Mbona wanaume huwa na kigugumizi kutamka 'mke wangu'

Polisi

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,082
639
Wakuu bila shaka mtakubaliana nami kuwa wanawake hutambulisha waume zao bila kuuma maneno yaani 'huyu ndiye mume wangu'. Kwa upande wa wanaume hali naona huwa tofauti kwani utawasikia 'huyu ndo shemeji yako' huyu ndo mama watoto' huyu ndo mamsap' huyu ndo mama polisi' n.k. Akijitahidi sana utasikia 'huyu ndo my wife'. Hivi tatizo ni nini wanandoa wenzangu?
 
huyo wa kwako ndio ana matatizo ya hicho kigugumizi, wanaume wengine wako proud na wake zao wanawaentitle 'mke wangu' anywhere everywhere anytime everytime.
 
Sijaona tatizo kwa Mwanaume kumtambulisha huyu ni mama watoto wangu kwanza inampa Heshima kuwa amemzalia hata watoto.
Hivyo kuitwa kwa mtu mke au mume inatakiwa itoke moyoni mwake sioni kama kunatatizo kwa hilo
 
ok.mimi nilidhani pengine kutamka mke wangu ina heshima zaidi
 
huyo wa kwako ndio ana matatizo ya hicho kigugumizi, wanaume wengine wako proud na wake zao wanawaentitle 'mke wangu' anywhere everywhere anytime everytime.

mh, labda tofauti ya sampuli tulizotumia. Maana hata walokole wanatumia 'baba'
 
Kutamka mke wangu inaheshima zaidi , japo hata ya kumuita mama Polisi nayo ni heshima pia ....Ila heshima katika ndoa ndio jambo la msingi na si kingine.
ok.mimi nilidhani pengine kutamka mke wangu ina heshima zaidi
 
kwani ni lazima muitane mama/baba fulani,mbona haijakaa kimahaba,hata hiyo mke wangu pia kama ya kijima fulani,itaneni majina matamu bwana yanayowafanya mshinde kutwa nzima mnayevukwa ndio maana mki.... inakuwa kila siku 1-0.
 
Ila mke wangu/mume wangu inanoga zaidi.

Kuna wageni hapo wamekaa afu unasikia. Karibu chakula mume wangu! Asante Mke wangu. Karibuni chakula wageni asante mama polisi.
 
Naunga mkono hoja, na mimi nina tatizo hili yaani namwita mke wangu jina lake kabisa na wala simwiti mke wangu au mama fulani/watoto. Ila yeye hupenda kuniita baba fulani(mtoto wetu) au nae huniita kwa jina langu na mambo yanakwenda vizuri, yaani raha tu.

Nyie wenzetu wa honey, sijui sweet heart or baby endeleeni tu wengine uzungu/kutumia kiingereza eti ndio kunogesha penzi hatutaki/hutuamini hivyo.
 
Nimeipenda hiyo, hayo majina si ndio mlianza kuitana bwana.ld mi nakupenda na mi nakupenda chapa nalo.
 
Naunga mkono hoja, na mimi nina tatizo hili yaani namwita mke wangu jina lake kabisa na wala simwiti mke wangu au mama fulani/watoto. Ila yeye hupenda kuniita baba fulani(mtoto wetu) au nae huniita kwa jina langu na mambo yanakwenda vizuri, yaani raha tu.

Nyie wenzetu wa honey, sijui sweet heart or baby endeleeni tu wengine uzungu/kutumia kiingereza eti ndio kunogesha penzi hatutaki/hutuamini hivyo.

hii ya kuitana majina halisi, sina comment ila mimi siwezi. Kuna majina ya kuitana mbele za watu na yale mkiwa peke yenu. Sweet, honey kwa maongezi ya cm au mkiwa room. Huwezi kumwita honey njoo akiwa ktk kundi la watu
 
Hahahaha...I think I will call her by her name (napendelea jina lake la kilugha kama analo). Kama tuna mtoto then I can say mama fulani. Ila nadhani mke wangu mpendwa ni jina maridhawa kabisa. Hiyo ya honey, dear na sweetheart mi naona ni artifical mno. Mimi aniite jina langu langu la utotoni au baba fulani.
 
Huyu ndio 'nyonga mkalia ini' wangu.
Nafikiri hilo linapendeza zaidi.
 
Mimi mume wangu amekuwa akiniita "baby" siku zote. Maokeo yake mwanagu (three years) anajua nina majina mawili including baby. Basi ananiia baby nisipoitika ananiita mama. Watu wakimuuliza mama yako anaitwa nani anataja majina mawili xx na baby. However it feels so sweet to hear my sons (na mtoto mkubwa) calling me baby, and the way they call it.
 
Jamani tatizo mbona si lioni hapo au lugha anayotumia ndio shida? wewe ukiambiwa huyu ndio mamsapu huwa huelewi kwamba anamaanisha mke wake.. mbona hivyo polisi
 
Wakuu bila shaka mtakubaliana nami kuwa wanawake hutambulisha waume zao bila kuuma maneno yaani 'huyu ndiye mume wangu'. Kwa upande wa wanaume hali naona huwa tofauti kwani utawasikia 'huyu ndo shemeji yako' huyu ndo mama watoto' huyu ndo mamsap' huyu ndo mama polisi' n.k. Akijitahidi sana utasikia 'huyu ndo my wife'. Hivi tatizo ni nini wanandoa wenzangu?

sidhani coz sina kigugumizi kabisaaa
 
Naunga mkono hoja, na mimi nina tatizo hili yaani namwita mke wangu jina lake kabisa na wala simwiti mke wangu au mama fulani/watoto. Ila yeye hupenda kuniita baba fulani(mtoto wetu) au nae huniita kwa jina langu na mambo yanakwenda vizuri, yaani raha tu.

Nyie wenzetu wa honey, sijui sweet heart or baby endeleeni tu wengine uzungu/kutumia kiingereza eti ndio kunogesha penzi hatutaki/hutuamini hivyo.

Bandiko lako zuri kwa maana limehitimisha mengi:
1. Kuitana majina inategemea mmezoea vipi . Wengine huanzia na mpenzi/darling kisha baba/mama fulani.Wengine huzoea kuitana majina yao halisi na siyo baba/mama fulani ( mimi mmoja wao).Wengine wakiitana majina yao watu huwashangaa, na wapo wanawake wasipenda kuitwa majina yao hasa kama wana watoto.Ni uchaguzi tu.

2. Mke /mume wangu ni "cheo" katika mahusiano. Mara nyingi hii hutumika kutambulisha rasmi kwa marafiki n.k. ili kutofautisha na watu wengine kama dada, shemeji wa kike, hawara etc.Mwanaume usipomtambulisha mkeo kwa cheo hiki kwa wenzio unajiweka kwenye hatari hivyo chunga.Siku nyingine hao hao wakikutongozea huyo mkeo utasema nini?
 
Back
Top Bottom