Mbona vile vyama vya siasa vidogo vidogo havihamasishi wanachama wao kuwania Uspika?

BURUTA

JF-Expert Member
Apr 27, 2015
589
765
Inaelezwa Tanzania ina jumla ya vyama vya siasa takriban 19, lakini inajulikana vingi vya hivi ni pro-CCM havifanyi shuguli zozote za siasa, yaani vipo vipo tu vikivizia matukio ya kitaifa.

Hujitutumua tu pale utawala unahitaji kuvitumia katika kuvibana vile vyama vya upinzani vikubwa hasa CDM, kwa mfano katika mchakato unaoendelea wa marekebisho ya katiba ambapo utawala hutumia utitiri wao katika kupitisha hoja na ajenda zake kwa maelezo kwamba maamuzi yalifikiwa kidemokrasia.

Sasa kama vyama hivyo vinajinasibu ni vyama vya siasa makini basi wahamasishe wafuasi wao kuchukua fomu kuwania uspika, viache kutaka kujulikana pale tu utawala unapotaka kuvitumia kwa haja zake.

Chama kikubwa kama CDM kwa mfano kina sababu zake kususia zoezi hilo.

NAWASILISHA.
 
Back
Top Bottom