Mbowe Afanyiwa Fujo Kubwa Hai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe Afanyiwa Fujo Kubwa Hai

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kamende, Oct 14, 2010.

 1. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2010
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ilikuwa kama sinema za akina Rambo ama matukio ya Rwanda Genocide. Mgombe wa ubunge jimbo la Hai kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe akiwa katika mkutano wa hadhara huko Masama Kati ghafla kijana mmoja wa Green Guard alivamia mkutano kwa lengo la kuanzisha fujo. Kikosi cha ulinzi cha CHADEMA kilimdhibiti kijana huyo na kumhifadhi katika gari moja kwa lengo la kupisha mkutano uendelee.

  Kumbe kijana huyo alikuwa ametangulizwa tu na kwamba pamoja naye walikuwepo vijana wa Green Guards wasiopungua 100. Vijana hawa wakiongozwa na Mgombea udiwani wa CCM katika kata hiyo walikwenda kufunga barabara ili msafara wa Freeman usipite eneo hilo. Kwa kawaida msafara wa Mbowe hutanguliwa na pick-up ambayo hubeba jukwaa na viti. Vijana hawa wa CCM waliliteka gari hilo lililokuwa linaendesha na Ndg. Lootore Lema na kumchukua kumpeleka katika nyumba ya mwanaCCM mmoja katika eneo hilo la Masama Mbweera.

  Mbowe kusikia kuwa kamanda wake ametekwa alivunja mkutano na kuondoka kwenda kumwokoa. Walipofika kama 200m toka eneo la mkutano walikuta jeshi kubwa la vijana wa CCM wakiwa wameshikilia mapanga, mawe, majembe na vyuma. Hapo vita kamili ikaanza.

  Katika vita hiyo magari ya msafara wa Mbowe yapatayo 6 yamevunjwa vunjwa vioo. Wanachama wa CHADEMA wameumizwa. Hata hivyo vijana wa CHADEMA walijitahidi kumlinda mwenyekiti wao wa taifa kwa kuongoza mapigano kama vita vya kawaida kabisa vya msituni. Ilimlazimu Mheshimiwa Mbowe kutoa bastola yake na kufyatua risasi kadhaa hewani ndipo Green Guards waliporudi nyuma na hivyo kuwezesha kupunguza kwa kiasi kikubwa madhara ambayo yangetokea kwa vita hiyo kuendelea uso kwa uso.

  Ilikuwa patashika. Walinzi wa Mbowe walikuwa wakiwafuata Green Guards na kuwanyang'anya silaha zao na kuzitumia kuwapiga nazo. Kwa nasibu vijana kadhaa wa CCM wamekamatwa na kwa sasa wako katika kituo cha polisi cha wilaya ya Hai kwa ajili ya kuandika maelezo.

  Taarifa zilizonifikia punde zinasema kuwa kijana mmoja ambaye amepigwa vizuri na CHADEMA ameomba asidhuriwe zaidi kwani atasema yote; namna walivyotumwa kuvamia na kuharibu mikutano ya Mbowe.

  Waheshimiwa haya ni matunda ya mafunzo ya kijeshi ambayo CCM waliyafanya kwa vijana wao wapatao 5000 huko Iringa mwezi March mwaka huu na baadaye kule Moshi Vijijini ambako walitoa mafunzo ya kijeshi kwa vijana 350.

  Chonde Chonde CCM!!
  Madaraka mnayataka, Sawa; Lakini Damu yetu mnaitakia nini?
  TUACHIENI AMANI YETU!!!!!!!!!
   
 2. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,082
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  hii kali, ndo amani wanayojinadi nayo sio?
   
 3. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Well, tunaelekea pabaya.

  Wananchi wanaumia kwa sababu ya matakwa ya wanasiasa.

  Hawa wanasiasa wao kwa wao ni marafiki saana wanachofanya ni kuchonganisha wananchi.

  Sielewi kwanini Mbowe aliamua kwenda yeye mwenyewe na asiombe msaada wa vyombo vya ulinzi?

  Kuna haja ya wananchi kuwasikiliza vyema hawa wanasiasa.
   
 4. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  ccm wanajua kuwa watashindwa kwenye huu uchaguzi. Wanajipanga kufanya fujo ili watangaze hali ya hatari (soma kipigo kwa wapinzani) nchini.

  Nchi inaogozwa kijeshi na wanajeshi - Kikwete, Makamba na Kinana.
   
 5. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli haya Mambo sio ya kuacha yakae yalivyo. Viongozi wa dini mko wapi?
  Viongozi wastaafu mko wapi?
  CHADEMA TUNAWASIHI MUWE WATULIVU NA ENDELEENI KUHUBIRI AMANI
   
 6. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapa sijakuelewa kabisaaaaa
   
 7. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Inakuwaje JK anatisha wananchi kuwa wapinzani watasababisha damu kumwagika kumbe yeye na chama chake wameandaa vijana wa green guard kuleta fujo??? Sasa kila chama kikiwa na guard wao patakalika kweli?? Chondechonde Kikwete na ccm yako fujo mtufanyie lakini ushindi wetu mtuachie na pia roho zetu mtuachie
   
 8. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Read between lines
   
 9. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Na hii nyingine nimeikuta nipashe inasikitisha sana tunapoelekea huku.

  Vijana wa CCM wawacharanga mapanga wafuasi wa Chadema


  Na Waandishi wetu
  13th October 2010


  [​IMG]
  Rehema Malima (15) ambaye ni mmoja ya watu waliokatwa mapanga wakati wa vurugu lilizotokea kati ya wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nawa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Musoma, akionyesha vidole vilivyokatwa kwa mapanga.

  Watu wanaosadikiwa kuwa wafuasi na viongozi wa CCM jimbo la Musoma mjini, wamewakatakata mapanga na kuwajeruhi vibaya watu wanaodhaniwa ni wafuasi wa Chadema.

  Tukio hilo lilitokea juzi usiku na jana subuhi katika kata ya Kigera mjini hapa.

  Wakizungumza na Nipashe juzi usiku katika Hospitali ya Serikali ya Mkoa wa Mara, mmoja wa majeruhi hao, Seleman Mwita, alidai alishambvuliwa na kundi la vijana wa CCM wakiwa na viongozi wa tawi la Kigera Bondeni.

  Alisema wakati akitokea katika mkutano za Chadema kata ya Buhare alikutana na kundi la vijana hao walikuwa wamevalia sara za CCM walimtaka kueleza sababu za kukishabikia Chadema, lakini wakati akijieleza walianza kumkata na mmoja wapo kuchomoa panga na kumkata kichwani.

  Hata hivyo, alisema wakati akifanyiwa kitendo hicho walikuwepo viongozi wengine wa CCM ambao walionekana kushabikia hivyo wananchi wa eneo hilo walianza kupiga kelele kwa lengo la kumuokoa.

  "Wakati nikiokolewa na wananchi kidogo likatokea gari la mgombea wa Chadema, Vicent Nyerere, ambalo lilinichukua na kunipeleka polisi kupata fomu namba tatu ya polisi kisha kunipeleka hospitalini," aliongeza.

  Alisema wakati madaktari wakijaribu kuokoa maisha yake, ghafla baadhi ya wananchi walimfikisha majeruhi mwingine Mapambano Malima akiwa amekatwa vibaya na panga sehemu ya kichwani na usoni.

  "Nilikuwa natokea gengeni nikiwa na vijana wenzangu sasa wakati nikiondoka kwenda nyumbani nikakutana na kundi hilo ambao wengi nawafahamu wakanihoji ni kwanini navaa beji ya Nyerere (Vicent) kabla ya kujibu walianza kunishambulia," alisema.

  Kadhalika, jana asubuhi, baadhi ya vijana hao walivamia nyumbani kwa mama Tatu William katika eneo la Kigera Bondeni na kumtaka ashushe bendera ya Chadema iliyokuwa juu ya nyumba yake, lakini wakati wakizidi kubishana walichomoa panga na kushambulia mototo wake wa kike, Rahab Malima(15) kwa kumkata vidole vya mkono wa kulia.

  Alisema pamoja na mtoto huyo kushambuliwa, pia walimchoma na chuma chenye ncha kali.

  Kamanda wa polisi mkoani hapa, Robert Boazi, alithibitisha kutokea kwa matukio hayo.

  Boaz alisema matukio hayo yalitokea baada ya ugomvi uliotokea wakati viongozi wa CCM wa kata ya Kigera walipokuwa wakitembea nyumba kwa nyumba wakiomba kura, kitendo ambacho kinadaiwa kuwachukiza wananchi wa eneo hilo na kuzua vurugu hizo.

  Waliojeruhiwa ni Kapuru Charlesi(44), Sele Mwita (27) na Mapambano Malima (30), wote wakazi wa Kigera Migombani.
  Boaz alisema polisi inawashikilia watu watano kwa mahojiano.

  Mgombea ubunge wa Chadema, Vicent Nyerere na Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Musoma mjini, Charles Kayele, walisema kuwa kitendo kilichofanywa na vijana wa CCM kinatokana na vyombo vya dola kufumbia macho malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa dhidi ya CCM kwa kuendesha mafunzo ya kijeshi kwa vijana wake.

  Katibu wa CCM wilaya ya Musoma, Haula Kachwamba, alisema kuwa suala hilo ni la polisi.

  CHANZO: NIPASHE
   
 10. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mamaaaaaaa,tunaenda wapi huku?????
  Kwani hawa walinzi wa kijani wana umuhimu gani?????
  Inamaana polisi wooooote wanao watumia waha toshi hadi watumie green guard????
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Muda mfupi bongo itakuwa kama Cosovo enzi hizo!
   
 12. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  lines zipi hizo?
   
 13. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kazi ipo
   
 15. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,082
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  usijidanganye hata polisi walikuwa wanajua huo mchezo kabla, it made sense for him to intervene mana wangeweza kumdhuru huyo mtu aliyekamatwa
   
 16. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  chadema wanailaumu ccm na ccm nao wanawalaumu chadema kuwa ndio wanaoanzisha fujo na kutumia silaha maana sio ccm wenye walinzi peke yao hata chadema nao wana walinzi wao hivyo hatuwezi kuwa upande mmoja na kulaumu upande mwingine bila uchunguzi wa kina kufanyika na ndipo atajulikana nani anaetaka kumwaga damu za wa tz ili aingie ikulu!!!

  Ama kuhusu member wa jf hatuna budi kuacha uchochezi na kuweka maslahi ya nchi kwanza kinyume chake nchi yetu itaingia ktk machafuko na watakao athirika ni watoto wetu, mama zetu, baba zetu, mabibi na mababu zetu!!!
   
 17. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Swali kubwa sana hili.... la kuhusu polisi.
  Tofauti ya vikosi vya chadema na ccm ni kuwa, wa chadema hawaendi kwenye mikutano ya ccm na kuanzisha fujo.
   
 18. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  kwa nini wana ccm wanakwenda kwenye mikutano ya chadema kuanzisha fujo?
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  vijana wa green guard hawana akili na Fuya ameshashindwa, walicofanya hakina maana... lakini mbowe ameonyesha upuuzi mkubwa kama mwenyekiti wa chama kushindwa kumalizia mkutano na kufuata utaratibu wa sheria (ambao yeye kwa wilaya ya hai ana priviledge hiyo kubwa tu na anaijua) kumtoa kijana wake

  Kama tunalaani violence, basi tuifanye kwa vitendo... kwa kwenda kufanya mambo ya tambaza nimesikitika sana

  siamini mtu mwenye staha anaweza kuvunja mkutano kwenda kuokoa kwa staili ya kibohehe, mringa au tambaza

  angetuma vijana

  Nimesikitishwa na green guards lakini nimesikitishwa zaidi na mbowe

  ukifanya ya kipumbavu na mpumbavu, watu hawatajua tofauti yenu
   
 20. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  There are no lines between.
   
Loading...