Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,571
Ziara ya CHADEMA, mbinyo mkubwa zaidi unakuja dhidi ya mafisadi wa ESCROW.
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe mwanzoni mwa wiki hii alikutana na kufanya mazungumzo na Kansela wa Ujerumani Bibi Angela Markel.
Mbowe alikutana na Kiongozi huyo wa Taifa kubwa duniani pembeni ya Mkutano Mkuu wa chama cha CDU kinachotawala Ujerumani na kinachoongozwa na Bibi Markel.
Ingawa mazungumzo baina ya vigogo hao wawili hayajawekwa wazi lakini inatarajiwa kashfa ya wizi wa fedha wa Tegeta Escrow,Ukandamizaji wa demokrasia nchini na Katiba haramu ya CCM inayoitwa Katiba mpya ni kati ya mambo yaliyojadiliwa.
Katika ziara hiyo nchini Ujerumani mbali na Mbowe pia alifuatana na Makamu Mkiti Professor Abdallah Safari,Naibu Katibu Mkuu Salum Mwalim,Mkiti wa Bavicha Pascal Patrobas,Katibu Mkuu Bawacha Grace Tendega na Mkurugenzi wa Halmashauri wa chama hicho John Mrema.