Mbowe: Alichowasilisha Wenje ni Msimamo wa Kambi ya Upinzani

hamna kinga kwa yeyote anayelihujumu taifa, katiba ya nchi yangu haisemi hivyo, labda katika ardhi inayoongozwa na genge la kihuni kama rwanda ulikokukimbia
wanaoihujumu nchi yetu ni wale wanaolazimisha kuingiza nchi yetu kwenye uadui usio wa lazima na majirani zetu!
 
Chanzo cha mgogoro huu ni nini?.... KIKWETE KUSHAURI MAZUNGUMZO! sasa unalaumu kitu gani? Lawama zote hapo juu zinatakiwa kuelekezwa kwa KAGAME! ambaye yeye kashauriwa kuzungumza na maadui zake, anatishia kutupiga!
kwanza kama ametishia kutupiga kwa nini tusijiimarishe zaidi kijeshi? Badala ya kupeleka viko congo? Mkuu weka ushabiki pembeni, serikali yetu ijiangalie upya katika hili...
 
kwanza kama ametishia kutupiga kwa nini tusijiimarishe zaidi kijeshi? Badala ya kupeleka viko congo? Mkuu weka ushabiki pembeni, serikali yetu ijiangalie upya katika hili...

kwa hiyo yeye kagame congo inamhusu nini? kwa nini alalamike kwa sisi kwenda congo kama yeye sio M23? kumbe unafahamu kuwa M23 ni Rwanda na kuwa TZ tumemchapa!:)
 
Kijana unatatizo kubwa,nikupe historia fupi wanachokifanya cm na adhari yake,
Mwaka 1978/9 tulikuwa na uhusiano mbaya na Uganda,sababu kubwa ni nchi ya uganda kuwa na rais dikteta aliyepindua serikali halali ya chama kilichowekwa madarakani na wananchi.
Rais wa marekani George w ,Bushmtoto aliitangazia dunia kuwa iraq imeficha siraha za maangamizi hivyo lazima ipigwe,
Kwa kiburi cha jeshi la kisasana uchumi mzuri alioacha mtangulizi wake akapeleka jeshi likawaua wananchi wa iraq,kilichotokea ni nchi ya marekani kukosa ushirikiano na mataifa ya mashariki ya kati.
Kwa ulevi tu wakukosa sayansi ya diplomasia alisababisha dunia ijue kuwa anapambana na uislamu.kwa ulevi huo,Uingrreza chini ya Tony Blair eaziri mkuu wa uingereza na waziri mkuu wa Australia aliingia vitani,baada ya vita bunge la uingereza maarufu( house of common) ,likisaidiwa na wataalam wa kimataifa,mossad na cia wakagundua kuwa ulikuwa ujanja wa yeyr kwenda kuvuna raslimali ya mafuta tu,Blair akanyang'nywa madaraka
Kwa sauti ya baba wa Taifa,mwl Jk Nyere alisema kuwa mwaka 1967, kuwa Tanzania haiko salama kama haitakuwa na mahusiano mema na nchi majirani kwani maadui watapitia huko,ndio maana wanyareanda walikuwa kaka na dada zetu,uganda,kenya,malawi,msumbiji,na nchi zote za kusini mwa Afrika tulikuwa marafiki,
Cha kuahangaza ni miaka ya sasa tunaanza kuhitilafiana na majirani zetu kiasi cha kusema hatuwezi kuwatetea wala kula nao sahani moja kulikoni( partriotism of the country is how you fell to any risc of your fell gets), chadema waneonya
Serikali hii imepoteza sera yake yakutofungamana na upande wowote,serikali hii imepoteza Azimio la Arusha, no committment ,hata inaposhauriwa na waziri wa kamvi rasmi ya upinzani umuhimu wa kutake conscience haitaki?, msituingize kwenye migogoro we need Rwanda,we berd our mother father ,sister & daughters! Chadema wameonyesha njia ifuareni acheni blaa za siasa za alinacha,tengeneni fedha za Economic diplomacy kama wenzenu USA,china,japan& India!, akili ni nywele.......

Hakuna point hapa. Hakuna. Mbona hujatueleza chanzo cha vita ndani ya DRC na athari zake kwa TZ? Nani kakufundisha kwamba kutofungamana na upande wowote maanake kutolinda maslahi ya nchi? Nani kakufundisha kwamba kutofungamana na upande wowote manake kutoomba pande zinazotofautiana kufanya mazungumzo kama ilivyopendekezwa na JK?

Ni wapumbavu wa jinsi ya Wenje watakaa kimya juu ya athari za vita ndani ya DRC kwa TZ. Sambamba na hilo kuna wajinga wanaodhani kwamba TZ tunatakiwa tuwe na marafiki tu na sio adui. Eboh, wewe unayesoma post hii huna maadui au watu unaotofautiana na kwasabau za msingi? Kwanini unadhani Tz tuwe na marafiki tu? Kama nchi gani? Siasa za nje zinahushisha kutengeneza rafiki na adui kadhalika.

Tuache ujinga na badala yake tuungane kuhakikisha vita ndani DRC inakwisha na hivyo kulinda usalama wa raia wetu mipakani.
 
Mashariki ya Congo. Watoto hawa hawakuwa wakipata nafasi kufurahi kwa pamoja. Baada ya kazi nzuri ya Monusco sasa hawana mashaka.
 

Attachments

  • 1401279135847.jpg
    1401279135847.jpg
    103.5 KB · Views: 47
Vijana ambao walipata madhara ya kukatwa miguu na waasi Wa m23. Wakicheza mpira baada ya hali ya utulivu kuaanza kurejea.
 

Attachments

  • 1401279339478.jpg
    1401279339478.jpg
    86.8 KB · Views: 47
kwa hiyo yeye kagame congo inamhusu nini? kwa nini alalamike kwa sisi kwenda congo kama yeye sio M23? kumbe unafahamu kuwa M23 ni Rwanda na kuwa TZ tumemchapa!:)
mkuu vita sio jambo la kufurahia, usiweke ushabiki hapa, kwani kila wanachokifanya rwanda na sisi lazima tufanye? Kwa nini tusiwasaidie congo kwa kidiplomasia?
 
kwahiyo wewe moto ukiwaka kwa jirani hauendi kusaidia kuzima kwasababu haukuathiri wewe!? Shame on you chadema!!! Hamjui hata maana ya uhusiano na ushirikiano wa kimataifa!
Kwa hiyo kulinda uhusiano na jirani ni kupeleka majeshi na kuwaua wote wanaopingana na jirani yako?
 
Kwanza,Nampongeza Waziri Wa Mambo ya Nje Bernard Membe kwa kukubali kuwa kuna haja ya kuwa na wataalamu wa uchumi kwenye Balozi zetu nje ambao wamebobea katika Diplomasia ya Uchumi .Hili suala nimeshaandika hapa mara kadhaa,nimeaandika JF na Pia makala kwenye magazeti.Ni hatua nzuri sasa kama Wizara imetambua umuhimu wa kutumia Balozi Zetu kuvutia watalii ,kuhamasisha Biashara kati ya Watanzania na watu au makampuni ya Nje na pia kuvutia wawekezaji (Foreign Direct Investment).Sasa tumeanza kwenda na wakati ingawa tunahitahi Sera yenye strategic focus kwa EAC,SADCC,AU,ARAB LEAGUE,ASIA,CHINA ,US n.k kama Potential Partners. Uingereza,Kenya,SA,China na US ni strategic partbers katika Uwekezaji.Hapa ni lazima tufanye formulation ya Unique Policy ili hata wanadiplomasia wetu waongozwe na Framework Specific

Pia Economic Intelligence Unit au Think Tank iundwe na iwe na Coordination ya Moja kwa Moja na Department ya Economic Diplomacy.kwa bahati mbaya Wabunge hawakumbana katika Eneo hili.Diplomasia ya sasa ni ya Uchumi na sio Diplomasia ya Kisiasa tena. Leo tunatuma wanasiasa wakatuwakilishe kule Doha kwenye Mikutano ya WTO wakati Wenzetu wanapeleka mabingwa mbinu za majadiliano ya kibiashara na Uchumi kutoka kwenye Economic Intelligence Unit zao

Pili,jana nilitahadharisha juu ya matamshi ya Mbunge Kessy kuhusu yeye kuituhumu Rwanda na nikasema alikosa weledi unaohitajika katika majadiliano ya mijadala ya kidiplomasia ndani ya bunge na nikaonyesha masikitiko yangu kwa Mhe.Bernard Membe kushangilia kauli ya Mhe.Kessy kuwa Rwanda inaiba Raslimali za Congo-DRC na pia inafadhili M-23.

Well,Nilisema Kessy ametuhumu (Hata kama ni Kweli) bila kufanya Rejea .Nikasema labda Membe aje afanye Rejea ya Ripoti ya UN lakini nikatahadharisha kuwa hata akifanya hivyo lakini Rwanda hajaadhibiwa.

Kweli Mhe.Membe alikuja kumsaidia Kessy kwa kufanya Rejea ya Ripoti ya UN na kutumia flirtiring Skills akidhani kuwa anamshambulia msemaji wa kambi ya upinzani.

Membe alichofanya ni makosa makubwa kidiplomasia na hili litachochea mgogoro mkubwa na Rwanda.

Je,Kauli alizotoa Kessy au Membe kuwa Rwanda ni Wezi na M-23 ni kundi la Serikali ya Rwanda,Rais Kikwete anaweza kuzitamka kwenye Mkutano wa EAC,SADCC,ICGLR,AU Au Kule UN General Asswmbly? Waziri mkuu Pinda aliyelitangazia Bunge Mwaka jana kuwa Serikali imemuomba Rais Museveni wa Uganda awapatanishe Kikwete na Kagame alimaanisha nini?Kwamba Rais angefuta kauli yake ya kumshauri Kagame kuongea na FDLR?Vipi mbona Ripoti aliyoinukuu Membe Bungeni pia imeituhumu Uganda kuwa wanashirikiana na Rwanda kulifadhili Kundi la March-23 Movement(M-23)? Siis wengine tulipinga tangu Mwanzo Uganda kuhusishwa maana kama ni confidence ya Mediator sidhani kama Tanzania ingekua nayo kwa Museveni na tena ningeshangaa sana.

Tanzania tumeonyesha kutokua na ajenda kimataifa na nimeshasema mara nyingi tunafuata sera ya fuata mkumbo (Bandwagoning Diplomacy).Tupo tupo tu na tunadandia kila kitu halafu tunasema tunaheshimika sana kimataifa?

Hiyo nguvu ya usuluhishi unaitoa wapi wakati huu wa sera ya Diplomasia ya Uchumi ambako nguvu ya uchumi na kijeshi ndiyo inayokupa nguvu katika medani za kimataifa ikiwepo usuluhishi? Marekani wakisema Usalama wanamaanisha nguvu ya kiuchumi. Nigeria baada ya Rebasing ya uchumi wao imekua taifa lenye uchumi mkubwa Afrika na hivyo nguvu ya taifa na sauti yao itaheshimika

Kenya wanatupita katika nguvu na sauti kimataifa katika ukanda huu kwa sababu ya nguvu ya kiuchumi na sisi tunaendelea kutumia ile akiba ya Diplomasia ya siasa za Frontline aliyoacha Mwalimu Nyerere

Sasa Ripoti ya Mhe.Membe iliyoandikwa na UN Expert Group ilipingwa na Rwanda,pia Ripoti hiyo ilipingwa na Uganda maana hata Uganda walituhumiwa lakini Membe kwa upotoshaji Mkubwa hakuitaja.

Ni jambo la ajabu kuwa Top Diplomat wa Nchi anashindwa kuzingatia kuwa Tayari Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilishaidhinisha Vikwazo kupitia Azimio namba 2136 (2014) ambalo liliungwa mkono na Rwanda kwa mtazamo wa kuwa Azimio namba 1533(2004) lilotanguliwa na Azimio 1494(2003) linaheshimiwa

Azimio namba 2136 liliweka Vikwazo kwa M-23(Bila kuitaja Rwanda katika Adhabu hiyo) na pia Congo -DRC waliadhibiwa kwa kuifadhili UFDLR ambayo pia ilitajwa na UN report aliyoitumia Membe

FDLR wana extrime Ideology iliyohusika na Mauaji ya Kimbari ya Rwanda na ilithibitishwa na UN Security Council.

Haya Membe hakuyajadili wakati Bunge lilihitaji mjadala ili nchi yetu iangalie namna ya kuwasaidia majirani zetu,pia tudumishe amani,mahusiano ya kidiplomasia hasa ya kiuchumi na pia kulinda mtazamo mpana wa umajumui wa Afrika

Membe alichagua Kufanya siasa kiduchu(Petty Politics) kumshambulia Wenje binafsi(Personal Attack) kinyume na weledi wa Diplomasia na pia kutoa matamshi yatakayochochea mgogoro zaidi baina ya Tanzania na Rwanda kwa kuituhumu Rwanda kuifadhili M-23 huku akijua kwa sasa kulingana na azimio 2136 Nchi wanachama wa ICGLR(Nchi za Ukanda Maziwa Makuu) zina jukumu la jumla na binafsi katika kusaidia kutekeleza maazimio hayo ikiwa ni pamoja na kushirikiana na UN Expert Group iliyopewa Mandate ya kurefusha Sanction Regime hadi February 1,2015 ili kuleta amani ya Kudumu

Waziri wa Mambo ya Nje kupotosha mjadala na kutuhumu kuwa Msemaji wa Kambi ya Upinzani anatumiwa na Mataifa ya Nje (Pengine Rwanda) ni udhaifu mkubwa katika kukwepa hoja .Kama kuhoji kuhusu tuhuma za Rais Kukutana na Kiongozi wa Waasi(Tena Sio Upinzani) basi inamfanya Wenje kuwa Mamluki anayelipwa na Rwanda kuisemea ndani ya bunge ,Je ni wapi Duniani tuliwahi kuona Rais Wa Nchi kulisemea na kulionea huruma kundi la Waasi? Membe hakupima Kauli zake

Ni mwaka jana tu Membe alitoa matamshi tata kuhusu kutengwa kwetu kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na kudai "tunasubiri Talaka".Tuliipinga kauli hii na kwa bahati nzuri Rais Kikwete aliliona hilo na akatoa hotuba nzito Bungeni kuwa hatuendi Popote.

Mimi ni mzalendo ninayelipenda Taifa langu na nitalipigania popote duniani.Sipendi Blind Patriotism.

Kagame ana matatizo yake ndani ya Rwanda lakini hatuwezi kuruhusu kauli aliyoitoa JK kuwa Rwanda Iongee na Waasi(Kauli ambayo nikiiunga mkono na naendelea kuiunga mkono) itumike kuhatarisha mahusiano yetu na watu wa Rwanda au Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kauli za Mawaziri ambazo wanazitoa bila kipimo

Pia suala la Majeshi yetu kule Congo DRC lipo na ni sehemu ya Tanzania katika kutimiza majukumu yake ya kimataifa(International Obligation) kupitia Azimio no.2098 la kuunda MONUSCO.

Hata hivyo halizuii mijadala bungeni maana hata Obama aliposema "Dumb War" ilikua ni matokeo ya mjadala ndani ya Congress kule US kuhusu Rais Bush kulidanganya Taifa kuwa Iraq ina silaha za Kemikali kumbe ni Uongo.Marekani ilipata hasara.

Ni lazima kuwe na mjadala bungeni kwa kukosoana na kurekebishana ili tuunde mwafaka wa kisera kama nchi tusonge mbele.Waziri alikosa weledi juu ya matumizi ya Code Words and Politeness

Unachagua kujadili millitary adventure huko DRC halafu unashindwa kutoa majibu ya kushindwa kwa Serikali kutuma Millitary Plane kufanya Evacuation hata ya Raia wetu kule Sudan Kusini wakati wa Vita? Kwanza nampongeza Membe kwa kukubaliana na ile Hoja yangu ya jana kuwa Tanzania imezubaa na wizara haina takwimu ya idadi ya Raia wa Tanzania nje hivyo hata mikakati ya kunufaika na Diaspora ni lazima tutatue changamoto hii kwanza

Tatu,Membe Alishangaza kwa kutetea ziara za Rais nje .Rais amefanya ziara zaidi ya 365 nje ya nchi kushinda Mwalimu Nyerere ambaye hakufikisha ziara 70 kwa kipindi chake cha miaka 24 madarakani.Rais anataka kuwa Member wa Diaspora?Maana ameshinda angani na nje ya nchi kwa sababu dhaifu kabisa kabisa.

Membe anatoa sababu dhaifu kuwa Rais anapendwa na kuheahimika,Je kati ya Rais Kikwete na Mwl.Nyerere ni nani alikua akiheshimika zaidi kimataifa?

Rais anashindwa kubaki nyumbani na kudhibiti wizi wa mali za umma kama bilioni 200 za ESCROW kwenye sakata la IPTL badala yake anaenda kuomba bilioni 40 au 100 nje ya nchi tena sehemu nyingine kama Singapore anapokelewa na mkurugenzi wa Idara kinyume na Itifaki kabisa?

You can't defend the trip maniac president in that way

Ifike Mahali sasa kwenye Katiba tudhibiti ziara hizi kama Mexico ambako Rais Vicente Fox alionja fedheha hii kwa kuzuiwa na Bunge lake la Senate mara Mbili Kusafiri ikiwepo ziara yake US na Canada.Safari za Rais ilikua ni lazima zipate approval ya Bunge. Chama cha Upinzani cha PRI kilizuia safari zisizokua na Tija.

Mexico walipata dawa ya kudhibiti Marais ambao ni wazururaji utadhani wamelelewa kwa supu za usafiri(Makanyagio) ya kuku wa kienyeji. Balozi za nje na hata wizara zinaweza kufanya baadhi ya safari na kupunguza gharama.

Hatuwezi kuegemea kwenye ziara za Rais katika Diplomasia ya Kuomba na Kushukuru badala ya kuweka Diplomasia ya Uchumi.Tunahitaji kudhibiti ziara za Rais kikatiba kabisa na safari zipate Approval ya Bunge kama Mexico. How can we justifty global trotting to seek aid and loans while we cant protect our Cash reserves?
 
Wadau, katika hali ya kuonesha kuwa CHADEMA wamedhamiria kumtetea Kagame na Rwanda, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe amesema kuwa alichowasilisha Ezekiel Wenje ni msimamo wa Kambi ya Upinzani.

Tahadhari, Ikiwa CHADEMA wameamua kushirikiana na Rwanda dhidi ya Tanzania, kuna haja ya kila Mtanzania kulaani huu uasi unaofanywa na CHADEMA na kuna haja pia ya vyombo vya dola kufuatilia kwa karibu nyenendo za viongozi wa CHADEMA

sio bure unagege...dwa
 
Ni aibu sana kwa chama cha siasa kuungana na waasi[/QUOTE

Ninahisi kama tunahitaji kuwa na uelewa mpana juu ya kinacho ongelewa kuhusu Rwanda na DRC. Hivi ni kweli kuwa wanachotueleza viongozi wa serikali yetu ni sahihi! na kama ni kweli ni sahihi, basi tunahita kujua mambo mengi kuliko tunayoambiwa. Hata kama ni kweli kuwa M23 ni ya Rwanda, majeshi yetu yapo DRC kwa masilahi gani? Na kama si kweli, ni kwa nini serikali itumie nguvu na pesa nyingi kuisaidia DRC? Huenda kambi ya upinzani imejua majibu ya haya na mengine mengi ndio maana wamefunguka tulivyosikia. Swala la kuwa wanamuunga mkono Kagame au la si la kukimbilia kama tunavyo jaribu kufanya huenda likatutoa kwenye kujua ukweli.
 
