Kwenye gazeti la Nipashe Leo Alhamis Novemba 16, 2017 katika ukurasa wa Mbele limeandika nukuu ya maneno ya Mbowe ambapo amesema “Masha hakuwa na msaada wowote ule Chadema”. Lahaula!!
Leo hii Mbowe huyu huyu ndio anaibuka na maneno ya kumtuhumu Masha kuwa hakuwa na msaada wowote ule Chadema? Mbowe anasahau kuwa:-
1. Ni Chadema ndio walimteua Masha kugombea Ubunge Afrika Mashariki (EAC). Utawezaje kumteua mtu asiye na msaada nanyi wowote ule?
2. Ni Chadema hao hao walikuwa wakimpandisha Masha kwenye majukwaa ya kisiasa ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na majukwaa mengineyo ya kisiasa. Huyu ndio ambaye Mbowe anasema hakuwa na msaada wowote ule?
3. Ni Masha huyu huyu alijitoa kwenye uchaguzi wa TLS uliosaidia kuongeza ushindi kwa Tundu Lissu wa Chadema na kunyakua Urais wa TLS. Utasemaje Masha hakuwa na msaada wowote ule? Maneno mengine ni heri Mbowe ngekaa kimya tu kuliko kuamua kuongea pumba tupu.
4. Ni Masha huyu huyu aliingia matatani na vyombo vya kisheria kutokana na uamui wake wa kwenda kituo cha Polisi cha Oysterbay kwenda kutoa dhamana kwa wanafunzi waliokusanyika bila kibali. Nakumbuka Chadema walimsifia sana Masha kutokana na kitendo hiki. Leo hii Mbowe atasemaje Masha hakuwa na msaada wowote ule Chadema?
5. Masha huyu huyu alikuwa anaiwakilisha Chadema kwenye mikutano, midahalo mbalimbali. Mbowe atasemaje Masha hakuwa na msaada wowote ule? Watampaje uwakilishi mtu asiye na msaada kwao?
Anachokifanya Mbowe ni ubabaishaji, ni mwendelezo wa kutokuthamini michango ya Watu ndani ya Chadema. Ni kama ilivyofanyika kwa Zitto Kabwe, Dk. Willbroad Slaa na wengineo. Ipo siku hata wengineo nao pia kuambiwa ni mizigo, ni suala la wakati tu.
Chadema wako hivyo, mtu akitoka Chadema kwao humwita msaliti, hana msaada, amehongwa na CCM, na majina ya ovyo ovyo hupewa. Akienda Chadema huyo hutafasiriwa kuwa shujaa, Mzalendo na kamanda. Huu ni ushahidi tosha kuwa nchini hakuna upinzani bali pamejaa wababaishaji mithili ya Mbowe