Mbowe ajiuzulu mwenyewe la sivyo nitamshitaki Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma

Benson Mramba

JF-Expert Member
Oct 29, 2013
644
1,482
Miaka yote tangu 2017 nimekuwa nikisema kuwa uwezo wa Mbowe kuiongoza CHADEMA ulikuwa umefikia mwisho kama kiongozi.

Nilisema sababu kubwa ni washauri wabovu, wenye uwezo mdogo wanamzunguka Freeman Mbowe. Niliwataja washauri hao kuwa ni Lema, Msigwa, John Mrema na Reggy Munisi. Nikasema CHADEMA inaharibiwa na kakikundi cha watu wasiozidi watano wakati ule. Watu hawakunielewa wakadhani nina chuki binafsi.

Jana yametokea makubwa kabisa kabisa ya kiongozi Mkuu kusema uongo hadharani kwa taifa, kulewa kupita kiasi mambo ambayo ni ukosefu wa maadili kwa kiwango cha juu kabisa kwa kiongozi wa ngazi yake.

Mimi nina maslahi makubwa na CHADEMA kama Mtanzania ninayependa upinzani na niliyepoteza muda wangu mwingi na rasilimali kuijenga CHADEMA na upinzani. Hivyo siwezi kumuacha Mbowe na kikundi chake wauvuruge upinzani nchini na CHADEMA.

Ninamtaka Mbowe, Kamati Kuu ya CHADEMA, Msajili wa vyama na kila anayehusika kumtaka Mbowe ajiuzulu kwasababu amekosa maadili na hana nia njema na CHADEMA wala Taifa letu la sivyo nitampeleka kwenye TUME YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA na ikilazimu Mahakamani.

Naomba kila Mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi hii aniunge mkono. Haya ni maamuzi yangu mwenyewe nikiwa na akili timamu bila kushinikizwa na mtu yoyote.

Naomba kuwasilisha
 
Sasa hapa leo ndio tutaona mapungufu makubwa ya siasa zetu, wanasiasa na vijana wasomi wa kitanzania waliosomeshwa na kodi zetu sisi wakulima.

Hatakuja mtu kuthibitisha kwamba mimi nilikwenda kumuona mbowe hakuwa amelewa wanamsingizia tu, watu watakuja na matusi na vioja vya kila aina.

Nchi hii tumepata uhuru kutoka kwa mkoloni tu, lakini uhuru wa kisiasa bado. Maana watu hawawezi kuhoji, kuuliza wala kudadisi chochote ndani ya chama, ukiuliza unakuwa msaliti, unabezwa na unakuwa adui namba moja wa chama.

Tusihangaike na mambo mengi hebu tutafute kwanza demokrasia ndani ya vyama vyetu halafu mengine yafuate
 
Aisee.!!

Ukomo wa Mbowe kuongoza ulifika kikomo kwa mtazamo wako kwasababu anawashauri wabaya, hivyo hao washauri ndio walimtuma akanywe pombe alewe?! is this what you mean!

Kwa maoni yako ni kwamba unataka mtu akiwa kiongozi asifanye yale yanayofanywa na wanadamu wa kawaida, unataka ageuke malaika!, usije ukasema namtetea Mbowe kwa ufinyu wako wa kufikiri unaouonesha hapa jukwaani kila kukicha, bali nakuonesha tu udhaifu wa hoja zako.

Hata hivyo ni haki yangu pia kumtetea kwasababu sijui ni kigezo gani umetumia kutuaminisha Mbowe alikuwa amelewa; je, wewe ndie huyo daktari wa Ndugai ulietumwa kumpima mkaanza kuropoka bungeni jana? au ulikuwa nae bar aliyokuwepo mkinywa wote?

Unasema Mbowe ana kikundi cha watu watano kinachomshauri vibaya, unataka kutuambia hao watu watano ndio waliompa Mbowe madaraka? halafu tena; unataka kutuaminisha wewe ndie mwenye ushauri mzuri zaidi ya hao "watano" uliowataja, hasa kwa hoja zako hizi za kitoto unazoandika hapa kila ukijiskia?!

Tambua, hata kama Mbowe alikuwa amelewa; kwani alilewa muda wa kazi akashindwa kutimiza majukumu yake kama kiongozi wa chama chake mpaka umpeleke kwa hiyo kamati yako ya Maadili? ni wapi utamshtaki mtu alieamua kunywa pombe baada ya muda wake wa kazi wakuelewe?!

Funny enough; kwa huu ujinga wako ndio unataka wenye akili timamu waungane na wewe kukusindikiza mahakamani!.
 
Mleta mada weka pia hoja ya ukosefu wake wa maadili wa kusimamia Pesa za chama mashahidi wapo wabunge waliokuwa wakichangia chadema
 
Sasa hapa leo ndio tutaona mapungufu makubwa ya siasa zetu, wanasiasa na vijana wasomi wa kitanzania waliosomeshwa na kodi zetu sisi wakulima.

Hatakuja mtu kuthibitisha kwamba mimi nilikwenda kumuona mbowe hakuwa amelewa wanamsingizia tu, watu watakuja na matusi na vioja vya kila aina.

Nchi hii tumepata uhuru kutoka kwa mkoloni tu, lakini uhuru wa kisiasa bado. Maana watu hawawezi kuhoji, kuuliza wala kudadisi chochote ndani ya chama, ukiuliza unakuwa msaliti, unabezwa na unakuwa adui namba moja wa chama.
Tusihangaike na mambo mengi hebu tutafute kwanza demokrasia ndani ya vyama vyetu halafu mengine yafuate
Umeikubali hoja kwasababu ya uelewa wako mdogo, ukaiona ndio "madini" wala sikulaumu kwa sababu umekiri wewe ni mkulima, kwa upeo wako ukaenda mbali zaidi kurusha mawe upande ambao kwa mtazamo wako na mwenzio mnauona una makosa, kumbe wewe na mwenzako ndio wenye upeo mdogo.

Unazungumzia vijana wanaotetea chama chao kama ndio kosa lao, kwanini hutaki wakitetee? hata kama wana hoja za kufanya hivyo wakae kimya tu ili kukuridhisha wewe, na huyo mjinga mwenzio?

Huyo alieleta huu upuuzi hapa ndio anastahili kutumiwa kama mfano wa kijana mjinga wa hii nchi aliesomeshwa kwa kodi za watz halafu kila kukicha yeye ni Mbowe tu, hajui huyo Mbowe alichaguliwa kwa kura halali zilizopigwa kwenye vikao halali, hana akili ya kuwafundisha waliomchagua Mbowe nini cha kufanya.
 
Tunapaswa kuwapenda Viongozi wetu, lakini isizidi kipimo kiasi cha hata mtu akijiharishia tunasema anakojoa

Huu upumbavu na uwongo unaotengenezwa na viongozi wetu na Sisi tukiendelea kuushabikia
na kuudekeza, unatutengenezeaa ujinga kwenye utawala wa akiri na utashi wetu

Hata kama Tunawapenda ifike mahali tuseme No.
 
Usihamishe mada, tujadili uwezo wa Mbowe kuongoza Chama Kikuu cha upinzani, kuhusu:

√ Tuhuma dhidi yake ya matumizi ya fedha za chama;
√ Tuhuma dhidi yake ya rushwa ya ngono;
√ Tuhuma dhidi yake ya kuhodhi madaraka ya maamuzi;
√Tuhuma dhidi yake ya kuingilia chaguzi za ndani ya chama na kufanya upendeleo katika teuzi; na
√ Sakata la jana kutuhumiwa kulewa kupita kiasi kulikosababisha kuteleza kwenye ngazi nyumbani kwake Dodoma hadi kuteguka mguu (na siyo kuvunjika - ushahidi upo wa kidaktari).

Kuthibitisha tuhuma zilizoorodheshwa hapo juu, kutokana na maelezo ya viongozi wenzake waliokihama chama kwa sababu ya uongozi wake mbovu, TAKUKURU imeanza uchunguzi. Yawezekana uchunguzi huo ndio unamsababishia kuwa katika hali ya msongo wa mawazo kiasi cha kudaiwa kulewa kupita kiasi, kama kuna ni kweli wa madai hayo.View attachment 1474040View attachment 1474041View attachment 1474042
 
Back
Top Bottom