Mbowe amuhoji Waziri Mkuu juu ya matukio yanayojenga chuki, avituhumu vyombo vya dola kukosa dhamira sakata la Lissu

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,426
7,736
Mwenyekiti wa kambi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe amemuuliza waziri mkuu juu matukio mengi ya siku za karibuni yanayovunja amani, usalama na yanayojenga chuki miongoni mwa vyama vya siasa na kuharibu utengamano wa kitaifa.

Amesema tukio la kushambuliwa kwa risasi kwa dhamira ya kuua kwa mbunge Tundu Lissu imezua hofu kubwa kwa Taifa, bara zima la Afrika na jumuiya ya kimataifa na taharuki hiyo imeharibu taswira na heshima ya Taifa.

Amesema hawajaona kama serikali imechukua hatua yoyote kujaribu suala hilo kutoendelea kuharibu taswira ya Taifa. Amesema hapo nyuma vilitokea vifo vya kisiasa na hakuna hatua zilizochukuliwa hadi sasa.

Akijibu swali hilo, waziri mkuu amesema yapo matukio yanajitokeza na japokuwa mheshimiwa Mbowe ameongelea upande wa siasa, yapo matukio kwa ujumla wake nchini kwenye maeneo kadhaa. Amesema wapo watu hawana nia njia wamejitokeza ikiwemo wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji kupoteza watu wengi pia kamanda wa JWTZ kupigwa risasi hiyo wayazungumze yote kwa ujumla wake.

Amesema vyombo vya dola vinaendelea kufanya uchunguzi na hauwezi ukawa uchunguzi wa leo na ufumbuzi ukatoka leo. Amesema vyombo vya dola vina uwezo na suala la muda tu kwani wahusika walitumia mbinu nyingi kuhakikisha wanajificha. Amesema uchunguzi ukikamilika watatoa taarifa na waendelee kujenga imani kwa vyombo vya dola.

Mbowe akiuliza swali la nyongeza alisema anajua ya kila mtanzania yana thamani kubwalakini swali lake lilikuwa specific kwa siasa, amesema kushambuliwa Lissu sio la kawaida na uonevu dhidi ya vyama vya siasa nchini na leo ni siku ya tatu tangu mbunge akamatwe Mtwara. Je, Serikali inaona shida gani kuruhusu vyombo vya kimataifa vya kiuchunguzi kuja kufanya uchunguzi kwa sababu sio mara ya kwanza serikali kuomba msaada kutoka nchi za nje akitolea mfano benki kuu ilipoungua hivyo ni jambo la kawaida. Amesema vyombo vya dola hawavidharau bali havina dhamira.

Waziri mkuu amesema hakuna aliefurahishwa na matukio yanayojitokeza ya mauaji au ya shambulio kwa mbunge mwenzao lakini vyombo vya dola vimepewa jukumu la kusimamia na kulinda na pia ikitokea vina wajibu wa kufanya uchunguzi.
 
Nimemsikiliza waziri mkuu akisema sio kwa Lissu pekee, akatolea mfano afisa wa JWTZ. Tofauti ni kwamba wahusika kwa shambulizi kwa afisa wa JW walitiwa hatiani ndani ya muda mfupi.
 
Waziri Mku Alimjibu Mbowe Kisiasa Nasuala La Wabunge Wa Upinzan Kunyanyswa Na Dola Hakujibu

Hakuna mtu anaenyanyaswa nchii hii na kua mpinzani sio sababu ya kuzarau na kutukana mamlaka jukwaani na kama mnajitegeza kwa kutukana viongozi wa serikali jukwaani akiwemo raisi na mkikamatwa kwa kuvunja sheria ili mpate sababu ya kusema mnanyanyaswa basi mtasema sana.

Pia kuhusu Tundu lisu serikali imetamka kua inafanya uchunguzi sasa si muachie vyombo vya dola na mbona kuna watanzania wengi hasa rufiji wananchi wameuwawa kinyama wakiwemo polisi wetu mbona hamuonyeshi kuguswa kama Tundu lissu??

Tendeni haki maana wote ni binadamu na ni watanzania wenzetu sio kila siku mchukulie Tundu lisu kama ndio mwenye haki pekee katika hili.
 
