Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,685
- 119,325
Wanabodi,
Nafulitilia kipindi cha maswali na majibu bungeni, Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe, leo amelipua bomu la siri ya ushindi wa CCM katika chaguzi za urais wa Zanzibar kuwa ni wizi wa kura, unaofanywa na serikali ya CCM, kwa kupeleka idadi kubwa ya askari polisi na askari jeshi Zanzibar kwa kisingizio cha kulinda amani na kuimarisha ulinzi, kumbe ni kwa ajili ya kuipigia kura CCM!.
Mhe. Mbowe amelipua bomu hilo, katika kipindi cha maswali na majibu bungeni, wakati alipouliza swali la nyongeza kwa Wizara ya Ulinzi, kuwa Jee wanajua kuwa askari jeshi kutoka bara, hupelekwa kwa wingi Zanzibar wakati wa uchaguzi ili kuipigia kura CCM?!.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dr. Hussein Mwinyi, alikanusha madai hayo kwa kujibu kuwa ni kweli idadi askari polisi na jeshi huongezwa Zanzibar wakati wa kukaribia uchaguzi mkuu, ile lengo la kuongezwa kwa idadi hiyo ya askari, sio ili kuipigia kura CCM, bali askari hao huongezwa ili kuimarisha usalama kwa kulinda amani na utulivu!. Dr. Mwinyi akasisitiza kuwa mtu hawezi kupiga kura Zanzibar kama sio mkaazi wa eneo husika!.
Wabunge kadhaa wakataka kuchangia hoja hiyo kwa kutokuridhishwa na jibu la Waziri, ila Spika Ndugai akauzima mjadala huo kwa kutoa amri ya swali linalifuata!. Mjadala huo ukafia hapo!.
Sasa huu ndio ukweli halisi kuhusu wanajeshi kuipigia kura CCM!.
Niliwahi kuwepo visiwani Zanzibar wakati wa uchaguzi mkuu. Kwa vile polisi na wanajeshi ni rais wa JMT kama raia wengine waWatanzania, pia wanayohaki ya kupiga kura kumchagua rais wa JMT popote walipo. Wakati wa Uchaguzi Mkuu, polisi na wanajeshi wanaruhusiwa kupiga kura kituo chochote walichopangiwa kwa ulinzi.
Kitu ambacho Dr. Mwinyi anakijua na ila hakukisema bungeni kuhusu wapiga kura wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar, hakusema kuwa kuna vituo maalum vya kupigia kura katika makambi ya majeshi, vituo hivyo ni mahsusi ni kwa ajili ya askari polisi na wanajeshi tuu au kambi za polisi. Vituo hivyo havina mawakala wa vyama, havina masheha wa kutambua wakaazi, wala waangalizi wa uchaguzi huwa hawaruhusiwi kuvitembelea!, na kushuhudia zoezi la upigaji kura katika vituo hivyo!, na hapa ndipo (kwa maoni yangu), ndipo yale makarateka ya zisipotosha zitatosheshwa yanakofanyika!.
Matokeo ya vituoni yanaweza kuonyesha CUF wameshinda kwa mujibu wa hesabu ya mawakala wa vituo vyao vyote zilizosainiwa na mawakala wa vyama vyote, lakini matokeo ya ZEC yataonyesha CCM imeshinda kutokana na kujumlishwa kura za vituo hivi maalum vya makambi ya jeshi!.
Natoa wito kwa CUF, kutosusia uchaguzi wa marudio wa Zanzibar, ila ili kuthibiti kua hizi za wizi, kuhakikisha matangazo yote ya matokeo ya uchaguzi kwa mujibu wa ZEC, yaandamane na scanned Copies za matokeo halisi ya kituo kwa kituo zenye saini za mawakala wa CUF, hivyo zikija hizo karatasi za vituo maalum, watasibaini kwa sababu watakuta hakuna saini za mawakala wao, na scanned copies hizo CUF wao hawatakuwa nazo!.
Mazingaumbwe ya bao la mkono linaweza kufanikiwa kwa tactics na playing with numbers, only lakini CUF wakijizatiti kwa kuingia na ndimu kwenye onyesho hilo la mazingaombwe ya uchaguzi, itafikia wakati, hata the greates magicians, can run out of tricks!.
Nawatakia uchaguzi mwema wa marudio wakazi wa visiwa vya Zanzibar na Pemba na vitongoji vyao.
Pasco