Mbowe ahamasisha maandamano ya kuishinikiza serikali kuchukua hatua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe ahamasisha maandamano ya kuishinikiza serikali kuchukua hatua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MED Org, Apr 19, 2012.

 1. MED Org

  MED Org Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe amewataka wananchi kuishinikiza serikali ya CCM kuchukua hatua za kuwawajibisha viongozi wake wanaoitia hasara nchi. Ameyasema hayo wakati wa kuchangia katika taarifa za Kamati za Bunge huku akishangazwa na uchache wa viongozi wa serikali kutokuwepo Bungeni wakati kikao kikiendelea. Aidha Mbowe amedai kuwa ni dharau kwa wabunge wa CCM kutaka kukutana kwenye vikao vya chama kuijadili serikali na badala yake walipaswa kufanya kazi hiyo katika ukumbi wa Bunge ambako ndiko walikotumwa na wananchi kufanya kazi hiyo ya kuiwajibisha serikali.

  Kwa kauli hii ya Mbowe kuna kila sababu ya kuwa tunakaribia kuingia kwenye maandamano kama hatua za haraka na za kuchukua hatua hazitachukuliwa na serikali. Wimbi la viongozi wa CCM kuendelea kujiunga na CHADEMA na Serikali kuendelea kukaa kimya bila kuwachukulia hatua viongozi wabovu au wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu; kunaweza kuchochea hasira za wananchi na kuyaamini kwa ukaribu maneno yoyote yanayoweza kuenezwa na upinzani hivyo kuisababisha nchi kuingia kwenye machafuko.

  Sisi wananchi wa kawaida tunaishauri serikali kuchukua hatua stahiki kwa kila jambo kwani dhana halisi ya uwajibikaji itajitokeza katika nchi yetu na kuongeza imani ya wananchi kwa serikali.

  Shime viongozi wa serikali na wale wa vyama bila kujali maslahi ya chama ba li ya Taifa; tuchukue hatua sasa.
   
 2. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  JK alijua cag amelipua ndiyo maana akasepea brazir, yaani huyu jamaa ***** ile mbaya!
   
 3. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  sio kila kitu kitaamuliwa na maandamano!!
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Tupe njia mbadala...
   
 5. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Na Maisha bora hayaletwi kwa Ufisadi,Uongo,Unafiki wala ushikaji.
   
 6. Mlingwa

  Mlingwa JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 382
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii serikali inamatatizo sana, ndo mambo ya kishaji na kupeana vyeo kiaina. Shame on you CCM
   
Loading...