Mbowe amkaribisha Kimaro CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe amkaribisha Kimaro CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngongo, Mar 21, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemtaka Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), kujiunga na chama hicho kama ana dhamira ya kweli ya kupambana na ufisadi, vinginevyo hataweza kutimiza malengo hayo akiwa ndani ya CCM.

  Hayo yalielezwa jana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Kilimanjaro, Philemon Ndesamburo, kwa nyakati tofauti wakati wakihutubia mikutano ya hadhara ya chama hicho, iliyofanyika juzi katika vijiji vya Kilema, Marangu Mtoni, Mwika na Himo, ikiwa ni mfululizo wa mikutano ya Operesheni Sangara inayoendelea mkoani hapa.

  Mbowe alimtaka mbunge huyo wa Vunjo kuungana na CHADEMA katika mapambano ya kweli dhidi ya ufisadi, kwani CCM haina dhamira ya kweli wala mfumo muafaka wa kukiwezesha kupambana na mafisadi.

  “Kama kweli mbunge wenu, Aloyce Kimaro, ana dhamira ya kweli ya kupambana na ufisadi wa nchi hii, basi aje CHADEMA tuunganishe nguvu. Huwezi ukasema unapambana na mafisadi halafu uko ndani ya CCM, haiwezekani. CCM ni chama cha mafisadi. Waheshimiwa wananchi wa Marangu ni bora usijue jinsi nchi hii inavyoibiwa na kutafunwa na CCM. Wizarani kote wizi, mikoani wizi, wilayani wizi, kwenye vijiji wizi, nchi hii ni wizi mtupu!”

  “Wakati wa kampeni nilisema chini ya mfumo wa CCM, hakuna mabadiliko. Nilisema hata aje malaika kutoka mbinguni halafu apewe kazi ya kuiongoza nchi hii, hataweza. Baada ya miezi sita tu naye lazima atakuwa fisadi. Namwambia ndugu yangu Kimaro kama kweli anawapenda wananchi wa Vunjo na anauchukuia ufisadi, basi atoke CCM, vinginevyo naye atabakia kuwa fisadi tu kama walivyo wenzake na chama chake cha kifisadi, CCM,” alisema Mbowe na kushangiliwa.

  Mbowe aliwataka wakazi wa eneo la Marangu Mtoni, ambalo ni sehemu ya Jimbo la Vunjo, kutokubali kugawanywa katika misingi ya vyama na badala yake, waunganishe nguvu zao katika kuutafuta ukombozi wa kweli kupitia CHADEMA.

  Alisema CCM ilitekeleza mkakati wa kuhakikisha kunakuwa na vyama vingi vya siasa kwa lengo la kuwagawa wananchi ili iwe rahisi kwa chama hicho kuendelea kutawala.

  Alisema inashangaza kuona Tanzania, nchi yenye umaskini mkubwa duniani ikiwa na vyama vya siasa 17, wakati Marekani nchi tajiri, yenye watu wengi na iliyo kubwa, ikiwa na vyama viwili tu vya siasa.

  Alisisitiza kuwa utitiri wa vyama vya siasa nchini, hauna manufaa kwa Watanzania, zaidi ya kukisaidia CCM kuwagawa na kuwatala wananchi kwa maslahi ya viongozi na matajiri wachache.

  “CCM inatumia wingi wa vyama vya siasa kuwagawa Watanzania. Wanatekeleza sera ya mkoloni wa Kiingereza, ya wagawe uwatawale, ‘divide and rule policy’. Leo watu wa Vunjo mmegawanywa katika misingi ya vyama na kusahau kilicho muhimu kwenu. Utakuta huyu TLP, mwingine CHADEMA, CUF, sijui CUF, NCCR Mageuzi, mmegawanywa ili mtawaliwe. Mmegawanywa katika itikadi za vyama ili iwe rahisi kwa CCM kuwatawala kwa maslahi yao,” alisema Mbowe.

  Akitoa mfano, alisema katika uchaguzi wa ubunge wa Jimbo la Vunjo mwaka 2005, Kimaro alipata asilimia 42 ya kura, huku asilimia 58 ya kura ikiwa imekwenda kwa vyama vya upinzani.

  Alisema licha ya Kimaro kupata asilimia 42 tu ya kura kulinganisha na asilimia 58 za wapinzani, bado aliweza kukinyakua kiti hicho kwa sababu kura za upinzani, zilipigwa kwa kugawanywa, huku vyama vya CHADEMA, NCCR-Mageuzi na TLP, kila kimoja kikipata kura pungufu na zile alizopata Kimaro.

  “Kimaro alipata asilimia 42 ya kura, upinzani ulipata asilimia 58. Alishinda kwa sababu kura za upinzani ziligawanyika, CHADEMA ilipata kidogo, TLP ilipata kidogo, NCCR nayo hivyo hivyo, ilipata kura pungufu ya zile alizopata Kimaro. Hayo ndiyo madhara ya sera ya wagawanye uwatawale,” alisema Mbowe wakati akihutubia umati wakazi wa mji mdogo wa Himo.

  Alisema baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliopita, yeye na viongozi wenzake walijitahidi kuunganisha vyama vya upinzani ili kuikabili CCM, lakini jitihada zao zilishindikana kwa sababu ya vyama hivyo kutofautiana na malengo na dhamira ya kuwapigania wananchi.

  Mbowe ambaye katika hotuba hiyo hakupenda kuwashambulia viongozi wa vyama vya upinzani kwa majina yao, alisema baada ya kuona jitihada za kuunganisha vyama vya upinzani zinachelewa na kushindikana, CHADEMA iliamua kubuni Operesheni Sangara ili kwenda kuwaunganisha wananchi wa vyama mbalimbali katika kupambana na ufisadi na kupigania maendeleo yao.

  “Ndugu zangu, tulipoona jitihada za kuunganisha upinzani zinachelewa na kushindikana, tukasema kama vyama vyetu vimeshindwa kuungana basi twende tukawaunganishe Watanzania. Kwa hiyo tulibuni operesheni sangara, tulikwenda majimbo yote ya Mkoa wa Mara, Mwanza, Mbeya, Dar es Salaam, tumekuja Kilimanjaro, tutarudi Dar es Salaam ili kukusanya nguvu kidogo, kisha tutakwenda Kagera, Kigoma, Shinyanga, Tabora………tunatembea nchi nzima kuwaunganisha Watanzania katika harakati za kujikomboa zinazoongozwa na CHADEMA,” alisema Mbowe wakati akiwahutubia wananchi wa Marangu Mtoni.

  Alisema baada ya CHADEMA kujaribu kuviunganisha vyama vingine vya upinzani bila mafanikio, sasa umefika wakati kwa wananchi kupima na kukiunga chama cha upinzani chenye nguvu kuliko vingine ili iwe rahisi kuikomboa nchi kwa kukiwezesha chama hicho kuing’oa CCM.

  Alisema aliwaambia wakazi wa Kilema, Marangu Mtoni, Mwika, na Himo, kuwa CHADEMA ndicho chama cha upinzani chenye nguvu hivi sasa kuliko vyama vingine na hivyo ni vema wananchi wakaunganisha nguvu zao kwa CHADEMA ili iwe rahisi kuing’oa CCM.

  “CHADEMA hivi sasa ndicho chama cha upinzani chenye nguvu kuliko vyote, uwongo? TLP haina mbunge hata mmoja, CHADEMA tuna wabunge 11, CHADEMA tunaongoza halmashauri tatu, za Kigoma, Karatu na Tarime, TLP na vyama vingine vya upinzani hakuna anayeongoza halmashauri. CHADEMA tuna madiwani zaidi ya 118, TLP wana madiwani kidogo. Ni rahisi kuwaunganisha Watanzania kupitia CHADEMA kuliko kupitia chama kingine chochote cha upinzani,’’ alisema Mbowe wakati akiwahutubia wakazi wa Mwika.

  Katika hatua nyingine, polisi waliokuwa wakilinda mkutano wa CHADEMA uliofanyika mjini Himo, walimwaamuru Mbowe kuhitimisha mkutano huo na kushuka jukwaani kwa kile walichodai kuwa muda ulikuwa umekwisha, lakini umati wa watu waliofurika ulimlazimisha mwenyekiti huyo wa CHADEMA, kuendelea na mkutano huo bila kujali amri hiyo ya polisi.

  “Hiyo ndiyo nguvu ya umma bwana. Ndugu yangu polisi, sisi tunajadili mambo yanayohusu maisha yako wewe, unataka tufunge mkutano! Angekuwa kiongozi wa CCM hapa angehutubia hadi usiku na wala asingeambiwa afunge mkutano, angekuwa Makamba hapa angehutubia hadi usiku. Lakini si kosa lake, najua wanasumbuliwa sana na CCM, ukiona hivyo ujue kashapigiwa simu na CCM. Sasa nilikuwa nafunga mkutano lakini kwa sababu mmeamua Mbowe niendelee, naendelea. Siogopi polisi, nawaheshimu ninyi wananchi,” alisema Mbowe na wakazi hao kushangilia.

  Katika mikutano hiyo, CHADEMA ilivuna mamia ya wanachama wapya, na kupokea michango ya fedha kutoka kwa wananchi wa maeneo husika, waliojitolea kwa ajili ya kugharamia mikutano mingine ya operesheni sangara inayoendelea mkoani Kilimanjaro.

  Mikutano hiyo ya operesheni Sangara, leo inaingia katika Jimbo la Rombo, kabla ya kuendelea tena kesho katika maeneo ya Mwanga, Same Magharibi na Same Mashariki. Source:Tanzania Daima
   
 2. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hiyo Sangara yenyewe Wizi mtupu! Haiwezekani huyo Mbowe akafanya mikutano mingi hivyo wakati hatumii helikopta

  ..........ndiyohiyo
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Chadema inaanza kupoteza mwelekeo taratibu na hii operasheni sangara imekuwa sehemu ya propaganda zaidi badala ya kuwaambia watanzania watawafanyia nini.Maudhui ya karibu mikutano yote yanafanana kiasi kwamba mikutano inakosa msisimko.Mwenyekiti Mbowe amenukuliwa mara kwa mara akisifia utawala wa Mzee Ruksa na kuuponda huu wa sasa.Zitto Kabwe naye alipokuwa katika jimbo la uchaguzi la mhe W Ngeleja alimwasifa kwamba ni waziri hodari sana,na akamshauri ajiunge na Chadema.Propaganda zimeamia kwa mh A Kimaro naye ajiunge na Chadema ili aweze kupambana na ufisadi ?.

  Hali inaweza kuwa mbaya sana kwa vyama vya upinzani kipindi cha uchaguzi iwapo A Kimaro,W Ngeleja na wabunge wengine wa CCM wanaosifiwa na viongozi waandamizi wa Chadema wataendelea kutetea viti vyao vya ubunge kupitia CCM.Fedha na muda wanaopoteza kusifia wabunge wa CCM inaonyesha wazi Operesheni Sangara ni mkakati wa hovyo.

  Bado nasisistiza bila upinzani kuungana na kuwa kitu kimoja wasitarajie wataweza kuiondosha CCM madarakani.Fedha na muda wanazotumia Chadema lazima zilenge kuondoa CCM madarakani.Nasikitika kusema kwamba Chedema na Operasheni sangara wanazidi kuwaondolea wananchi wengi tuliokuwa na matumaini ya uchaguzi mkuu mwaka 2010.
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,868
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Kaazi kweli kweli!!!
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,309
  Trophy Points: 280
  Huo ni ushauri mzuri kwa Kimaro, Moshi hawaipendi CCM, Kimaro bila kuhama CCM atalipoteza jimbo la Vunjo.
  Sio kweli kuwa Chadema ndio chama kikuu cha upinzani. Chama kikuu ni CUF, Chadema ni baadhi ya maeneo bara. Lazima kiunganishe nguvu na vyama vingine kwa kutosimamisha mgombea maeneo ambayo vyama vingine vinakubalika zaidi.
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Mar 21, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kazi hii sio kosa la wananchi ila Upinzani na hakika CCM wataendelea kushinda hata kama Chadema itachukua wabunge wote wa CCM...
  Ikumbukwe tu kwamba wananchi huchagua mgombea kutokana na kuwepo kwa vyama vingi na sio nani mgombea..mpenzi wa CCM, CUF, NCCR ataendelea kuchagua mgombea wake..
   
 7. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Chadema si chama kikuu cha upinzani wala haitakuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania hata siku moja.Viongozi wa Chadema wako tayari kusema uongo ili kutimiza malengo yao ya kifisadi.Ki msingi CCM ya kwanza na TLP ilikuwa ya pili kwa tofauti ya kura zisizozidi mia Chadema ya tatu.Ni kwanini Mbowe na Ndesamburo hawataki kuelewa TLP inakubalika zaidi Vunjo kuliko Chadema !.Badala ya kuiunga mkono TLP wanaanza kuwachanganya wananchi kwa maneno ya uongo na upuuzi.Mrema atachukua kiti cha ubunge Vunjo Chadema watake wasitake.
   
 8. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kabonde

  Wewe ndio uko tayari kusema uongo kwa malengo yako. Si kweli kwamba TLP ilikuwa ya pili kwa kura zisizozidi mia. Ilizidiwa kwa kura nyingi. Lakini alichokisema Mbowe hapo juu ni kuwa kura za upinzani zingeunganishwa, zingemishinda wa CCM.

  Kwa taarifa yako, TLP imeporomoka vibaya vunjo kama ambavyo Mrema amekuwa akiporomoka. Kwa TLP ni Mrema na Mrema ndio TLP. Kumbuka kwamba matokeo ya mwaka 2000 TLP ilishinda jimbo hilo, pamoja na kuwa kulikuwa na wagombea wa vyama vingine kama CCM, CHADEMA, NCCR.

  Hivyo, kushindwa mwaka 2005 ni aibu kwa TLP kwa kuwa ilishuka na kupoteza jimbo lake lililokuwa chini ya Jesse Makundi pamoja na Mrema kuweka kambi kule.

  Sababu sio kugawana kura tu kwa kambi ya upinzani, kwani kama ingekuwa hiyo ndio sababu pekee TLP isingeshinda mwaka 2000. Sababu ni watu kupunguza matumaini na Makundi, Mrema na TLP ndio maana wakafikiria vyama vingine, CHADEMA na NCCR kule.

  Sasa hiyo ni mwaka 2005, sasa ni 2009. Hali imebadilika zaidi, TLP imekwisha kule kabisa. Utakuja kuniambia matokeo ya mwaka 2010, TLP hata Mrema akigombea yeye mwenye akijitahidi sana anashika nafasi ya tatu.

  Na hii si vunjo tu, maeneo mengi katika nchi ambapo TLP ilishika nafasi ya pili imeporomoka kabisa katika chaguzi za sasa. Mfano ni Arusha ambapo TLP ilikaribia kuing'oa CCM lakini kwenye uchaguzi wa juzi wa marudio pale Arusha kati ilipata kura moja tu! Na kushika nafasi ya nne, walishindwa hata na CUF.

  Siasa za Tanzania bara zimebadilika sana, mwaka 1995 ilikuwa ni fursa ya NCCR, Mwaka 2000 TLP, mwaka 2005 ilikuwa ni CUF. Sasa upepo wa siasa uko CHADEMA. Tuombe heri upepo huu udumu na kufanikiwa kuindoa CCM madarakani. Kwa upande wa Zanzibar upepo bado ni wa CUF. Huyo Kimaro, kama bado anapenda kuongoza vunjo, asipoteze muda CCM. Atapita kwa tabu kura za maoni, na atakuja kushindwa na CHADEMA.

  Asha
   
 9. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkandara,

  Mbona Zitto alishinda Kigoma Kaskazini pamoja na kuwa palikuwa na mgombea wa CUF? Au Mbona Dr Slaa alishinda pamoja na kuwa kulikuwa pia na wagombea wa NCCR na SAU. Mbona Ndesamburo alishinda wakati palikuwa na vyama vingi vya upinzani ikiwemo TLP?

  Ukipitia matokeo ya uchaguzi mwaka 2005, ni majimbo hayafiki kumi kati ya majimbo zaidi ya mia mbili ndiyo ambayo kura za upinzani ukizijumlisha zinazidi za yule wa CCM. Kwa hiyo vyama kuungana sio sababu kuu ya kufanya upinzani ushinde.

  Asha
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi ni kwa nini katika siku za hivi karibuni Chadema imekuwa ikiwakaribisha sana hawa wabunge wa CCM wanaitwa kuwa ni wapambanaji dhidi ya ufisadi... juzi tulisikia wakimwita Mwakyembe aungane nao
   
 11. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  yes, ccm si chama cha uleta mabadiliko katika hali kama hii ya matajiri tu wanatumia kisingizio cha kupambana na ufisad kwa maslahi yao na vikampuni vyao mikobani.
   
 12. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Asaha inamaana kuwa unaona ni jambo zuri la Mwenyekiti wenu kumkaribisha KIMARO kujiunga na CHADEMA. Hivi kweli mnakitakia mema CHADEMA na nchi yetu Tanzania? Kuna wengi wa kuwakaribisha lakini sio KIMARO ninayemjua mimi.....

  omarilyas
   
 13. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Bwana mzee nadhani hii ni lugha ya picha. Anaekaribishwa hapa sio Kimaro, isipokuwa wapiga kura wa Kimaro, kwani angekuwa kimaro angekuwa approached popote pale na sio jimboni kwake.
   
 14. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #14
  Mar 22, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Simuungi mkono Mwenyekiti kumkaribisha Kimaro. Kwani CHADEMA ina wagombea wazuri waadilifu ikiwemo vijana wenye kuweza kugombea hilo jimbo. Lakini naamini hapo Mwenyekiti ametumia lugha ya picha kuonyesha uozo wa CCM na kuvunja kila Kimaro aliposhikilia. Hivi mnadhani ni nani anafaa kugombea hilo jimbo?

  Hapo juu kwenye maelezo yangu nilikuwa namjibu huyo aliyedhani TLP ina nguvu tena kule.

  Asha
   
 15. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2009
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kwani CHADEMA hawajatoa sababu za kuwakaribisha wabunge hao wa CCM?Mbona kila siku wanazitaja sababu hizo na hata katika habari hii Mbowe ameeleza bayana kwamba ni vigumu mno kwa wabunge wanaopambana na ufisadi kufanikiwa ndani ya CCM kwa vile chama hicho kinalea mafisadi...
   
 16. Nyumbu

  Nyumbu Senior Member

  #16
  Mar 22, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakitumia helikopta mnawaita wabadhirifu. Wakiacha kutumia helikopta mnasema wizi mtupu. Acheni wivu. Chadema kimebaki kuwa chama chenyewe kinachoweza kufanya mikutano inayovuta wananchi wengi bila kutumia mafuso au misikiti. Nenda mwenyewe ukajionee.
   
 17. Nyumbu

  Nyumbu Senior Member

  #17
  Mar 22, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Zamani, Mwaka 2005, Mwenyekiti wa chadema, Mbowe alipata kura 13,812 za urais jimbo la vunjo. Mwenyekiti wa TLP, Mrema alipata kura 12,587 za urais katika jimbo hilohilo. Ndani ya Vunjo, ALIKOZALIWA MREMA, waliomkubali Mbowe walikuwa wengi kuliko waliomkubali Mrema. Sio hivyo tu, majuzi katika uchaguzi mdogo wa kijiji ALIKOZALIWA MREMA Chadema imeshinda.

  Zamani, Mwaka 2005, Aloyce Kimaro wa CCM alipata kura 30,554 na Jesse Makundi wa TLP alipata kura 21,771. Tofauti hapa ni maelfu sio "zisizozidi mia" kama unavyotaka tukuingiza mjini.

  Hata hivyo, takwimu za 2005 zitakusaidia ku-evaluate vyama vinavyokuwa active wakati wa uchaguzi tu - Vyama kama UPDP, NRA, NLD, Jahazi Asilia, UMD, Makini etc. Vyama ambavyo viko active vinavyojijenga kila siku takwimu hizi haziwezi kukupa picha kamili.

  Ukitaka kujua chama kikuu cha upinzani Tanzania bara ni kipi waulize walioko madarakani, yaani CCM. Waulize Tambwe na Makamba wanaopoteza nusu ya muda wao kufukuzana na operation sangara. Mwulize Mama Nsilo Swai anavyohaha sasa Kilimanjaro na operation nyavu. Waulize vikao vyao vya usiku visivyoisha wanamjadili nani? Simple observation - hapa JF ni vyama vipi vinavyoongelewa kupita vingine? Utake usitake chama kikuu cha upinzani bara ni Chadema, na chama kikuu cha upinzani visiwani ni CUF.

  Baada ya mkutano mkuu wa april 19 chama cha TLP kitagawanyika mapande mawili. Wa Mtungirehi na wa dictator Mrema. The final nail on Mrema's coffin.

  Habari ndiyo hiyo.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Jul 22, 2015
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Tarariraaaaaa! Haya walokuwa wakinibishia wako wapi?... UKAWA chanu....maskini Mbowe anatapatapa kama nahodha wa Tatinic kujiokoa hawezi bora afe na chama..

  Wanaojiunga na Chadema toka CCM ni kundi la Lowassa ambao wameshajua hawatapata ridhaa ya CCM kugombea hata Udiwani. Lowassa na kundi lake lote limetemwa CCM hivyo msishangae kuona kundi la Nyumbu wakivuta mto Mara, marisho kule ng'ambo yamekwisha!
   
 19. N

  Non-Shatter JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2015
  Joined: Dec 2, 2014
  Messages: 598
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Wewe kweli taahira, angalia pumba ulizoandika hapa. Usirukie maneno ya vijiweni kwamba CHADEMA imeshindwa kuviunganisha vyama vya upinzani bila ya kuwa na ushahidi wowote ule bali uzushi tu. Ndiyo matatizo ya kuwa na elimu mulugo. Sasa kama wanaojiunga na chadema ni kundi lowassa iweje tena muanze kutumia vitisho dhidi yao kwamba watashughulikiwa kwa kutaka kukigawa chama, waachwe tu waongee chochote watakachopenda kuongea kuhusu uozo wa chama cha wahuni.

   
 20. M

  Mshika Bunduki Member

  #20
  Jul 22, 2015
  Joined: Jan 14, 2015
  Messages: 79
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Angalia hiyo Post ni ya mwaka gani
   
Loading...