Mbona wanawake mna wivu wa kijinga hivi

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,516
47,752
Tumesafiri kikazi na jamaa yangu fulani Mtanzania. Sasa yeye muda mwingi baada ya shughuli za kazi huwa anaingia chumbani hotelini na kubaki humo ndani muda wote, ilhali mimi na wenzangu tunatoka na kuserebuka mjini, tunamuacha na tukirudi tunamkuta ametulia anasoma soma wala hataki kabisa kutoka.

Tatizo ambalo sielewi ni pale mkewe amekua mgomvi, anampigia simu na kufuata fuata akimtuhumu mambo ya ovyo. Kuna siku jamaa alikua amelala na aliweka simu kwenye silent mode, alipoamka akakuta miscalls nyingi sana za mkewe, na meseji kibao za ugomvi.....yaani kichizi.

Sasa swali langu kwa wanawake, hususan mlioolewa, mbona mnakua na wivu wa kijinga hivi? Mnafahamu kwamba nyie ndio chanzo cha waume zenu kuchepuka maana kama ukimzingua sana hivi inabidi awe na mchepuko basi ili ndio tuhuma zako ziwe na mantiki. Na kingine, nani aliwadanganya kwamba kupiga piga simu ovyo na meseji ndio zitazuia mwanaume kuchepuka. Mtie akili jamani.
 
Mke kabila gani?mkikuyu?

Hehehe!! Kabila tena?? Ni Mtanzania, siunajua tena kwenu hamuulizani makabila, hivyo wewe generalize tu kwa wanawake wote bila kuangalia kabila gani.
 
Hehehe!! Kabila tena?? Ni Mtanzania, siunajua tena kwenu hamuulizani makabila, hivyo wewe generalize tu kwa wanawake wote bila kuangalia kabila gani.

Wewe ni Mkenya
so huwajui vizui wanawake wa TZ
nakuuliza kabila sababu najua tabia zao kutokana na kabila tofauti
 
MK254 unapozaa mtoto, unamlea, unacheza nae, umeshamzoesha kuchezea gololi zako, sasa siku akichezea gololi zako mbiele ya wageni utasema huyu mtoto ana tabia mbaya? Huyo rafiki yenu amezoesha mkewe hivyo au inaelekea ndani ya nyumba mama ndiye mvaa suruali.
 
Sasa hapo ni wanawake au ni huyo mwanamke?
Kama nyie mna wake na hawawafanyii hivyo ndio maana mnazurura, kwa nini u generalise kwa wote?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
MK254 unapozaa mtoto, unamlea, unacheza nae, umeshamzoesha kuchezea gololi zako, sasa siku akichezea gololi zako mbiele ya wageni utasema huyu mtoto ana tabia mbaya? Huyo rafiki yenu amezoesha mkewe hivyo au inaelekea ndani ya nyumba mama ndiye mvaa suruali.

Hehehe aisei dah!! Nilijua ukiibuka huku utakua na jibu lililojitosheleza, nimecheka balaa. Haya bana ugomvi sina, yangu macho.
 
Wewe ni Mkenya
so huwajui vizui wanawake wa TZ
nakuuliza kabila sababu najua tabia zao kutokana na kabila tofauti

Nimeuliza na kuambiwa mkewe jamaa ni Mchagga, ila mwanaume ni kabila la kule kanda ya ziwa.
 
Kuchunga usalama wa mali zako ni muhimu.

Btw, ilikuwaje akakuhadithia hayo yote? au na ww unaona wivu?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom