Daimler
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 556
- 973
Kwa sasa tunaishi maisha ya kizungu, ya kuwa na vyakula na vinywaji kwenye majokofu. Huu ni ustaarabu ulioletwa na wazungu na umeenea maeneo yote duniani. Kwa Nchi masikini kama Tanzania, majokofu yanatumika sana mijini kutokana na kipato mikubwa cha wakazi wa mijini.
Imeshafikia kama ni kitu cha aibu kwa mkazi wa Dar kukosa jokofu nyumbani. Watu wenye uwezo hununua kreti ya soda ha kuiweka nyumbani lakini wasio na uwezo hununua kuanzia moja na kuendelea.
Je, ulishawahi kujiuliza kuwa, majokofu ya familia nyingi za Bongo, ukitoa wale wa nafasi ya juu huwa hayana vinywaji muda mwingi?
Kwa kawaida, mara moja moja utaona familia inanunua soda labda mbili, tatu ama tano lakini changamoto inayowapata kama hawajazinywa soda hizo, watasumbuka sana siku nzima watazifikiria tu hizo soda. Yaani wasipozinywa wataendelea kuteseka kuwa wanakumbuka tu kuwa, kuna soda kwenye jokofu. Utashangaa kwa siku hiyo hiyo moja watajikuta wamezinywa soda zote.
Yaani wasipozinywa basi watapata tabu sana.
Wadau naomba kupata mwazo yenu, hili suala likoje kwako ama nyumbani kwenu: je, huwa na nyie kuna ka kitu kanakuwa kanawakereketa kuwa kuna soda kwenye jokofu?
Najua wazee wa gambe hawasumbukiagi visoda so siyo issue kwao.