Mbona umetafuta balaa - nakusikitiakia

Lutala

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
848
103
Daktari abaka mtoto wa ofisa usalama

DAKTARI wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Haruna Nyagoli, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa, kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike ambaye baba yake ni Ofisa Usalama wa Taifa wa Wilaya ya Mbeya.

Binti huyo, ambaye jina tunalo, alipatwa na mkasa huo baada ya kutishiwa silaha, kabla ya kumuingilia kinguvu.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata na kuzifanyia uchunguzi wa kina zinaonyesha kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 3 umbali wa kilometa zipatazo 30 kutoka katikati ya Jiji la Mbeya, baada ya daktari huyo kutumia nguvu na kumteka binti huyo anayetarajiwa kuanza masomo katika Chuo Kikuu cha Tumaini.

Habari ambazo zimethibitishwa na baba yake mzazi (DSO) wa Wilaya ya Mbeya, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kutaka sheria ichukue mkondo wake.

Tanzania Daima ilipofuatilia kwa undani tukio hilo ilibaini kuwa lilitokea Novemba 3, majira ya saa 9 alasiri katika hoteli moja inayomilikiwa na Kanisa la Uinjilisti la Mbalizi (MEC), ambako huko kuna hosteli na kwamba kwa ushawishi alimshawishi binti huyo kwa kumpa lifiti, lakini alikijuta akipelekwa nje ya mji.

Mashuhuda wa tukio hilo na habari za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinadai kuwa daktari huyo baadaye kumfikisha binti huyo kwenye hoteli hiyo, alimlazimisha kufanya naye mapenzi kwa kutumia bastola yake yenye namba za usajili MD/IR/9571/2010, kisha alifanikiwa kutimiza azima yake.

Mganga Mkuu wa Hosiptali ya Mkoa wa Mbeya, Haruon Machibya, alipohojiwa akiri kuwapo daktari huyo katika hospitali yake na kudai hivi sasa yuko safarini mkoani Morogoro.

“Hivi sasa nipo Morogoro, ni kweli Dk. Nyagoli tunaye katika hospitali ya mkoa lakini sina taarifa za tukio lolote linalomhusu, nitafuatilia ili kuweza kujua ni kitu gani kimetokea huko,” alisema Dk. Machibya.

Baba mzazi wa binti huyo ambaye ni Ofisa Usalama wa Wilaya ya Mbeya, alipohojiwa alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuomba sheria ichukue mkondo wake na kwamba hawezi kuliongelea kwa kina suala hilo akihofia litamchanganya binti yake.

“Tukio hili limetokea, tupo kwenye vyombo vya dola, naomba tuiachie sheria ichukue mkondo wake, sipendi jambo hili tuliingize kwenye vyombo vya habari linaweza kumchanganya zaidi binti yangu,” alisema ofisa huyo na kuthibitishiwa na Tanzania Daima kuwa haitatumia majina yao.

Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi, alipotafutwa kuelezea tukio hilo, simu yake haikuweza kupatikana kutokana na kuita bila kupokewa.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom