Mbona wakati wa sasa watu wa PCM, PCB, CBG wanafaulu sana kidato cha sita kuliko enzi zetu au kizazi hiki ubongo wao mzuri zaidi?

Mkuu maadili ya mtoto yanachangiwa na wazazi wapo vijana wengi Wana maadili mazuri Tu Kwa sababu wamelelewa vizuri, usisubili dunia imfundishe mtoto wako atakutana na mengi na maadili yatakuwa mabaya,mwongoze kijana wako apate uelewa

Upo sawa kabisa ndio maana huko juu nimehusisha na kupungua kwa maadili ndio chanzo cha kuporomoka kwa elimu
 
Nimetazama matokeo nikagundua tofauti ya miaka yetu n'a sasa.. Nimeona vijana wa kidato cha sita PCM.. PCB... CBG wakifauli kuliko miaka ya 2011 kurudi nyuma
Maji yameongezwa ili uji uwe mwingi.
 
Tanzania bado watu wengi wana kasumba ya kuona kuwa masomo yanayofelisha wanafunzi kwa wingi ndiyo hutowa ma-graduate wenye ujuzi. Bado tuna ile kasumba ya kuona kwa mfano chuo kikuu kinachofelisha sana ndiyo ''hupika'' wanachuo wazuri. Hii ni kasumba mbovu. Wanafunzi kufeli kwa wingi inaonyesha kasoro kwenye ufundishaji au kutahini. Siku hizi njia za wanafunzi kusoma zimekuwa nyingi hasa baada ya kuingia kwa internet. Pia uelewa na umuhimu wa elimu unaonekana zaidi kuliko zamani.

Apo umenenaa kaka
 
Hakuna maswali mapya, ni yale yale ya miaka ya nyuma yanajirudia na wanasoma of course, tuition kila sehemu na solving as well!

Tusilinganishe usomaji wa mwaka 2000 na wa sasa, teknolojia inakua tukubali mabadiliko wala hakuna mambo ya utekelezaji wa ilani hapo....

I stand to be corrected....!
 
PGM bado Ngoma inogile sijaona tatu ya PGM
Wakati nasoma nioidhani Geography no rahisi na ningefaulu zaidi ya physics na maths, matokeo yake Geography nilipata marks za chini zaidi.

Shida kubwa ni kwamba, tuliosoma PGM tulikuwa tunapiga msuli zaidi kwenye physics na maths huku Geography ikiwa ni 'somo rahisi tu'!!
 
Ukiwa unapenda kusoma you tube kuna lectures nzuri sana, topic yeyote unayotaka. Sisi hatukuwa navyo hivyo. Kitabu cha ABBOT kitatembea kutoka chuo kikuu mpaka Mbagala
Ebu mkuu nipe lecture mzuuri wa physics anaepatikana youtube mkuu
 
Mbona sijawahi kumuona mwanafunzi yoyote yupo kwenye mtandao anasolve physics au anaangalia excretion system na kujifunza zaidi naona wanaenda tuition kama wanakwenda disco mtoto amejiremba hadi mwalim anaona uvivu kumtizama hiyo technolojia inayofanya watu wafaulu sana ni ipi hiyo?
 
Miaka ya nyuma mtu akifaulu amefaulu kweli na kichwani yupo vizuri, uzuri aina ya walimu inajulisha nini kinaendelea kwa sasa na hata mitihani imekua dhaifu sana, serikali boresheni mazingira ya walimu zama zinabadilika kuishi kiujamaa na walimu ni dhambi
Ni kweli mkuu ukilinganisha form six wa zamani na wa Sasa ni tofauti kabisa uelewa wao.
Imagine hao waliofaulu form 6 na kwenda chuo kikuu hadi kumaliza degree ni weupe sana upstair.
Wengine ndio tupo nao humu hata kuandika kiswahili cha kujieleza tu au kujitambulisha ni shida.
 
Tanzania bado watu wengi wana kasumba ya kuona kuwa masomo yanayofelisha wanafunzi kwa wingi ndiyo hutowa ma-graduate wenye ujuzi. Bado tuna ile kasumba ya kuona kwa mfano chuo kikuu kinachofelisha sana ndiyo ''hupika'' wanachuo wazuri. Hii ni kasumba mbovu. Wanafunzi kufeli kwa wingi inaonyesha kasoro kwenye ufundishaji au kutahini. Siku hizi njia za wanafunzi kusoma zimekuwa nyingi hasa baada ya kuingia kwa internet. Pia uelewa na umuhimu wa elimu unaonekana zaidi kuliko zamani.
👍
 
Magoli yamepanuliwa, mitaala imerahisishwa, vitabu and other learning materials vimekuwa kama makaratasi ya kufungia vitumbua, mitihani imerahishwa hadi physics kuna multiple choice, hakuna ku derive formula kama zamani
 
Kwahiyo masomo yakiwa magumu ndio ubora wa elimu?
 
Kwasisi tuliofanya paper kama 'PC' mambo yamekuwa magumu kidogo sijui tatizo lipo wapi maana lile Paper tulitusua sana.

Anyway!! Ngoj mwakani tutupe tena karata huenda malengo yetu ya kupiga one ya 8 yakatimia.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom