Mbona wasifu wa Lowassa una mushkeli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbona wasifu wa Lowassa una mushkeli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jul 13, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Edward Lowassa halali bila ya kuutafakari Uraisi wa 2015...........bila ya kujua historia inapingana na azma yake hiyo....................Ni Nyerere tu aliyewahi kuwa Waziri Mkuu alienda kuwa Raisi katika nchi hii lakini wengineo wote waliojaribu kupanda cheo hiki wakiwa wamepitia U-PM waliambulia pua kugonga mwamba..................waulize Warioba, msuya, Malecela, kawawa, Sumaye, Saim Ahmed Salim na wengineo........hata Nyerere ilibidi ajivue Uwaziri Mkuu na kumwachia Kawawa baada ya kugundua hiyo haikuwa njia ya kuukwaa Uraisi......................

  sababu za hilo zilijengwa vyema na Sumaye alipokuwa anawashukuru wabunge mwaka 2010 wakati Bunge la awamu ya Mkapa linavunjwa.......................aliposema huu uwaziri mkuu umemletea uadui na wabunge na watendaji wengi serikalini waliodhani bughudha walizokuwa wakizipata ni yeye ndiye amewasukia.....................................lakini kwa maono yangu ni kuwa utendaji wake ulikuwa umegundulika na hivyo kuonekana hafai.....

  Lowassa anataka kuwa Raisi wetu na kuuvunja mwiko huu uliowashinda wenzie lakini njia anayoitumia.......................ni hadaa ambazo ni vyema tukazitafakari kwa undani wake.....................................kwanza amekuwa akicheza mchezo wa kuonekana onekana kwenye matamasha........ wazungu huita "visibility"...................lengo asisahaulike machoni pa jamii.................kwa kujionyeshaonyesha kwenye sherehe kama za michango ya kanisa na nyinginezo za kuchangia shughuli za maendeleo..........................................lakini ni kauli yake ya kuikandia utawala uliopo kuwa unapwaya kwa kushindwa kufanya maamuzi magumu ndiyo imemleta kwenye "focus"...............................bila ya kufafanua ni maamuzi gani hayo.................hasa ukizingatia ya kuwa ufisadi ndiyo unatishia mwelekeo na umoja wa taifa hili............................

  sasa hebu tupenyeze jicho kwenye wasifu wa Lowassa wa karibu miaka 30 hivi tuone yeye na ufisadi wakoje?

  a) Utawala wa kiimla wa Mwinyi......................


  i) Lowassa alipokuwa waziri wa ardhi alimmegea Mwinyi na mkewe Mama Siti viwanja viwili vya maeneo ya wazi...isivyo halali na kinyume cha sheria....................yote haya aliyafayna ili kulinda ugali wake kutoka kwa Raisi Mwinyi...........................je haya ndiyo maamuzi magumu ya kukwapua mali za ummma...................????????????????????????????

  ii) akiwa bado katika ofisi ya waziri mkuu na ni waziri anayeshughulikia maafa..........................waathirika wa mafuriko wa Lindi na nachingwea walionja cheche zake pale ambapo alihamishia michango ya wahisani kwa walanguzi na ikazagaa barabarani ikiuzwa huku waathirika hao wakiachwa solemba....................................je haya ndiyo maamuzi magumu ambayo Lowassa amekuwa akiyapigia baragumu?

  b) utawala wa mjasiria mali Mkapa..............................


  i) Lowassa aliwekwa benchi kutokana na Nyerere kuchukizwa na kijana Lowassa kujihusisha katika vitendo vya ufisadi.......................hivyo jina lake halikuwepo kwenye baraza la mawaziri........la kwanza la mjasria mali Mkapa..........ambaye ujasiria mali wake ni kutupora maliasili yetu kama vile Kiwira mines.....n.k....................

  ii) akiwa waziri wa maji alishinikiza mradi wa maji ya Ziwa Victoria ambao gharama zake za awali zilikuwa ni Tshs 50 billions.......lakini hadi hivi sasa umevuka billions 350...............na ni wanavijiji chini ya 10, 000 ambao wameunganishwa na wengi wao wameshindwa kumudu gharama zake na kuufanya mradi huo kuishi kwa kupumulia fadhila za hazina.....................lakini Lowassa na wenzie walizitafuna fedha za mradi huo.............bila ya zengwe....sasa sijui haya ndiyo maamuzi magumu ambao wapo madarakani wapaswa kumuiga????????.....

  iii) akiwa bado maji alishinikiza mradi wa kuwang'oa wazawa DAWASA........................na baadaye kuwarudisha baada ya kung'amua ya kuwa ni wazawa tu ambao wataitoa nchi hii kwenye lindi la umasikini................................................lakini hatua hizi zote yalikuwa maamuzi magumu ambayo hayakuwa na tija ila hasara tupu...................kwetu..............

  c) Utawala wa mlaji JK

  i) lowassa aliukwaa U-Pm kwa sababu JK alihitaji Lowassa ajitoe kwenye kinyang'anyiro cha Uraisi na hivyo kutogawa kura ambazo Sumaye angelikuwa mnufaikaji mkuu............................................Lowassa hakuwa na sifa nyingine zaidi ya hiyo ya kuwa powerbroker..............................

  ii) Katika U-PM wake hakuna hata kesi moja ya ufisadi iliyofikishwa mahakamani...........kwa sababu yeye binafsi hauchukii ufisadi uliomwezesha kuwa mtu mashuhuri katika taifa hili la masikini..................Hapo uamuzi mgumu ulikuwa ni kufunika ufisadi tu............

  iii)alipoondolewa U-PM tuhuma yake ilikuwa kufanya maamuzi magumu ya kulipora taifa hili changa kupitia kampuni hewa ya RICHMOND/ DOWANS kwa kile yeye mwenyewe Lowassa alijitia kitanzini Bungeni alipokiri kuwa aliunda tume aliyoiita ni ya wataalamu ili kubariki ujambazi huu dhidi yetu bila ya kufuata kanuni na sheria za manunuzi......................................................

  Lowassa ni vyema akahojiwa zaidi hivi maamuzi magumu anayoyaongelea ni sawasawa na yale ya nyakati za utawala wake..............au sasa amebadilika siyo yule yule lowassa we know........................................power hungry..............and megalomaniac...............
   
 2. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu mchango mzuri sana ila hizo desh ulizoweka unamaanisha kuna kitu unataka watu wajaze au ndio style ya Uandishi wako???
   
 3. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  a) Utawala wa kiimla wa Mwinyi...

  Alipokuwa Waziri wa Ardhi alimgawia mzee Manji viwanja kifisadi kitendo
  kilichomchukiza Mwl. Nyerere na kusababisha mzee Manji akimbie nchi
  na kwenda kuishi uhamishoni Marekani hadi alipofariki huku akimwachia
  mwanaye Yusuf Manji...

  b) Utawala wa mjasiriamali Mkapa...

  Aliwalazimisha City Water kuichangia CCM mamilioni ya fedha wakati ule
  wa mkutano wao mkuu katika mchakato wao wa kumtafuta mgombea
  urais kupitia CCM... walipokataa aliwaundia zengwe kuwa hawafai wakafukuzwa.

  c) Utawala wa mlaji JK...

  Alikuwa akitumia ubabe kuwalazimisha wafanyabiashara kuichangia CCM
  mamilioni ambayo hata hivyo yaliishia mikononi mwa wajanja wachache,
  pia alilazimisha mikataba minono wapewe marafiki zake...
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  sina la kuongeza hapo...............umejaliza vizuri madudu ya huyu mheshimiwa...............
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  [h=2][/h]
  yote mawili......ninakwepa kukutafunia kila kila kitu na kukumalizia uhondo lakini vile vile ningependa kuona na wewe unalionaje suala hili...............
   
 6. N

  Nakwetu Member

  #6
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata wewe uandishi wako una MUSHKELI kubwa sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, doti doti za nini? Jirekebishe.
   
 7. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #7
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  hivi nyie mkoje? mmeshindwa kuchangia hoja ya mtoa mada, mmeona dots tu? aisee.........na mm nawaongezea dots nyie mnaohoji dots...................................................akili zenu....................................................
   
 8. F

  FUSO JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,867
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 9. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Heri ya Lowasa alikuwa anazalisha cha kuiba kuliko hii misukule iliyobaki inaiba cha kuzalisha!
   
 10. M'bongo

  M'bongo Senior Member

  #10
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mh, hii kali babake'
   
 11. M

  Msharika JF-Expert Member

  #11
  Jul 13, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo unataka sema Lowassa ni mwizi bora kuliko hawa wengine? Kushneiiiiiiiiiiiiii
   
 12. Mkenazi

  Mkenazi Senior Member

  #12
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Lakini Lowasa ni tunda la mti gani? maana mti utambulika kwa matunda yake; hivyo ikiwa yote yaliyoorodheshwa yamefanyika chini ya utawala wa CCM na anendelea kudunda tunapata picha kuwa mti uliomzaa (CCM) ndio mbovu hivyo haitakiwi kupewa ridhaa ya kuongoza nchi hii. Thread hii ilitakiwa iwe na heading hii " Mbona wasifu wa CCM una mushikeli?"
   
 13. Mkenazi

  Mkenazi Senior Member

  #13
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Lakini Lowasa ni tunda la mti gani? maana mti utambulika kwa matunda yake; hivyo ikiwa yote yaliyoorodheshwa yamefanyika chini ya utawala wa CCM na anendelea kudunda tunapata picha kuwa mti uliomzaa (CCM) ndio mbovu hivyo haitakiwi kupewa ridhaa ya kuongoza nchi hii. Thread hii ilitakiwa iwe na heading hii " Mbona wasifu wa CCM una mushikeli?"
   
 14. M'bongo

  M'bongo Senior Member

  #14
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Heri kiongozi fisadi ambaye anazalisha na kuiba kidogo huku akiwaachia kingine
  kuliko kiongozi legelege ambaye hazalishi ila anaachia watu wanaiba tu bila kuwakemea...
   
 15. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2017
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,463
  Likes Received: 10,673
  Trophy Points: 280
  Ni vizuri kuendelea kuhoji
   
Loading...