Jana mnafiki bashe alikuwa anatowa wosia kuwa taifa hili halihitaji umoja,leo yuko kimya wabunge wanadhalilishwa na mapolis
 
Nimemsikiliza waziri mkuu akisema sio kwa Lissu pekee, akatolea mfano afisa wa JWTZ. Tofauti ni kwamba wahusika kwa shambulizi kwa afisa wa JW walitiwa hatiani ndani ya muda mfupi.

Ushirikiano ulikuwepo kwenye tukio la kushambuliwa askari wa JWTZ. Kwa Lissu wale waliotakiwa kutoa ushirikiano wanahujumu juhudi za polisi. Kwa mfano kumficha dereva wa Lissu kwa makusudi ni kuhujumu juhudi za polisi kwenye uchunguzi. Kuna uwezekano mkubwa sana tena sana tu kuwa waliochora mpango wa kumuua Lissu walimshirikisha dereva wake. Dereva leo kafichwa Nairobi sasa uchunguzi utafanyikaje ikiwa prime suspect au prime witness anawekewa kifua asihojiwe?
 
Hakuna mtu anaenyanyaswa nchii hii na kua mpinzani sio sababu ya kuzarau na kutukana mamlaka jukwaani na kama mnajitegeza kwa kutukana viongozi wa serikali jukwaani akiwemo raisi na mkikamatwa kwa kuvunja sheria ili mpate sababu ya kusema mnanyanyaswa basi mtasema sana. Pia kuhusu Tundu lisu serikali imetamka kua inafanya uchunguzi sasa si muachie vyombo vya dola na mbona kuna watanzania wengi hasa rufiji wananchi wameuwawa kinyama wakiwemo polisi wetu mbona hamuonyeshi kuguswa kama Tundu lissu?? Tendeni haki maana wote ni binadamu na ni watanzania wenzetu sio kila siku mchukulie Tundu lisu kama ndio mwenye haki pekee katika hili.
kwani suala la kibiti si wao serikali walikataa lisizungumzwe, sasa watu wamekaa kimya halafu wao wanarudi kusema mbona watu walikaa kimya? wacha nicheke mie
 
Ushirikiano ulikuwepo kwenye tukio la kushambuliwa askari wa JWTZ. Kwa Lissu wale waliotakiwa kutoa ushirikiano wanahujumu juhudi za polisi. Kwa mfano kumficha dereva wa Lissu kwa makusudi ni kuhujumu juhudi za polisi kwenye uchunguzi. Kuna uwezekano mkubwa sana tena sana tu kuwa waliochora mpango wa kumuua Lissu walimshirikisha dereva wake. Dereva leo kafichwa Nairobi sasa uchunguzi utafanyikaje ikiwa prime suspect au prime witness anawekewa kifua asihojiwe?
kwani camera mlizong'oa mumezipeleka wapi, wale walinzi waliokuwepo mbona hamuwahoji, kwa hiyo dereva angekufa ndio hakuna upelelezi, msituone watz mazwazwa kiasi hicho tunawachora tu, mnavyojihashua
 
Mbowe anajua kama amepoteza mvuto kwa kula na wachafu na ni mchafu?

Naona hata taarifa zake siku hizi hawachangamkii.
Mkuu hapa hoja sio Mbowe,bali ni maswali aliyouliza ndio yanayojadiliwa.
Kama vipi anzisha uzi kihusiana na Mbowe,kuliko kuhamisha magoli.
 
Halikuwa swali serious. Huez hoji uwajibikaji kwa serikali ya ccn ya awamu hii. Utakamatwa kwa uchochezi!!
 
Mimi nafikiri UPINZANI ndio unaoongoza kwa kumnyanyasa hasa magufuli. Wao matusi,kejeli,dhihaka na maneno yote machafu dhidi ya magufuli ni MOJA YA HAKI ZAO ZA MSINGI. Haishangazi kuona mbunge anaona ameonewa baada ya kumuita Rais ni mtu wa ovyo mara anamaamuz ya kijinga. Magufuli ni binadam kama binadam wengine,inapotokea mtu anatumia uwezo wake vibaya wa kisheria na influence aliyonayo ktk jamii,inaumiza sana.Nafikiri neno UKOSOAJI ktk siasa za Tanzania tungeliondoa,Maana huu sio ukosoaji,huu ni UDHARIRISHAJI.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom