Mbowe akamatwa na polisi na kuhojiwa kwa dk 15... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe akamatwa na polisi na kuhojiwa kwa dk 15...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Dec 12, 2011.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mbunge wa Hai (Chadema), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, jana alishikiliwa na jeshi la polisi kwa takribani robo saa kwa mahojiano baada ya kupiga fataki katika maadhimisho ya miaka 50 ya kuzaliwa kwake bila kuwa na kibali cha kupiga fataki hizo.

  Tukio hilo lilitokea majira ya saa nne usiku katika ofisi za Hai Kilimanjaro Development Initiative ambapo alifanya tafrija ya kujipongeza kwa kutimiza miaka hiyo ya kuzaliwa kwake na ndipo askari walipofika na kumchukua kwa ajili ya mahojiano.

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya jeshi la polisi, ni kwamba mbunge huyo alifanya hivyo kinyume na taratibu na pasipokuwa na kibali kutoka kwa jeshi hilo.

  Taarifa hizo zilieleza kwamba baada ya kuhojiwa kwa muda, Polisi walimwachia.

  Kwa upande wao, wananchi waliozungumza na NIPASHE, walilaani kitendo cha polisi kumkamata mbunge huyo na kusema kuwa ni kumnyanyasa kisisasa na kumyima uhuru wa kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.

  John Mbowe na Mama Salama, waliliambia gazeti hili kuwa kitendo hicho ni cha kumdhalilisha na kulidhalilisha jeshi hilo kutokana na ukweli kuwa kupiga fataki tena katika maeneo ya wazi si kosa na kuongeza kuwa wapo watu wengine wamekuwa wakipiga fataki na hawakamatwi.

  Kwa upande wake, Mbowe hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo kutokana na kuwa na shughuli nyingi ambapo alikuwa akielekea kwenye harambee ya kuchangia upanuzi wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), usharika wa Nshara.

  Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi wilaya ya Hai, Revocatus Malin ili azungumzie tukio hilo, ziligonga mwamba kutokana na kutokuwepo ofisini wakati Kamanda wa polisi mkoani hapa, Absalom Mwakyoma hakupatikana kwenye simu yake ya mkononi.

  Source:
  Nipashe

   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaani polisi wa tanzania ni matapishi matupu..wanaaacha ku deal na mambo ya msingi wanahnagaika na vitu kama hivi
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  he! Mbona mi napigaga fataki hawajawahi kunikamata?
   
 4. P

  PreZ 2B EL Member

  #4
  Dec 12, 2011
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ina maana polisi walikuwa wanalinda hiyo sherehe au walikuja baada kusikia fataki
   
 5. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #5
  Dec 12, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hizi tunazopigaga kuukaribisha mwaka mpya mbona hatukamagwi???!!!
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Dec 12, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  wangekua wanafanya hivyo kwa kila mtu basi wangekamata wahindi wote wa kwa kubutua mafatakaki,
   
 7. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #7
  Dec 12, 2011
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Usiku huo ndio alikuwa anaenda kwenye harambee?
   
 8. S

  Stephen Kagosi Member

  #8
  Dec 12, 2011
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kamanda wa ukweli lazima apitie misukosuko........na tusiwalaumu polisi tatizo katiba inaelekeza watii amri zote zinazotolewa na wakubwa...wameamriwa na mkubwa sasa waache kibarua kiote nyasi.....
   
 9. matungusha

  matungusha JF-Expert Member

  #9
  Dec 12, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hawa polisi hawakusoma makala ya mwigamba nin? wapumbavu hawa vibaraka wa ccm!!!
   
 10. I

  Imurumunyungu Senior Member

  #10
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shule jamani shule qualification ya police ni PRIMARY LEVEL of education.Kwa hiyo wengi wao ni zero brain,huwa wanafikiriwa na watu wengine.Msiwalaumu ni ma mbumbu ndo maana kila wanachoagizwa wanafanya kiwe kizuri au kibaya.
   
 11. Chief Isike

  Chief Isike JF-Expert Member

  #11
  Dec 12, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Walikuja baada ya kusikia fataki. Walikuja katika gari nne. Tatu zikijaa FFU, mbili zilifichwa sehemu moja, moja ikafichwa sehemu nyingine, kisha moja ikaja kusimama getini, ambapo OCCID na wengine kadhaa waliokuw ana silaha, waliingia ndani, huku bosi wao, OCCID, akimwomba na kumsihi sana Kamnda Mbowe wakati anatoka kituoni apitie Polisi ili aandike maelezo juu ya upigaji fataki, tehe tehe tehe. Polisi wetu bana!
   
 12. Chief Isike

  Chief Isike JF-Expert Member

  #12
  Dec 12, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Walikuja baada ya kusikia fataki. Walikuja katika gari nne. Tatu zikijaa FFU, mbili zilifichwa sehemu moja, moja ikafichwa sehemu nyingine, kisha moja ikaja kusimama getini, ambapo OCCID na wengine kadhaa waliokuw ana silaha, waliingia ndani, huku bosi wao, OCCID, akimwomba na kumsihi sana Kamnda Mbowe wakati anatoka kituoni apitie Polisi ili aandike maelezo juu ya upigaji fataki, tehe tehe tehe. Polisi wetu bana!
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,554
  Likes Received: 1,902
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye bold kuna contradict story nzima.

  Walienda na gari nne na wakamwomba akitoka kituoni apitie polisi?

  Kituoni ni wapi na polisi ni wapi?

  Rekebisha ueleweke basi...
   
 14. Chief Isike

  Chief Isike JF-Expert Member

  #14
  Dec 12, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Labda tunaweza kusaidina maana hasa ya Polisi kumkamata mtu na kumshikilia. Askari walikuja katika eneo la hafla, kama alivyoripoti mwandishi baada ya kusikika kwa milio ya fataki. Hoja yao kubwa ni kwamba hazikuombewa kibali. Hivyo wakawmomba John Mrema, mmoja wa wakurugenzi wa CHADEMA awasaidie kumwita na kumpata Mheshimiwa Mbowe. Askari kadhaa wakiw ana bunduki wakaingia ndani ya 'ukumbi'. OCCid akafanikiwa kuzungumza na Mheshimiw aMbowe. Wakamwomba baada ya sherehe apitie kituo cha polisi, aandikishe maelezo yake juu ya suala la milio ya fataki.

  Polisi wale wa ajabu. Walikuja katika gari nne, tatu zimejaa 'FFU', moja ndiyo ikaja na kusimama getini, ambamo wale askari wenye bunduki, wakiongozwa na OCCID walikuwemo.

   
 15. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #15
  Dec 12, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa ana matatizo ya akili. Masuala madogo tu, anataka polisi wamsukume ili atoe tamko. Alishindwaje kwenda kutoa taarifa polisi?
   
 16. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #16
  Dec 12, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  duh mzee utakuwa wa udom wewe maana mna akili sana nyie, vipi upo lkn?? Kitabu kinaendaje?? Kama kawaida yako lazima utoke na pum******a zako, aya bana wawakilishe vilaza wenzako, alamsiki mkuuu.... Log off
   
 17. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #17
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Stupid! Wana jf hv mnaona h kinyaa hapa?
   
 18. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #18
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  hivi hawa polisi kama wangepata bahati ya kutembelea china mbona wangewakamata wachina woooooooooooote
  maana hawa jamaa fataki zinalipuka kama mabomu,kila wafunguapo ofisi mpya ni lazima zipigwe fataki za nguvu,lakini pia ifikapo mwakampya serikali huwashughurikia wale wote ambao hawakupiga fataki ktk kusheherekea mwaka mpya baada ya kipindi cha barii kuisha

  sasa bongo nchi masikini kupiga fataki nayo ni issue tena,imekuwa ni dili tena kukamatana,duuuuuuuuuuuuuu ni hatari kweli
   
 19. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #19
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ni ajabu sana maana uhindini wanapiga kila wakiwa na shamrashamra wala hawatoi taarifa...mimi nimekaa sana maeneo ya uhindini !
   
 20. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #20
  Dec 13, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Acha wewe, hakuna anaeshughulikiwa kwa kutokupiga fataki. Ni hiyari ya mtu kusheherekea kwa kupiga fataki, na ni utamaduni wao wa mwaka mpya wao, bila fataki mtu hajisikii kama kashererekea, lakini si sheria...duh
   
Loading...