Mbona wakati wa sasa watu wa PCM, PCB, CBG wanafaulu sana kidato cha sita kuliko enzi zetu au kizazi hiki ubongo wao mzuri zaidi?

Internet pia inachangia sana, mtoto akitaka info za kitu flani ana google chap.... Smartphone zimesambaa sana ukilinganisha na enz hzo.
 
Kama we in mdau wa elimu jibu utakuwa nalo, ukweli ni kwamba vijana wa siku hizi ni hovyo sana(siyo wote), sijajua vizuri lengo LA serikali ni nini haswa, mbali ya kwamba uwezo wao ni mdogo sana kuliko kawaida lakini wanazidi kufanya vizuri kuliko miaka yote. Mfano matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa juzi ndo yametia simanzi, watoto wetu wamefanya vizuri kuliko uwezo wao, hatukatai yote mema, lakini inatisha kuona kijana tayari amefanya vizuri kidato cha 6 lakini bado hana uwezo wa kuchanganua mambo madogo hata ya kawaida, mfn hai kuna mzazi ananiambia binti yake amepata 2 ya point 10, lakini anajua fika Huyo binti yake hakuwa na uwezo wa kupata alama hiyo...huu ni mfano halisi. Ila yote tunashukuru acha maisha yaendelee.
Hili ndio jibu sahihi
 
Mleta mada hivi unafikiri kwa nini kizazi hichi kuna teknolojia ya hali ya juu ukilinganisha na miaka yenu ya 60,ina maana wazee wa siku hizi(vijana wa enzi zenu) hawakuwa na akili na uwezo mkubwa wa kufikiria na kufanya gunduzi mbalimbali ambazo zingeleta mapinduzi ya teknolojia tangiapo?
 
Acheni izo nyie watu wazamani, wapeni sifa zao madogo wanafaulu kwasababu upatikanaji wa material saiv ni rahisi kuliko zamani, tuition nk msijifanye mko vzur kuliko sisi malecture wangapi wazamani nawaona uwezo wao wakawaida tu
 
Mkuu ulichoongea hakina uhalisia you tube hizi hizi zilizojaza Amber ruty na ushilawadu mwingi, yani sisi tu watu wazima kutumia mitandao kwa faida bado kuna tatizo sembuse vijana, clip kibao mitandaoni watoto wanakata viuno, tatizo kubwa sana sasa hivi ni maadili ya wazazi kushuka, zamani mtoto kujua baba amegombana na mama ni ishi, ila sasa hivi mtoto anajua hadi michepuko ya mzazi, sasa tunafundishana nini kimaadili
Umeona logic zenu watu wazamani zilivyo zakishamba
 
Siku hizi siasa za ccm zimeathili sana Elimu

Quantitatively wanalazimisha ufaulu wa idadi kubwa.

Quantitatively wanalazimisha numbers na grades ziwe za juu

Ukweli mitihani ni hafifu sana na haina qualities kama siku za huko nyuma.

Kifupi siasa za ccm zinaathili taasisi nyingi.
Umefanya uchunguzi au yanakutoka tu, umetoa wapi data, wasomi na watu wa vijiweni hakuna tofauti
 
Kama za kishamba zimekuuma nini, sisi tumeona zamani na sasa tunaona, usinitibue dada yangu
Relax hakuna inaemuuma its just a comment usije pata ugonjwa wa moyo kwa comment ya jammiiforumn, ila sitengui kaul umeongea pumba
 
Kwasisi tuliofanya paper kama 'PC' mambo yamekuwa magumu kidogo sijui tatizo lipo wapi maana lile Paper tulitusua sana.

Anyway!! Ngoj mwakani tutupe tena karata huenda malengo yetu ya kupiga one ya 8 yakatimia.
Ni malengo tu mkuu inawezekana
 
Inawezekana mfano wangu huu hauna uhusiano wa karibu sana na mada hii, ila zamani kidogo niliwahi kuwa mwalimu wa UDSM. Akaja kijana mmoja kutokea Kibaha akiwa amepasua PCM AAB. Alipokelewa kwenye idara kama shujaa na alitegemewa kuwa atapasua tena na kubakishwa kama TA, hivyo alikuwa treated cautiously sana. Unfortunately mwaka wa kwanza tu akakamatwa na sup mbili, mwaka wa pili akaurudia, na mwisho akagradauate na makarai mengi sana. Wakati mwingine performance ya mitihani form six siyo representation ya academic agility ya mtu.
 
Sababu NANE (8) za wazi za wanafunzi kufaulu PCM, PCB na CBG:
  • Wanafunzi wengi kujitambua. (Kwenda tu A-Level si pekee jambo la kujivunia kama wakati ule, ni lazima upige huko hivyo juhudi ya wanafunzi kujisomea ni kubwa)
  • Vitendea kazi kupatikana kwa urahisi. Vitabu, majarida, mitihani iliyopita n.k. Vitu hivi zamani ulikuwa unavihesabu, leo hii licha ya vitabu vya shuleni, karibu 50% ya wanafunzi wanavitabu vyao binafsi n.k.
  • Kuwepo na walimu wengi waliohitimu/degree hata wengine bado hawajapata ajira, hivyo kusukumwa ama kuanzisha tuition center zao au kufundisha mwanafunzi mmoja mmoja au vikundi. Aidha wanatengeneza majarida, vitini n.k ambavyo ni msaada mkubwa kwa wanafunzi.
  • Ueleo wa wazazi katika kutambua umuhimu wa elimu. Hii inasaidia kwa vile wazazi wengi huwasukuma watoto wao katika kusoma, ikiwa pamoja na kushirikiana na walimu katika maendeleo ya mwanafunzi.
  • Hata wanafunzi wasio na wazee wenye ueleo, hufuata mkondo wa wanafunzi wenzao wenye mwanga na kufanya juhudi zao kuongezeka.
  • Kuongezeka kwa shule za private za A-Level
  • Kuongezeka kwa shule za A-Level za serikali, hususan za wasichana wenye hasira na kitabu.
  • Na jingine ni kuongezeka kwa shule za kata za O-Level pia ni chachu kubwa ya ufahamu wa elimu.

Aidha Kuongezeka kwa wanafunzi wanaofanya mitihani ya private ni kiashiria kingine kuwa elimu haijabaki pale pale. Na kizuri zaidi si tu kuwa wanafunzi wa private candidate wameongezeka bali hata ufaulu wao ni mzuri kwa vile kuna walimu wa kutosha wataaluma, vitendea kazi n.k.

Mwisho: Tusiibeze elimu yetu, ni yenye ubora na umakini mzuri hasa zile shule za kata. Shule za kata zina wahitimu wengi leo hii chuo kikuu kuliko mnavyodhani, na wanafanya vizuri sana. Pengine hawatoi ma- TO, lakini wapo hapo kati kati.
 
Back
Top Bottom