Mbowe achaguliwa Mwenyekiti Mwenza Democratic Union of Africa - DUA

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,794
71,214
TAARIFA KWA UMMA
Mkutano mkuu wa vyama vya Kidemokrasia Barani Afrika - Democrat Union of Africa (DUA) uliofanyika Jijini Abidjan, Ivory Coast kuanzia Jumapili tarehe 06 Novemba, 2022 na kuhitimishwa leo tarehe 09 Novemba, 2022 umemchagua Mhe Freeman Aikaeli Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa kuwa Mwenyekiti Mwenza wa umoja huo.

Mkutano mkuu wa DUA pia umemchagua Louisa Atta-Agyemang wa chama tawala nchini Ghana, NPP ( New Patriotic Party).

kama Mwenyekiti Mwenza atakayesaidiana na Mh Mbowe kufanya mageuzi ya kimfumo na utendaji ndani ya DUA ili kukidhi mahitaji ya vyama vya mrengo wa kati barani Afrika.

Mkutano mkuu wa DUA umeamua kuwa na wenyeviti wenza wawili ili kurahisisha utendaji na ufuatiliaji wa mkakati wa kueneza itikadi ya mrengo wa kati barani Afrika.

Wenyeviti wenza wataongoza bodi ya watu nane (8) itakayojumuisha makamu wenyeviti kutoka kanda tano za Afrika ambazo ni Kaskani (Morocco), Magharibi (Togo/ Nigeria), Kati (Equatorial Guinea) Mashariki (Kenya) na Kusini (Malawi).

Kikao cha kwanza cha bodi ya DUA kilichoongozwa na Mh Mbowe kimeamua kuhamisha makao makuu ya sekretariati ya DUA kutoka Accra Ghana kwenda Afrika ya Kusini.

Kwa nafasi hii, Mhe Freeman Mbowe atakuwa mmoja wa makamu wenyeviti wa Umoja wa vyama vya Kidemokrasia Duniani- International Democrat Union (IDU) kutokea Afrika.

Imetolewa leo tarehe 09 Novemba, 2022 Jijini Abidjan, Ivory Coast.

My Take;
Uwezo wa Freeman Mbowe na uimara wake unatambulika miongoni mwa wanasiasa ulimwenguni.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Hawa Wahuni hata Ofisi hawana mnawaaminije?
Kuwa na akili ya kutosha kichwani na mipango ni zaidi ya jengo kubwa la ofisi, jiulize kwanini licha ya kutokuwa na ofisi bado wanazuiwa kufanya siasa kinyume cha sheria? hao wanaowazuia wanaogopa kitu gani?

Uongozi wa Mbowe umeisogeza Chadema hatua kubwa zaidi ya wenyeviti wote waliowahi kupita Chadema, chini ya Mbowe imezidi kutambulika kama chama makini cha upinzani Tanzania, huku akiyashinda majaribio ya mapinduzi na usaliti toka kwa kina Kitila, Zitto, Slaa nk.
 
TAARIFA KWA UMMA
Mkutano mkuu wa vyama vya Kidemokrasia Barani Afrika - Democrat Union of Africa (DUA) uliofanyika Jijini Abidjan, Ivory Coast kuanzia Jumapili tarehe 06 Novemba, 2022 na kuhitimishwa leo tarehe 09 Novemba, 2022 umemchagua Mhe Freeman Aikaeli Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa kuwa Mwenyekiti Mwenza wa umoja huo.

Mkutano mkuu wa DUA pia umemchagua Louisa Atta-Agyemang wa chama tawala nchini Ghana, NPP ( New Patriotic Party)
kama Mwenyekiti Mwenza atakayesaidiana na Mh Mbowe kufanya mageuzi ya kimfumo na utendaji ndani ya DUA ili kukidhi mahitaji ya vyama vya mrengo wa kati barani Afrika.

Mkutano mkuu wa DUA umeamua kuwa na wenyeviti wenza wawili ili kurahisisha utendaji na ufuatiliaji wa mkakati wa kueneza itikadi ya mrengo wa kati barani Afrika.

Wenyeviti wenza wataongoza bodi ya watu nane (8) itakayojumuisha makamu wenyeviti kutoka kanda tano za Afrika ambazo ni Kaskani (Morocco), Magharibi (Togo/ Nigeria), Kati (Equatorial Guinea) Mashariki (Kenya) na Kusini (Malawi).

Kikao cha kwanza cha bodi ya DUA kilichoongozwa na Mh Mbowe kimeamua kuhamisha makao makuu ya sekretariati ya DUA kutoka Accra Ghana kwenda Afrika ya Kusini.

Kwa nafasi hii, Mhe Freeman Mbowe atakuwa mmoja wa makamu wenyeviti wa Umoja wa vyama vya Kidemokrasia Duniani- International Democrat Union (IDU) kutokea Afrika.

Imetolewa leo tarehe 09 Novemba, 2022 Jijini Abidjan, Ivory Coast.

My Take;
Uwezo wa Freeman Mbowe na uimara wake unatambulika miongoni mwa wanasiasa ulimwenguni.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Hii inatoa funzo kubwa Sana , ukisimamia kile unakiamini bila kuyumba basi , Mungu naye atakuinua , CCM watakua wanatafutana chini ya meza,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom