tinkanyarwele
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 2,017
- 1,940
Kama we in mdau wa elimu jibu utakuwa nalo, ukweli ni kwamba vijana wa siku hizi ni hovyo sana(siyo wote), sijajua vizuri lengo LA serikali ni nini haswa, mbali ya kwamba uwezo wao ni mdogo sana kuliko kawaida lakini wanazidi kufanya vizuri kuliko miaka yote. Mfano matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa juzi ndo yametia simanzi, watoto wetu wamefanya vizuri kuliko uwezo wao, hatukatai yote mema, lakini inatisha kuona kijana tayari amefanya vizuri kidato cha 6 lakini bado hana uwezo wa kuchanganua mambo madogo hata ya kawaida, mfn hai kuna mzazi ananiambia binti yake amepata 2 ya point 10, lakini anajua fika Huyo binti yake hakuwa na uwezo wa kupata alama hiyo...huu ni mfano halisi. Ila yote tunashukuru acha maisha yaendelee.