Boniphace Kichonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 1,606
- 1,956
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema ameshangazwa na kauli ya Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Elizabeth Mkwizu kwamba hakuna rufaa ya uchaguzi wa Jimbo la Longido mahakamani hapo.
Elizabeth akizungumza na Mwananchi juzi alisema, “Hapa hatuna rufaa ya uchaguzi wa Jimbo la Longido, bali kuna maombi ya kuongezwa muda wa kuwasilisha ‘notice of appeal’ (taarifa ya kusudio la kukata rufaa). Walileta notice of appeal lakini ikatupiliwa mbali, sasa wanaomba muda ili waiwasilishe tena. Maombi si rufaa, kwa hiyo haya maombi yasingeweza kusimamisha shughuli za uchaguzi.”
Alikuwa akirejea uchaguzi mdogo uliofanyika Januari 13 baada ya aliyekuwa mbunge wa Longido kwa tiketi ya Chadema, Onesmo ole Nangole ushindi wake kutenguliwa na Mahakama Kuu.
Hata hivyo, Mbowe akizungumza na Mwananchi jana alisema kuna vitu vinaendelea kwa namna moja au nyingine katika Mahakama vinafikirisha na kuona wapinzani hawatendewi haki.
“Kama wanakiri maombi yalipelekwa na wanayo, kufungua kesi si ni ‘process’ (mchakato), zote za kwenda kukata rufaa sasa kama maombi yatakubaliwa na tukakata rufaa, huo uchaguzi ulioitishwa na kufanyika inakuwaje?” alihoji;
“Hakuna mtu anayetaka kukata rufaa bila sababu, maombi hayo ni sehemu ya kesi. Lakini kwa nini wasingesikiliza haraka hayo maombi ili kama yanakataliwa uchaguzi ufanyike.”
Mbowe, ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alisema, “Kuna mambo ambayo yafanyika katika Mahakama zetu baadhi yanatia doa na ndilo tatizo la nchi yetu.”
Katika ufafanuzi wake, Mkwizu alisema kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya Mahakama ya Rufaa, maombi hayo yamepangwa kusikilizwa na Jaji Jacob Mwambegele, Februari 5.
Wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo, mwombaji kupitia kwa mawakili wake atalazimika kutoa sababu za kuiridhisha Mahakama ni kwa nini alichelewa kuwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa.
Ikiwa Mahakama haitaridhika na sababu zake, itatupilia mbali maombi hayo lakini ikiridhika nazo itamruhusu kuwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa.
Baada ya kuwasilisha taarifa hiyo, atasubiri kupata kumbukumbu za rufaa, yaani nyaraka zitakazohusika kwenye rufaa yake, ikiwamo hukumu anayoilalamikia, mwenendo wa kesi ya msingi na vielelezo vilivyotumika.
Akipata nyaraka hizo, ndipo atakapowasilisha rufaa kamili, yaani sababu za kwa nini anapinga hukumu iliyomvua ubunge wa jimbo hilo, na upande wa pili (wajibu rufaa) nao utawasilisha hoja zake na baada ya Mahakama kusikiliza hoja za pande zote ndipo itatoa hukumu.
Ole Nangole alivuliwa ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Juni 29, 2016 kutokana na kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya CCM, Dk Steven Kiruswa akipinga ushindi wake.
Baada ya Mahakama kumvua ubunge, Ole Nangole kupitia mawakili John Materu na Dancan Oola aliwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.
Hata hivyo, taarifa hiyo ya kusudio la kukata rufaa ilitupiliwa mbali kwa kuwa muda wa kisheria wa siku 14 za kuwasilisha kusudio la kukata rufaa ulikuwa umeshaisha ndipo alipoomba kuongezewa muda wa kuwasilisha taarifa hiyo.
Maombi hayo pia yalitupiliwa mbali na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, ndipo wakapeleka maombi Mahakama ya Rufani
Chanzo: Mwananchi