Mbona wazungu kwenye muvi zao wanatumia lugha ya Kiswahili kama lugha inayotumika na magaidi?

Kesiman9

Senior Member
Jun 23, 2016
117
160
Hivi karibuni nimekuwa nikiangalia baadhi ya season za kizungu Na miongoni mwa filamu hizo nimeona waigizaji wakitumia lugha ya kiswahili hasa Kwenye upande wa Ugaidi
Miongoni Mwa filamu hizo ni Quantico Na The Widow
Kwa walioziangalia watajua nini nazungumzia
 
Kiswahili haijaanza kutumika leo. George ze jangle, king lion ( hakuna matata) na nyingne nying za zamani ziltumia kiswahili kama kuonesha uhusiano na africa.

Jibu ni kuwa, kiswahili ndyo kama lugha ya Africa. Nchi nyingi zinazungumza kiswahili ukilinganisha na kifaransa. Sema kifaranca sio origin ya africa.
 
hivi karibuni nimekuwa nikiangalia baadhi ya season Za kizungu Na miongoni Mwa filamu hizo nimeona waigizaji wakitumia lugha ya kiswahili hasa Kwenye upande wa Ugaidi
Miongoni Mwa filamu hizo ni Quantico Na The Widow
Kwa walioziangalia watajua nini nazungumzia
QUANTICO SEASON YA NGAPI?
 
Wa TZ bongo lala,Jisifuniii lakini ujue hicho kiswahili kinachotumika hao wanao kitumia wenyewe wanajua ni kiswahili ya Kenya
Kweli, nadhani wakenya hukisambaza Kiswahili kimataifa kupitia wasanii wakubwa kimataifa, sie bongo tunajifanya wa zungu @wemasepetu, na wenzake, R. I. P Kanumba
 
Kiswahili cha kenya cha kipuuzi sikipendi hata kukisikia binafsi nahisi kichefuchefu
 
Labda Wasanii Wa Kitanzania Nao Watakapopenya Huko Holywood, Bolywood Na Nolywood Huenda Watakipaisha Kiswahili Zaidi Kwenye Anga Za Kimataifa. Wakenya Wameweza Kukiingiza Kiswahili Cha Lafudhi Yao Kwenye Season Za Kihindi. Watanzania Nao Waingie Huko.
 
Kiswahili haijaanza kutumika leo. George ze jangle, king lion ( hakuna matata) na nyingne nying za zamani ziltumia kiswahili kama kuonesha uhusiano na africa.

Jibu ni kuwa, kiswahili ndyo kama lugha ya Africa. Nchi nyingi zinazungumza kiswahili ukilinganisha na kifaransa. Sema kifaranca sio origin ya africa.
Mkuu umenikumbusha George the jungle ilikua na cartoon yake nzuri sana
 
Kiswahili haijaanza kutumika leo. George ze jangle, king lion ( hakuna matata) na nyingne nying za zamani ziltumia kiswahili kama kuonesha uhusiano na africa.

Jibu ni kuwa, kiswahili ndyo kama lugha ya Africa. Nchi nyingi zinazungumza kiswahili ukilinganisha na kifaransa. Sema kifaranca sio origin ya africa.
Tuanzie na wimbo wa Micheal Jackson girl wa Liberian Wako alichomekea kiswahili nakupenda pia nakutaka pia mpenzi we.
 
Back
Top Bottom