a legal person) ndo maana kampuni inaweza kukopa au kukopwa, inaweza kushtaki au kushtakia, pia kampuni inaweza kuzaliwa na kufa

  hapo ni kwa ufupi tu, ukiona nimekuchanganya, njoo darasani kwangu ufute ujinga. Kwahiyo Mbowe siyo billicanas, na ndo maana hakushtakiwa mbowe, bali ilishtakiwa billicanas. na hata hao NSSF wakishinda madai yao hafilisiwi au hadaiwi mbowe, inadaiwa au inafilisiwa billicanas, na collaterals zilizowekwa na bodi ya wadhamini wakati wa kukopa

  Pole sana gamba
   
Loading...