Mbona wanafunzi wa vyuo hawapewi mikopo inayotosheleza?

field marshall1

JF-Expert Member
Sep 17, 2017
1,171
2,730
Serikali imesema wanafunzi wanalipwa mikopo lakini mbona hiyo mikopo inalipwa robo tu hadi nusu?

Kama unamlipa mwanafunzi mkopo ambao ataurejesha, kwanini umpe mkopo ambao haumtoshelezi?

Mbona tunajisifia kuwa tunakusanya kodi kubwa kila mwezi lakini wakati wa kulipa ni matanga?

Hata wanafunzi wa elimu ya juu siyo wengi kulinganisha na majirani lakini tunashindwa kuwapa mikopo ambayo watailipa baadaye?

Kama ni kumlipia ada ya elimu ya juu kwanini serikali yetu ishindwe kulipia wanafunzi? Ina maana pesa hizo tunazokusanya hazitoshi?

Mheshimiwa Rais, hilo suala la Mikopo ya wanafunzi ni vyema lifanyike vizuri.
 
Na nyie mnatakiwa utoto uwatoke, kwani mnajidhania bado kuna mzazi wenu wa kuwadekeza? Sio huyo wa kambo,
Nyie hamuoni yanayotokea na watu wanalalamika humu, chagueni kitimiza wajibu wenu katika mapambano haya, sio muda wa kudeka huu, mdai haki zenu sawa, ila biashara ya, " mama, mama, mama" muache ,, its time to hate the regime and wait for the right timing, be rrady for anything, ,
 
Back
Top Bottom