Mbowe amuomba Rais Samia kuunda kamati ya maridhiano

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,763
4,327
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amemwomba Rais Samia Suluhu Hassan kuunda Tume ya Ukweli na Maridhiano, ili kutibu majeraha ya makundi mbalimbali ya kijamii yaliyotokana na alichokisema uongozi usiozingatia sheria na Katiba.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo Jumatatu Julai 19, Mbowe amesema japo wapo ambao maumivu yao yanajulikana ni viongozi wa kisiasa na wanaharakati

"Wafugaji mifugo yao imetaifishwa, wafanyabiashara wameporwa fedha zao kwenye akaunti, wale wa maduka ya fedha za kigeni nao hawakubaki salama; maduka yalifungwa na fedha zao kuchukuliwa," amesema Mbowe

Amesema japo siyo wengi wanathubutu kujitokeza kuzungumza, lakini ukweli ni kwamba watu wengi wameathirika na kuna haja ya kupewa fursa ya kuzungumza madhila yao ili kuponyesha nafsi zao na Taifa kwa ujumla.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom