nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Tumeweka Makala kadhaa kuhusu Wazanzibari jinsi wanvyoukataa muungano na Bara wanaita ni wa kichawi, wakila maneno mabaya; lakini Moderator hapa anaiondoa kuna sababu? Au tunatakiwa kuongelea tu tofauti Kati ya CCM na Chadema na sio matatizo mengine? Mimi naota tatizo kubwa kwetu ni huu muungano tunahitaji kuujadili kwa ufasaha wakati katiba mpya inatakiwa.
Chini ni makala kuhusu Muungano jinsi wazanzibari wanavyouona jinsi ulivyo...
MAFUTA YETU HATUTOI NGO!
Na: Malik Nabwa
Kama kuna kitu kilichopangwa na kushuhulikiwa kwa umakini mkubwa hapa nchini ni Muunagano wa Tanzania na Zanzibar. Yaani kila kitu ambacho bara wanakifanya juu ya Muungano basi huwa very strategic kiasi ambacho mikakati hiyo inavyopangwa kwa umakini mkubwa laiti ingekuwa inatumiwa kuleta maendeleo ya Taifa basi Taifa hili lingekuwa mbali kimaendeleo.
Mara kadhaa tumejaribu kuonesha kuwa muungano wa Zanzibar na Tanganyika haukufanywa hata kwa chembe moja ya nia njema. Naufananisha kabisa na mungano wetu na chama cha wachawi huko Gingingi. Kwa anaewafahamu wachawi vizuri basi umoja wao huwa hauko katika nyoyo zao bali hamu na matakwa ya nafsi zao tu. Wachawi hawana chembe ya nia njema wala upendo kati yao na walivyonavyo kwa mfano watoto wao au hata familia zao. Hivi ndivyo ulivyo Muungano kwa wenzetu wa bara dhidi yetu.Ni chama cha wachawi tu kila mtu ana lengo lake tena leno baya dhidi ya mwenzake.
Tumeona kuwa msingi wa kuungana kwetu ulikuwa wa magube matupu. Kwanza hakukuwa na ulazima wa kuungana kwani ukiungana na mchawi lazima siku moja atakuliza tu au kukutia wanja jicho moja, tumulize shekh Karume kama tunataka ushahidi juu ya hili. Pili, mara tu baada ya Muungano tulishuhuduia mambo kadhaa ya kuipora Zanzibar kuwa nchi na kujitegemea kwake. Tuakunganisha vyama na kila kitu. Ikafika wakati lazima kila kitu kiamuliwe bara. Hii ndio taswira halisi ya Muunagno wa kinafiki sawa na muungano wa Kichawi. Muungano usio na nia njema siku zote hukimbilia msihipa ya kuvutia pumzi ya mwenza wake na kuidhibiti. Ikishafanya hivyo mwenye kuzibwa pumzi lazima atii amri na akishindwa basi hana hiari ila ni kufa au kukosa kila kitu kabwi na mtindi. Muungano wetu sisi Wazanzibari umetufikisha hapa.
Si vibaya tukijikumbusha kidogo ajenda za siri za Muungano kutuchagulia viongozi wa juu kama moja ya mbinu yao ya kuendelea kututawala na kuimaliza mirija michache ya kuvutia pumzi iliyobaki tuanzie na Raisi wa Kwanza. Raisi Karume alipokuja tanabahi tu kuwa kujiingiza katika Muungano lilikuwa kosa la jinai akataka kujitoa pale alipoanza kubwatuka hadharani; muungano mwisho Chumbe huku akisahau kuwa ukishaingia uchawini huwezi kutoka. Yaliyomkuta ndio yale. Mauaji yake yalikuwa hayahitaji uchunguzi wa CIA,FBI, KVB, wala Scotland Yard.
Nini kilitokea baada ya kikwazo cha kuendeleza Ubabe wa kutaka kuungoa Muungano kuondoka yaani baada ya kifo cha Sheikh K. Dodoma ilipanga nani ni mtu wao atakaeweza kutimiza azma yao ya kuidhibiti mirija muhimu ya kuvutia pumzi ya Zanzibar na kuiweka chini ya himaya ya Muungano. Akaletwa Jumbeambae alikuwa mwenzao badala ya Sefu BAKARI alietakiwa na Baraza la Mapinduzi lenyewe. Kwa upande mmoja ilikuwa shufaa kuwekwa Jumbe kuliko Sefu Bakari maana japo Seifu alikuwa hana malengo na Muungano lakini alikuwa kichwa maji kuliko hata Karume kwa hiyo hata angewekwa yeye tusingepata shufaka yoyote. Afadahali huyo Jumbe ni anagalau afadhali ya kungtwa na nge ukakoswa na tandu, wala si afadhali kitu maana mchawi ni mbaya tu hata awe vipi.
Muungano ulifanikisha azma yake kwa kumuweka Jumbe. Baada ya kupandikiza mtu wao huyu wakajichukulia hatua moja muhimu ya kuudhibiti mshipa mkuu wa pumzi wa Zanzibar. Nao ni pale Jumbe alipokubali Kuunganisha vyama na Nyerere mwaka 1977. Katika kosa kubwa katika historia ya Zanzibar ni hili alilolifanya Jumbe (The grave mistake over Zanzibar future stake in the Union). Kwa kuunganisha Chama ndio alijimaliza yeye mwenyewe kama Rais kamili wa Zanzibar na pia ikawa kashaiondolea kinga dola ya Zanzibar. Kuanzia hapo ndio Zanzibar ikawa ni sehemu tu ya Jamhuri ya Muunagano.
Kama nilivyotangulia kusema hapo awali kuwa ngoma ya kichawi haina mwisho mwema. Mwema wako leo kesho ndie mbaya wako wa mwisho. Jumbe akawa amejitia kitanzi mwenyewe na bila kinga wala hifadhi akatolewa kikoa katika hali ya aibu kabisa na idhilali. Haya ndio malipo ya kushirikiana na watu wabaya. Tukumbuke kuwa Nyerere alimtimua Jumbe baada ya kuhakikisha ameshashikilia maeneo muhimu ya Zanzibar. Kwa mfano kama Jumbe hakuunganisha vyama Nyerere angepata nguvu wapi ya Kumfukuza? Lengo lake ikawa limefanikiwa.Kinachofuata sasa ni kungatuka maana mission accomplished.