Mbona wabunge wa CCM wanakumbana na aibu kubwa Sana majimboni kwao?

Ata America watu wanajazana kuwasikiliza wabunge wao
Hao ni followers wao yaani Kuna mambo wanakuwa wanayakubali kutoka kwao hivyo wanakwenda kuwasapoti, Sasa huku mbunge anakuja akiwa Hana alichofanya kiasi cha kuwakuna watu mioyo yao na yeye anakaa jukwaani kulalamika kama wananchi Sasa nani atamfollow mtu wa hivyo kiasi cha kuacha kazi zake?
 
Wote waliopata kitonga uchaguzi ujao pia watapata kitonga...

Otherwise watakiona cha moto
 
Shida iko hapo jamaa aliwapambania wote waingie Bungeni kwa kutumia tume ya uchaguzi,polisi na usalama wa Taifa kwa nia moja ovu sana mabadiliko ya katiba yapite bila kupingwa 100% atawale milele sawa lakini ya kesho ni Mungu tu ndie ajuae.imekuwa historia.
 
Hali ni tete kwa wabunge wa CCM wanaoenda majimboni kwao, kufanya mikutano ya hadhara na wananchi wao. Katika hali ya kushangaza wabunge wa CCM waliopata kura za kihistoria kwa kupata ushindi mkubwa, wanakosa kabisa ata kukusanya watu 50

Wiki iliyopita Prof Mkenda alienda Rombo kufanya mkutano, alikosa watu kabisa,ikabidi mkutano aachane nao.

Jana Mbunge wa Nyamagana Mabula amepata aibu ,ya karne kwa kukosa watu kwenye mkutano wake, yaani pamoja na ukubwa wa Nyamagana bado Mabula alikosa ata watu 50 wa kumsikiliza, imebidi ahairishe mkutano.

Jana Prof Kitila mkumbo alipata aibu ya mwaka, pale alipokosa watu kwenye mkutano wake wa hadhara, yaani pamoja na jimbo la ubungo kuwa na watu wengi, Mkumbo amekosa ata watu 50 wa kuwahutubia.

Tatizo liko wapi kwa baadhi ya wabunge wa CCM kukosa kabisa uungwaji mkono kutoka kwa Raia, wakati walichaguliwa kwa kura nyingi sana

View attachment 2135981
View attachment 2136014
nasikia hata kuchefuchefu unavyoita wabunge. walichaguliwa na nani?
 
Back
Top Bottom