Mbowe amvaa Magufuli Bungeni; Ubomoaji wa nyumba za Wananchi linazingatia Sheria au ni Utashi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe amvaa Magufuli Bungeni; Ubomoaji wa nyumba za Wananchi linazingatia Sheria au ni Utashi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by nngu007, Apr 16, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  na Mwandishi wetu  KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amembana Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, kutaka alieleze Bunge kwamba zoezi la ubomoaji wa nyumba za wananchi, linazingatia sheria au linatokana na utashi wa viongozi wa nchi.

  Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai (CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, aliomba ufafanuzi huo wakati akiuliza swali la nyongeza.

  Alisema kumekuwa na kauli zinazotofautiana za viongozi kuhusu ubomoaji wa nyumba zilizoko eneo la barabara kiasi kwamba wananchi wengi hawajui zoezi hilo linafanyika kwa mujibu wa sheria au linafuata matamko ya viongozi.

  “Tuhahitaji kufahamu kuhusu zoezi la bomoabomoa, maana hatuelewi linafanyika kwa mujibu wa sheria au matamko ya viongozi kwani hali hiyo inawafanya wananchi wa kawaida washindwe kutambua haki zao kwa mujibu wa sheria, sasa ni wakati muafaka kwa serikali kutoa ufafanuzi,” alisema Mbowe.

  Akijibu swali hilo, Waziri Magufuli alisema zoezi la ubomoaji wa nyumba zilizo maeneo ya barabara, linatekelezwa kwa mujibu wa sheria namba 4 mwaka 1999, 5 mwaka 1999 na mabadiliko ya sheria ya barabara ya mwaka 2008, 2007 na 2013, ambazo zinaelekeza utekelezaji wa sheria hiyo.

  Alisema kama waziri mwenye dhamana, atatekeleza na kusimamia sheria hiyo kwani hata alipoapa alisema atailinda sheria na aliomba Mungu amsaidie.

  Alisema sheria hiyo ndiyo inayosimamia na kutekelezwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), kinachoongoza serikali.

  Hata hivyo Waziri Magufuli, hakuwa tayari kuzungumzia mgongano wa kauli za viongozi wa juu ambazo zinatofautiana na kauli yake (Magufuli).
  Hivi karibuni, Waziri Magufuli aliagiza ubomoaji wa nyumba zote zilizojengwa kwenye eneo la hifadhi ya barabara, lakini Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Rais Jakaya Kikwete kwa nyakati tofauti, waliingilia kati kusitisha zoezi hilo kwa madai kuwa litaathiri wananchi ambao wengi wamejenga nyumba zao kwa shida.

  Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Majaliwa, alisema wakazi 1050 wa Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam, hasa wa mitaa ya Kizani na Mwera, watalipwa fidia ya mali, usumbufu, malazi, upotevu wa faida na usafiri kwa nyumba 249.

  Aliyasema hayo wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Philipa Mturano, aliyetaka kujua kiasi cha fedha watakazolipwa wakazi wa mitaa ya Kizani na Mwera. Waziri Majaliwa, alisema zoezi la ulipaji wa fidia kwa wananchi hao, linatarajia kuanza rasmi Aprili 18. Alisema serikali imetenga sh bilioni 7.5 kwa ajili ya malipo hayo.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kumbe hata Magufuli amekubali kuchutama kwa mafisadi!
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,892
  Trophy Points: 280
  hivi serikali inakuwaga wap i hadi watu wajijengee pembezoni mwa bara bara?? sijaelewa bado mimi
   
 4. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Akisema Rais Kikwete amekosea, Akisema PM Pinda, amekosea. Ila akisema Freeman ahhhaaaa hapo ndiyo. this is crazy.
   
 5. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbowe alitegemea magufuli ajibu nini? Magufuli anafuata sheria inasema nini, lakini siasa za wakubwa wake ni kikwazo, sasa magufuli hawezi kusema kwamba wakubwa wake ni kikwazo, atamwaga unga wake, na hapo ndio tatizo letu watz lilipo.Watz tunafanya kazi kwa kujali sana matumbo yetu binafsi siyo ustawi wa nchi na hivyo kupiga hatua ya maendeleo kama nchi itaendelea kuwa ndoto. Namheshimu sana magufuli kwa stahili yake ya utendaji kazi, ila asimia nyingi nimezipunguza toka kwake kwa kutochukua hatua muafaka katika tatizo lililotokea la kuzuiwa kufanya kazi yake kisheria kwa hoja za kisiasa, pale alitakiwa ajiuzulu, lakini kwa kuwa sisi watz tunafanyia kazi za serikali matumbo yetu sio nchi jamaa kaona aendelee tu kubaki waziri kwa kuwa hana binafsi anachopoteza.Yule mama waziri wa uingereza mambo ya afrika Clare Short aliamua kujiuzulu uwaziri wake kule uingereza kupinga tz kuuziwa rada kwa bei ya kuruka, nampongeza sana yule mama kwa ujasiri wake ila kwa upande mwingine namhurumia sana sana maana anatuthamini sisi wakati sisi wenyewe hatujithamini, anatujali wakati sisi wenyewe hatujijali, namhurumia sana.
   
Loading...