Mbowe ajibu tuhuma dhidi yake juu ya matumizi ya gari la KUB.

Sasa zile kelele za Mbowe hakuna kulala, mpaka kieleweke, Pipozz power, wao wana pesa sie tuna Mungu...

Siasa hizi usanii mtupu...
 
Katuhumiwa nini kwa maana halisi ya neno tuhuma!!

Hapo tuhuma haijajibiwa; badala yake ameibua malalamiko yake ingawa hajaiweka kimalalamiko zaidi; suala la kutofuatilia stahiki yako ya makazi,Samani na Mlinzi hilo laweza kuwa ni tatizo pia kwa namna mbili tofauti.

Moja ana uhakika gani kama stahiki yake aloiacha inaingia kwenye kusaidia uchumi wa Taifa na hauliwi na walafi kwa maana upo ndani ya utaratibu!!

Kwa uelewa wako mwajibikaji ni mtu asitefuatilia haki na wala mdhulumaji wa haki??!!

Pili kwa kutofuatilia haki yake haoni kwamba kuna haja pia ya kuja kututhibitishia kuwa hata House allowance nayo hapokei!!

Kama wafanyakazi wa TANZANIA DAIMA hawalipwi mshahara basi ni ujinga wao hawamfikishi mahakamani mwajiri wao.

Maadam kaamua kujibu. Mbowe pia atueleze kwa nini waandishi wa gazeti lake la Tanzania Daima linalosimamiwa na mkewe hawalipwi mishahara.

Na aseme kwa nini mkewe hivi karibuni aliwajibu wahariri wake kifedhuli kuwa "asiyetaka kazi bila malipo aache! "
 
CCM wanahangaika na Mbowe wakati leo wamejitwisha bomu? Hiyo bajeti italipuka muda si mrefu.
 
Mchagga akatae gari, "pesa"(200K/mo), "numba", mlinzi? ......Labda mbowe siyo mchagga
 
Nilifikiri matatizo ya kuzuwa kwenye tarakimu za mahesabu ni tatizo la waziri wenu kivuli kumbe wote mnatatizo hilo?

Hiyo hesabu yako (niliyokuwekea nyekundu hapo juu) ni uongo na uzushi. Weka hesabu za ukweli.

mkuu nilijua kabisa watu kama wewe hawakosekani ndio maana nikaweka source hapo..kama unalo gazeti soma kwenye habari inayohusu baraza jipya kivuli mwisho wa hiyo habari ndio utakuta matamshi yake haya(hawakuiweka kama habari kamili)..au tembelea website yao
 
Kufuatia tuhuma zilizo elekewa kwake juu ya matumizi shangingi la kambi ya upinzan mbowe alikua na haya yakusema:

"Mimi nilikataa gari kwa kipindi cha miezi sita na nikawa natumia gari langu kwa shughuli zote za vikao vya bunge,lakini nataka umma uelewa kuwa kwa nafasi yangu natakiwa kulipwa posho ya madaraka sh 200000 kila mwezi,kupewa nyumba ya kuishi ikiwa samani zake.

Ila mpaka sasa sina nyumba ya serekali,wala mlinzi,wala kulipwa fedha za mawasiliano,vyote natumia fedha zangu...kama ningetaka ningedai mambo mengi ambayo natakiwa kupata lakini kulingana na hali ya uchumi wa nchi ni lazima nitumie fedha zangu ili kunusuru uchumi" alisema.

Source: Tanzania daima 22 june, 2012

Akizungumzia tuhuma zilizotolewa na wabunge wa CCM, Mwigulu Nchemba (Iramba Magharibi) na Mbunge Livingstone Lusinde (Mtera), kuwa anawahadaa Watanzania kwa kukataa gari kuu kuu la Kiongozi wa Upinzani Bungeni (KUB), lakini akageuka kwa mlango wa nyuma na kuchukua jipya, Mbowe alisema kauli hizo ni za kisiasa.

Mbowe alisema ni kweli kuwa hivi sasa analitumia gari la KUB ambalo alilikataa kwa kipindi cha miezi sita bila kulitumia, lakini Serikali imekataa kubadili sera yake za kuacha kununua magari ya kifahari.

“Mimi nilikataa kwa miezi sita, nilikuwa silipwi gharama zozote za mafuta ikiwamo hata hii ya kila siku ya wabunge na gharama ya mafuta ya kutoka jimboni na kwenda jimboni, na nia yangu ilikuwa ni kuionyesha Serikali kuwa tunaweza kukataa haya matumuzi mabaya lakini, wamegoma,” alisema Mbowe.

Alisema kimsingi, asingeweza kugoma milele kwani lengo lake lilikuwa ni kutoa msukumo ambao ungewezesha magari yote ya kifahari yapigwe mnada.

“Hawa jamaa hawataki kubadilika, nimeona suluhu hapa sio tu kukataa gari lao bali ni kuungana na wadau wengine kuwang’oa madarakani kwa sababu hata katika bunge la mwaka huu, hawajasema kama kuna sera rasmi ya kupunguza matumizi kwa kununua magari ya kifahari,” alisema Mbowe.

Kuhusu kugomea posho ya Sh80,000 ya bunge na kuchukua posho ya Sh 2 milioni kwa mwezi kama KUB, alisema suala hilo anayepaswa kuulizwa ni Katibu wa Bunge, lakini mtu anapokuwa kiongozi wa upinzani bungeni ana stahili zake ambazo zimepangwa.

“Unapokuwa kiongozi wa upinzani kuna stahili nyingi wanapanga sasa zipo kisheria hata kama ukikaa hapa kuna mambo ya kisheria na kiutaratibu, lakini kama nilivyosema awali kikubwa hapa ni kuiondoa Serikali tu, ili kufuta mambo haya,” alisema Mbowe.

Mwenyekiti huyo, pia alikanusha tuhuma zilizotolewa na Nchemba kuwa anasomesha mtoto wake chekechea katika shule ya kimataifa kwa dola 15,000 (karibu Sh20 milioni) kwa maelezo kuwa hana mtoto anayesoma chekechea, watoto wake wote ni wakubwa.

Source; Mwananchi Juni 21, 2012.

 
chadema mnanini jamani kila kukicha kashfa mara heche katukana na kudhulum haki ya makamanda, mara lema na kikapu cha...,.., mara mboye na v8/posho, mara slaa na mshahara wa ubunge, mara shibuda, mara mnyika na mituc, mara nasari na uhuru wa kaskazini, mara komu na ufisadi wa epa, nawapenda sana kama wapinzani wetu hebu tatueni hizi kashfa kwanza then ndo mjikite kisawasawa kupambana na sisi
 
Kama ameamua kulirudia na kulichukua gari baada ya kuona kuwa anaweza kulitumia kueneza elimu ya uraia itakayo wakomboa watanzania walioko gizani na hivyo kuwa mtaji kwa 2015 kwangu sioni kuwa ni kitu kibaya maana ni jambo jema hasa ukizingatia kuwa ni moja ya stahili zake kama kub. Mimi nitafurahi kusikia kuwa hata posho wanachukua ili zisaidie kukijenga chama pamoja na michango inayo changwa kwenye m4c kwa ajil ujenzi wa ofisi za chama na matawi nchi nzima kuliko kuwaachia hawa manyang'au waliouza madini yetu kwa bei poa ya mikataba feki, bila aibu wakatuuza na sisi wenyewe kwa kutuweka rehani kwa mamikopo tutakayo lipa mpaka tufe na sasa wamegeukia kuuza na kutorosha mpaka wanyama nje ya nchi.
Kamanda kanyaga twende usipote muda na watu wanaofikiria kwa jina la mayor wao wa Darisalamu.
Naipenda chadema, naichukia nyinyiemu.
 
Maadam kaamua kujibu. Mbowe pia atueleze kwa nini waandishi wa gazeti lake la Tanzania Daima linalosimamiwa na mkewe hawalipwi mishahara.
Na aseme kwa nini mkewe hivi karibuni aliwajibu wahariri wake kifedhuli kuwa "asiyetaka kazi bila malipo aache! "

si mgeacha kweli au vielimu vya kungaunga..kama hulipwi mshahara unaendeshaje maisha yako au bahasha....
 
Mbowe apunguza Baraza Kivuli la Mawaziri


na Danson Kaijage, Dodoma


amka2.gif
KIONGOZI wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amelipangua Baraza lake Kivuli la Mawaziri kwa kuunda wizara mpya zinazopunguza ukubwa wa lile la awali.
Mabadiliko hayo pia yamewaacha nje mawaziri kadhaa na kujaza nafasi zilizoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, aliyeenguliwa na Mahakama Kuu na marehemu Regia Mtema wa Viti Maalumu.
Hata hivyo, Mbowe hakuwaingiza wabunge wa vyama vingine vinavyounda kambi hiyo vya NCCR-Mageuzi, CUF, TLP na UDP kwa maelezo kuwa bado wanaendelea na mazungumzo yenye kuwafanya waaminiane zaidi.
Wanaounda baraza hilo ni yeye mwenyewe ambaye atakuwa na Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, akisaidiwa na David Silinde, Said Arf anakwenda Miundombinu akisaidiwa na Pauline Gekul, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais atakuwa Profesa Kulikoyela Kahigi, Fedha, Uchumi na Mipango ni Zitto Kabwe akisaidiwa na Christina Mughwai.
Katiba, Sheria na Muungano itaongozwa na Tundu Lissu, Maliasili, Utalii na Mazingira ni Mchungaji Peter Msigwa, Mambo ya ndani ya Nchi, Vincent Nyerere, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ezekiah Wenje atakayesaidiana na Raya Ibrahim Khamisi.
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ni Mchungaji Israel Natse, Maji Mifugo na Uvuvi, Sylvester Kasulumbayi ambaye atasaidiwa na Sabreena Sungura wakati Kazi, Habari, Utamaduni na Michezo ikiongozwa na Joseph Mbilinyi akisaidiwa na Cecilia Pareso.
Nishati na Madini anaendelea kubaki John Mnyika, Viwanda na Biashara, Highness Kiwia na Afya, Jinsia na Jamii ni Dk. Gervas Mbassa, akisaidiana na Conchester Rwamlaza, Elimu, Sayansi na Teknolojia, Suzan Lyimo atasaidiwa na Joshua Nassari.
Wizara ya Kilimo na Ushirika itaongozwa na Rose Kamili wakati Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inabakia kwa Halima Mdee.
Pia, Mbowe alifafanua sababu za kuendelea kutumia gari la serikali ambalo alikuwa amelikataa, akisema kuwa amelazimika kufanya hivyo kutokana na maelekezo ya serikali iliyopo madarakani.
Alisema kuwa alikuwa amelikataa ili kuishinikiza serikali kupunguza matumizi ya magari na kutaka apewe gari dogo lakini kutokana na kutosikilizwa alilazimika kuendelea kulitumia.
"Mimi nilikataa gari kwa kipindi cha miezi sita na nikawa natumia langu kwa shughuli zote za vikao vya Bunge, lakini nataka umma uelewe kuwa kwa nafasi yangu natakiwa kulipwa posho ya madaraka sh 200,000 kila mwezi, kupewa nyumba ya kuishi ikiwa na samani zake.
Ila mpaka sasa sina nyumba ya serikali wala mlinzi, kulipwa fedha za mawasiliano, vyote natumia fedha zangu….kama ningetaka ningedai mambo mengi ambayo natakiwa kupata lakini kulingana na hali ya uchumi wa nchi ni lazima nitumie fedha zangu ili kunusuru uchumi," alisema.


Source: Tanzania Daima Ijumaa, 22 juni 2012
 
Akizungumzia tuhuma zilizotolewa na wabunge wa CCM, Mwigulu Nchemba (Iramba Magharibi) na Mbunge Livingstone Lusinde (Mtera), kuwa anawahadaa Watanzania kwa kukataa gari kuu kuu la Kiongozi wa Upinzani Bungeni (KUB), lakini akageuka kwa mlango wa nyuma na kuchukua jipya, Mbowe alisema kauli hizo ni za kisiasa.

Mbowe alisema ni kweli kuwa hivi sasa analitumia gari la KUB ambalo alilikataa kwa kipindi cha miezi sita bila kulitumia, lakini Serikali imekataa kuba
magamba mna lingine.??
 
hiyo habari iko ukarasa wa ngapi mbona sijaiona kwenye hilo gazeti lililotajwa?

mkuu mimi nimeisomaa kwenye website yao kwahiyo sijui kurasa..ila nenda kwenye habari inayohusu baraza jipya kivuli,mwisho wa hiyo habari ndio utakuta taarifa hii(waandishi hawakuiweka kama habari kamili,ilionganishwa na habari ya baraza jipya)
 
Jibu bado halijaonekana hapo sababu ya kulirudia. Ni kwa sababu hajapewa nyumba na samani zake? Ni kwa sababu hjataka hela ya mawasiliano? Ni kwa sababu anatumia ulinzi binafsi?
Nafikiri hapa mwenyekiti wetu ukiri kuwa ni ajali ya kisiasa. Ulirudisha mbele ya waandishi wa habari, ilibidi ulirudie hivo hivo.

mkuu unaelewa kiswahili kweli au taarifa umeisoma juu juu tu?...mbona kila kitu kimeainishwa
 
Chezea mchaga weye tena akiwa kachanganya uchaga wake katika siasa, watanzania jiandaeni kuumia zaidi endapo huyu mchaga na kampuni lake(Chadema) watapata sehemu ya kula kivulini(serikalini) baada ya kusota juani(upinzani).
The unseen is illustrated by the seen.
 
Back
Top Bottom