Decree Holder
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 2,556
- 3,741
Ndugu wanajamvi salamu kwanza!
Ikiwa ni mapema mwakani chama chetu CHADEMA kitaingia kwenye uchaguzi wake mkuu utakaohusisha ngazi zote za uongozi wa chamoa.
Sina shida na nafasi zingine za uongozi ndani ya chama chetu bali nafasi ambayo imekuwa ikiishughulisha akili yangu kwa sasa ni nafasi ya juu ya chama yaani Mwenyekiti.
Huenda wanachama wengi tungependa kuona mabadiliko katika nafasi hiyo kubwa ndani ya chama baada ya kukaliwa na mtu mmoja kwa muongo na miaka minne sasa.
Swali la mjadala ni je ni nani mwenye uwezo ndani ya CHADEMA wa kuvivaa viatu vya Mbowe vikamtosha? Nani mwenye uwezo huo mkubwa ambaye ataweza kukivusha chama, sifa zake ni zipi na ana uzoefu upi.
Ndugu zangu nimeileta hii mada ili tukisaidie chama hiki kikuu cha upinzani nchini. Tutakuwa hatutendi haki kama tutakuwa tunalaumu kutokufanyika mabadiliko katika nafasi hiyo kubwa wakati hatutoi mbadala wa kile tunachotaka kibadilike.
Ikumbukwe kwamba mabadiliko sahihi ni kutoka sehemu moja kwenda sehemu bora zaidi swali ni nani unayemuona bora ndani ya CHADEMA atakayeweza kuvaa viatu vya Mbowe?
Nahitaji hoja siyo matusi na kejeli.