Wadau, katika hali ya kuonesha kuwa CHADEMA wamedhamiria kumtetea Kagame na Rwanda, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe amesema kuwa alichowasilisha Ezekiel Wenje ni msimamo wa Kambi ya Upinzani.

Tahadhari, Ikiwa CHADEMA wameamua kushirikiana na Rwanda dhidi ya Tanzania, kuna haja ya kila Mtanzania kulaani huu uasi unaofanywa na CHADEMA na kuna haja pia ya vyombo vya dola kufuatilia kwa karibu nyenendo za viongozi wa CHADEMA
....kwa hiyo wewe unataka watu wote wafikirie swala la congo na hao waasi kama ambavyo gazeti lako la jambo leo linavyoandika???wakati mwingine fikiria nje ya boksi,zimekamatwa meli hapa zinavua katika ukanda wetu kitu gani kimetokea??imekamatwa meli hapa ikiwa na shehena ya meno ya tembo,kitu gani kimefanyika??wametajwa hapa magwiji wa bishara ya madawa yakulevya na jamaa ako mkubwa kasema anayo majina,kitu gani kimefanyika??wametajwa hapa mafisadi jamaa ako mkubwa anawajua,kitu gani kimefanyika??sasa kama katika mswala yako ya ndani unashindwa kuwa na maamuzi chanya yasiyo na makengeza,kwa nini utuaminishe kuwa Rwanda ndo inahusika na hiko kikundi kama wewe haujatumiwa na congo kuchafua rwanda ili ufaidike kwa malipo flani...nacha kujiuliza hapa,inakuwaje gazeti moja tu la jambo leo ndo kila siku linaandika habari ya kagame???
 
mkuu vita sio jambo la kufurahia, usiweke ushabiki hapa, kwani kila wanachokifanya rwanda na sisi lazima tufanye? Kwa nini tusiwasaidie congo kwa kidiplomasia?

Kagame alichotaka ni kumega DRC, tayari M23 walikuwa wanataka eti kura ya maoni ili maeneo ya kivu yawe nchi huru, hapo ni baada ya kusambaratisha vijiji vya wacongo. Kura zingepigwa na hao watutsi halafu guess what, baada ya uhuru ingeungana na Rwanda, kesho yake tena wanaanza moja kumega eneon lingine, hilo ndilo lilikuwa lengo lao.
kwa hiyo ujanja wao ulikuwa kujifanya wanataka maongezi huku M23 waachiwe kufanya wanavyotaka, huu ni upuuzi, hivi unakumbuka M23 baada ya kuteka goma nzima walitaka kwenda kinshasa kuchukua nchi nzima? Sasa baada ya kupigwa na monusco hebu niambie kale kakikundi ka M23 kalikuwa kanaungwa mkono na nani hapo DRC? nobody!
 
haa haa, kwa hiyo raia wasio na hatia wanakufa congo tu? Je wale mnawaua kwa mabomu kwenye mikutano ya wapinzani vip? Je wale wanaouawa na Boko haramu pale nigeria vip? Je wale wanaokufa somalia je? Acheni unafiki mainterahamwe!
kosa moja halihalalishi kosa lingine.
 
Wewe ndo una upeo mdogo wa kuelewa na inaelekea umekurupuka tu kuchangia

dogo unahangaika sana aisee

hivi una muda hata wa kuwaza mambo ya maana kweli??

it seems like you are becoming a total dumba$$
 
Back
Top Bottom