Mbosso ndiye mrithi wa Harmonize pale WCB

Nobunaga

JF-Expert Member
Mar 22, 2019
1,169
4,985
Hili liko wazi kabisa, wala halihitaji ubishi. Kijana huyu ana cheche na moto haswaa wa kuweza kukamata siti iliyoachwa wazi na Harmonize.

Najua matarajio ya wengi ni kwamba Rayvany ndio ataziba hilo gap, lakini nionavyo mimi uwezo wake ndipo ulipoishia. Kama ni kumfikia Harmonize basi alipaswa awe ameshamfikia kitambo sana kwani ana muda mrefu sana pale WCB.

Mbosso kwa muda na kazi chache alizofanya akiwa WCB ameonesha kiwango cha hali juu kabisa na kwa sasa ana thamani kubwa kumzidi Rayvany na Lavalava ambao ni wakongwe pale WCB.

Japokuwa WCB walidai wametumia gharama kubwa sana kum-brand Harmonize, lakini faida waliiona kwani mbali na uwekezaji mkubwa, Harmonize personally ana juhudi kubwa na kipaji cha kutosha kwani tangu ajiunge pale WCB thamani yake imezidi kupanda siku hadi siku.

Nadhani katika uwekezaji ambao haujarudisha faida ni huu wa Rayvany na Lavalava. WCB wametumia gharama kubwa kuwa-brand lakini hawa vijana hawana jipya wako level zilezile tuu.

Vivyo hivyo kwa Mbosso, mbali na uwekezaji wanaoufanya WCB kwake pia yeye kama yeye ana kipaji na juhudi kubwa. Nadhani baada ya muda tutamuona kijana akiwa level zingine kabisa tena huenda akafikia level za kushindanishwa na boss wake Diamond kama ilivokuwa kwa Harmonize.

Ukweli ndio huo, povu ruksa.

 
Back
Top Bottom