Uchaguzi 2020 Mbowe aitahadharisha Tume ya Uchaguzi kuhusu tuhuma za kupanga njama ya kumuengua Lissu kwenye mbio za Urais

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
119,370
222,530
Hili hapa andiko lake

Watanzania wenzangu, tuna masaa 24 kwa NEC kuweka Msingi wa Amani ya Tanzania. Mkakati wowote wa kuengua kwa hila wagombea wetu utapokelewa kwa kishindo kikubwa. #NoLissuNoElection!#SasaBasi! Uzalendo uonyeshwe kwa kusimamia haki na si vinginevyo.


Instagram media - CERjb2yp3fr ( 639 X 640 ).jpg
 
Kuna jambo hapa limepangwa na si bure.

Wapinzani bila shaka wana informers ndani ya hii ya serikali, hivyo habari hii si ya kupuuza na tukumbuke hata Lissu jana aliongelea jambo hili.

Wacha tusubiri,kesho sio mbali ila wajue tu, watatufikisha wanakotaka lakini na wao pia wakiwemo maana wote tuko kwenye jahazi moja.

Ishara za awali(iwapo kweli upo huo mpango), ni kesho kuwa na ulinzi usio wa kawaida katika Mahakama ya Kisutu na maneno ya jirani, na hata Makao Makuu ya CHADEMA nayo yanaweza kuzungukwa na ulinzi wa aina hiyo-mtazamo wangu.

Na kwa tweet hii,sitashangaa kusikia Mbowe kaitwa kwa mahojiano au anashikiliwa.
 
Naishi leo lakini naifikiria kesho, naiomba Tume ya Uchaguzi Tanzania itoe mchango wake katika kulinda amani ya taifa letu, hasa kipindi hiki tukielekea uchaguzi mkuu, pasiwepo na jambo lolote litakalosababisha kuzua taharuki isiyo ya lazima.
 
Haki ni pamoja na Lissu kufuata SHERIA na taratibu tulizoziweka. Tume fanyeni kazi yenu. Kama vipi wazee wa kazi mtakutana nao barabarani. Acheni kujihami kwa kuwatisha Tume na watanzania.

JPM tuko nyuma yako. Kila mtu atahukumiwa sawasawa na matendo yake. Kwanini Lissu asihukumiwe kama atakuwa amekwenda kinyume na utaratibu?
 
Kuna jambo hapa limepangwa na si bure.

Wapinzani bila shaka wana informers ndani ya hii ya serikali, hivyo habari hii si ya kupuuza na tukumbuke hata Lissu jana aliongelea jambo hili.

Wacha tusubiri,kesho sio mbali ila wajue tu, watatufikisha wanakotaka lakini na wao pia wakiwemo maana wote tuko kwenye jahazi moja.

Kiukweli, fitina za kisiasa popote pale haziepukiki....

Lakini CCM na serikali wanayoingoza wameshavuka kwenye viwango vya fitina sasa wanatumia nguvu kulazimisha mambo kwa kuvunja sheria na katiba waziwazi na hivyo kuuvuruga uchaguzi huu na kuvuruga amani kabisa ya nchi yetu nzuri....

Katika hili mtu anaweza kujiuliza; Hivi Tundu Lissu aenguliwe kwa sababu zipi hasa za kisheria....??

Mimi bwana, sijaona vigezo vya kisheria wala kimaadili vitanavyoweza kutumika kumuengua....

Hakuna, hakuna, hakuna...!!!

Mpango ambao ulisukika na kuonekana uta - work out ni huu wa kutumia kesi kwa kushirikiana na NEC...

Bahati njema ni kuwa, umegundulika mapema na unaweza kudhibitiwa kirahisi tu....

Mimi nina hakika, kuwa, Tundu Lissu mpaka sasa ni mgombea halali wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA, na hakuna wa kumzuia....

Mwamuzi atakuwa BALLOT BOX siyo maamuzi ya mezani...
 
Mbowe hamhitaji Lisu maskini Nani asiyejua kuwa alimhitaji Nyalandu mwenye pesa ndio maana kamati kuu ilimkataa Lisu .Baraza kuu likatengua maamuzi ya kamati kuu Mbowe kachanganyikiwa .Tume mwacheni Lisu agombee Mbowe anywe sumu akitaka

Njia ya kuua rushwa chadema Tume mpeni Lisu ugombea Hana hata Mia ya kumpa Mbowe

Mpitisheni Lisu Mbowe anywe sumu akitaka kwa kukosa rushwa
 
Mbowe anatamani Lisu akatwe ili wafaidi mpunga wa Membe kwenye kampeni.

NEC siyo wajinga hakatwi mtu.
John bwana. Kwahiyo unasubiri asikatwe ili uje usema ni kwa sababu hiyo??
Tunajua hakuna sababu wala faida ya kumkata Lissu kwenye uchaguzi huu.
 
Mbowe hamhitaji Lisu maskini Nani asiyejua kuwa alimhitaji Nyalandu mwenye pesa ndio maana kamati kuu ilimkataa Lisu .Baraza kuu likatengua maamuzi ya kamati kuu Mbowe kachanganyikiwa .Tume mwacheni Lisu agombee Mbowe anywe sumu akitaka

Njia ya kuua rushwa chadema Tume mpeni Lisu ugombea Hana hata Mia ya kumpa Mbowe

Mpitisheni Lisu Mbowe anywe sumu akitaka kwa kukosa rushwa
Kumbr ni hayo?
Tunajua hakuna sababu wala faida ya kumkata Lissu.
 
Haki ni pamoja na Lissu kufuata SHERIA na taratibu tulizoziweka. Tume fanyeni kazi yenu. Kama vipi wazee wa kazi mtakutana nao barabarani. Acheni kujihami kwa kuwatisha Tume na watanzania. JPM tuko nyuma yako. Kila mtu atahukumiwa sawasawa na matendo yake. Kwanini Lissu asihukumiwe kama atakuwa amekwenda kinyume na utaratibu?

Kweli kabisaa kila mtu ahukumiwe kwa matendo yake hata wale waliojaribu kunuua lissu hukumu yao itafika,wale waliokataa kutoa fedha za matibabu ikiwa ni haki watahukumiwa ila safari haki ya nani kama mbwai iwe mbwai....
 
Mbowe anatamani Lisu akatwe ili wafaidi mpunga wa Membe kwenye kampeni.

NEC siyo wajinga hakatwi mtu.
Na wasijaribu hao NEC kufanya upumbavu wa kukata majina ya wagombea , kuna mstari mwembamba sana kati ya utulivu na vurugu,NEC wasipelekeshwe na Muoga wa wapinzani JIWE,wamuache akapambane naye kwenye box la kura ,na hizo kura zinahakikiwa mwanzo hadi mwisho...

Na kuna taarifa kwamba NEC wamesajili baadhi ya majina(Sura ni ile ile) kwa ID 2 hadi 3 na ndio wamepata wapiga kura mil 29.
 
Back
Top Bottom