Mbona Waganda Hawapo!!!

waganda hawaongei kiswahili na wanaoongea kusoma kiswahili wanapata tabu. Na wanaoweza kusoma kuandika ni wachache zaidi. JF imetawaliwa na kiswahili. Mi nashauri kuanzia leo tuwe tunatumia kingereza tu hapa au mnasemaje wana JF?
 
Me370, heshima yako,

Mimi naona kiswahili sawa tu maana we have to have our
own identity.Hao waganda kama namna gani vipi si inabidi
tuwafundishe kiswahili?...ama mnasemaje?
 
Good observation!

Nadhani EA section covers all Ug, Burd, Rwn, Kny na Tz!

Kenya was given a special section tokana na homa ya uchaguzi!

Sasa sii unaona M7 alikimbilia kuunga Kibaki mkono mara moja? Na Kagame alisema eti Jeshi litumike haraka?

Tz walikuwa neutral..na hii imetupa heshima!

Mimi naona tuwakaribishe tu wenzetu nao wazoee Kiswahili!

Sii mnajua Kiingereza ni lugha ya mzungu?
 
waganda hawaongei kiswahili na wanaoongea kusoma kiswahili wanapata taabu. Na wanaoweza kusoma kuandika ni wachache zaidi. JF imetawaliwa na kiswahili. Mi nashauri kuanzia leo tuwe tunatumia kingereza tu hapa au mnasemaje wana JF?

Tunajitahidi sasa kufanya Kiswahili kiwe lugha ya bara hili, na kwa kuanzia kimekubalika hata ktk AU...kwa nini tukiengue ktk kuwasiliana na Waganda badala ya wao kujitahidi kujifunza lugha ya bara hili?

Kuna nchi tisa zinaongea Kiswahili, Waganda inabidi wajitahidi kuongea lugha hii na waache kufikiri kuongea kiswahili ni upungufu fulani wa kutokijua kiingereza.
 
Kiswahili kinawapa waganda hisia mbaya kihistoria. Enzi hizo za hayati Idd Amin Dada kiswahili kilikuwa kinaongewa sana jeshini (uganda) kwa wingi, na wakati ule wanajeshi walikuwa wakatili sana, kwa hiyo ukiongea kiswahili watu wanakukimbia na hupati rafiki wa kuongea naye labda awe mjeshi mwenzako. Hii swahili stigma imeendelea mpaka leo. Kwa kuwa tunaingia EAC then Uganda hawana jinsi na ni lazima wajifunze kiswahili otherwise they will be an island in East Africa Coop.
 
Nilisomea shahada yangu ya 1 Uganda. Kiujumla, ni watu wenye maringo. Mbona dunia nzima isiwe na 'English stigma' baada ya ukoloni? Hawataki tu kukubali kiSwahili, the reasons given are totally and completely baseless.
Jambo jingine, wanatudharau waTZ, 2kiwaalika hapa 2taishia kupigana virtual ngumis!
PS SIWABAGUI, ACTUALLY AMONG MY GREAT FRIENDS 3 R UGANDAN
 
Kiswahili kinawapa waganda hisia mbaya kihistoria. Enzi hizo za hayati Idd Amin Dada kiswahili kilikuwa kinaongewa sana jeshini (uganda) kwa wingi, na wakati ule wanajeshi walikuwa wakatili sana, kwa hiyo ukiongea kiswahili watu wanakukimbia na hupati rafiki wa kuongea naye labda awe mjeshi mwenzako. Hii swahili stigma imeendelea mpaka leo. Kwa kuwa tunaingia EAC then Uganda hawana jinsi na ni lazima wajifunze kiswahili otherwise they will be an island in East Africa Coop.

Sawa kabisa bwana Jafar, on top of that ukiongea kiswahili wanajua lazima wewe ni mwizi
 
tusiwabague Waganda ni wenzetu hata JOHN OKELLO alitusaidia......!tuwawekee sehemu kwa maendeleo ya EAST AFRICA!
 
Kiswahili kinawapa waganda hisia mbaya kihistoria. Enzi hizo za hayati Idd Amin Dada kiswahili kilikuwa kinaongewa sana jeshini (uganda) kwa wingi, na wakati ule wanajeshi walikuwa wakatili sana, kwa hiyo ukiongea kiswahili watu wanakukimbia na hupati rafiki wa kuongea naye labda awe mjeshi mwenzako. Hii swahili stigma imeendelea mpaka leo. Kwa kuwa tunaingia EAC then Uganda hawana jinsi na ni lazima wajifunze kiswahili otherwise they will be an island in East Africa Coop.

safi ndugu Jafar,

Mie nakumbuka katika pitapita zangu Kampala nilikutana na
bwana mmoja anayeendesha teksi na nikamuuliza mbona Kiswahili
has not taken root in Uganda.Naye akaniambia kama usemavyo... sababu ni za kihistoria.

Kando na hio ishu na wanajeshi, alinitonya pia kua Kiswahili kinakua linked na slave traders were East Africa ambao walitoka Pwani ya Afrika Mashariki na walikua wanaongea kiswahili kingi. Kwa hivyo they wanted to shun the slave master's language.

Hata hiyvo kuna mtu ametoa notion kua kama tunaangalia atrocities basi we have no business speaking English maana it is the language of the colonilialists who took our land and freedom then subjected us to servitude.

Kwa hivyo ni sawa kujaribu kuwa-challenge waganda kuongea kiswahili na pia kushiriki katika midahalo ya kiswahili ili kukuza lugha.Kiswahili is here to stay na kama namna gani vipi it is expected to grow in leaps and bounds for the benefit of posterity.
Naomba kuwasilisha
 
Sawa kabisa bwana Jafar, on top of that ukiongea kiswahili wanajua lazima wewe ni mwizi

Hahaha!!!!!....hapo Ushirombo umeniacha hoi kweli!
Kwa hivyo kwa mujibu wa hio statement wabongo wote wezi sio!!?
 
MI NAONA BADALA YA KUWASEMEA HEBU TUWAPE NAFASI WAO WENYEWE WASEME KUHUSU KISWAHILI NA WAO.....!
 
MI NAONA BADALA YA KUWASEMEA HEBU TUWAPE NAFASI WAO WENYEWE WASEME KUHUSU KISWAHILI NA WAO.....!

Kweli kabisa mahesabu,
lakini swali ni je jamaa wapo humu kwa kweli?
Yaani hata sijaona forum za waganda.Anybody out there
with a link?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom