Mbowe 'amjeruhi vibaya' Fuya Kimbita wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe 'amjeruhi vibaya' Fuya Kimbita wa CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Isaac, Oct 28, 2010.

 1. Isaac

  Isaac JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 627
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Wakuu habari za usiku?

  Jana niliwaahidi kuwaletea picha juu ya mikutano ya kampeni za Mbowe jimboni Hai mchana wa leo.

  Naomba mnisamehe kwa kushindwa kuziweka hapa kwani kifaa changu cha mawasiliano kinanitoa ushamba. Kama ilivyokuwa pale Arusha jana ndivyo ilivyokuwa hapa Hai ambapo Mbowe anashindana na mgombea wa CCM Fuya Kimbita.

  Katika hali ya kustaajabisha,wana wa nchi walipiga mayowe kila waliposikia jina la mgombea huyo wa ccm ambaye pia ni mbunge aliyemaliza muda wake.

  Katika kampeni hizo zilizotawaliwa na amani ya hali ya juu,Mbowe alifanya takribani mikutano 25 aliyoiita ya kusalimia wana wa nchi. Sehemu nyingi wana wa nchi walisikika wakimuita KAKA WA UKWELI na kumuahidi kumpatia madiwani wa kutosha kwani yeye ni mbunge tayari.

  Katika mikutano yake aliwataka wale wote wanaopenda ufisadi waichague CCM,Kama wanataka umasikini waichague CCM. Pia hakuogopa kuwaambia polisi waliokuwa wakilinda mikutano yake wasiache kuichagua CHADEMA.

  Wakati akitokea mji Mdogo wa Bomang'ombe, wana wa nchi walifunga barabara kwa takribani dakika 45 kwa lengo la kumsalimia Mbowe hivyo kuzuia magari yasipite hadi pale polisi wa FFU walipowasihi kupisha upande mmoja wa barabara.

  Nina picha nyingi tu ila nimeshimdwa kuziatach kwani niko mobile. Kama kuna mwenye uwezo wa kuziweka hapa JF,zinapatikana kwenye page yangu ya FACEBOOK ambayo ni Isaac 'Ankali' Babu. Video nitaziweka youtube.
   
 2. h

  hagonga Senior Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Heko wana wa hai kwa ujasiri wenu
   
 3. u

  urasa JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  senkyuuuuuuuuuu
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimekwenda facebook mbona nimezikosa? Nimekuta ile moja ya mama wa kibera anatoka kuchota maji!
   
 5. Mantissa

  Mantissa JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 870
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Singida mkoa maskini nao ubadilike jamani
   
 6. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2010
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Aika Mbee, Mangi Mbowe.!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Naomba aende kumsaidia Mgombea Ubunge wa Moshi Vijiji kwa tiket ya Chadema. Huyu Fuya Kimbita ni finished kabsaaaa.
   
 7. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu nimechungulia kwenye face buk yako yako sikuziona.
   
 8. Isaac

  Isaac JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 627
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Mchana wa leo mgombea ubunge wa jimbo la Hai kupitia CHADEMA na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho, mheshimiwa Freeman Mbowe,alifanya takribani mikutano 25 ya 'kusalimia' wana wa nchi.
  Katika mikutano yote Mbowe alionekana kumjeruhi kisiasa mpinzani wake ndugu Fuya Kimbita toka CCM ambaye pia ni mbunge aliyemaliza muda wake. Sehemu nyingi alizopita wana wa nchi walisikika wakimwita KAKA YETU WA UKWELI huku na yeye akiwatambua kama WASHIKAJI.
  Katika mkutano wa mwisho alioufanya pale mji mdogo wa Bomang'ombe, Mbowe alikusanya watu wengi kuliko hata Dr. Slaa na Jakaya Kikwete waliofanyia mikutano yao eneo hilohilo. Mbowe aliwahamasisha wana wa nchi kujitokeza kwa wingi Jumapili vituoni na kuwahakikishia kuwa kura hazitaibiwa na yeyote licha ya CCM kujinadi kuwa itashinda jimbo la Hai. Mbowe aliwaambia wananchi hao kuwa kuthibitisha kuwa kura haziibwi ameandaa utaratibu ambao itakapofika saa 4 usiku wa tarehe 31 atakuwa ameshayajua matokeo toka vituo vyote jimboni. Na atamtangaza mshindi kabla hata NEC hawajapata matokeo yote.
  Mbowe pia hakusita kuwaambia polisi waliokuwa viwanjani hapo kumchagua Dr. Slaa na Yeye(Mbowe) huku akishangiliwa na polisi hao kuonesha tabasamu.

  Kivutio katika kampeni hizo za amani Mbowe aliwaambia wana wa nchi kuwa Hai ilikuwepo kabla ya CCM na CHADEMA hivyo hamna haja ya kugombana kwani mwisho wa siku uchaguzi utapita na Hai itabaki.
  Pia barabara kuu ya Moshi- Arusha ilifungwa kwa takribani dakika 45 na wana wa nchi waliotaka kusalimiana na Mbunge wao. Ililazimu polisi wa FFU kuingilia kati na kuwasihi wana wa nchi kwa ustaarabu kuhamia upande mmoja wa barabara hivyo kupelekea magari yaliyokuwa yamesimama muda wote kuweza kupita.
  Hakukuwa na nyimbo wala maigizo ila katika vituo kadhaa vijana walikuwa wakionesha ufundi wa kuendesha pikipiki kwa mbwembwe huku wakimsubiri Mbunge.


  Wakuu nina picha nyingi za matukio ila nimeshindwa kuziweka hapa kwani niko mobile. Kama kuna anayeweza kuzipost hapa zinapatikana kwenye page yangu ya FACEBOOK ambayo ni Isaac 'Ankali' Babu. Video nitaziweka youtube.
  Naomba kuwakilisha.


  My take,
  CCM wametufanya kama karai la fundi ujenzi. Analithamini sana wakati wa kazi ila baada ya kazi analitupilia mbali.
   
 9. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu check kama hizo picture ziko huko kwenye face book, maana nimechungulia huko haskuziona
   
 10. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Fuys hata akipewa kura 20,000 bure toka kwenye rundo la Mbowe bado hawezi kushinda.
   
 11. M

  Mutu JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kweli kijana ajeruhi
   
 12. M

  Mutu JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
Loading...