Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,885
Najiuliza tu, Maandamano na kesi zote wanafungua zinahusiana na wao kushika madaraka. Mbona hawaandamani serikali ikifungia wakulima mipaka, mbona hawaendi mahakamani kupinga sheria za kodi etc. Mbona hawaendi mahakamani kupinga makato ya bodi ya mikopo.
Kama wako kwa maslahi ya wananchi si wanaweza anza na hapa. Leo nimemkumbuka Mtikila ndiyo maana nimeandika hili, alikuwa anashinda mahakamani japo alijua si rahisi kuishinda serikali. Kesi zake kama ile ya kudai mgombea binafsi ilifungua sana watu masikio na nafikiri alishinda.
Wanasiasa wangeonyesha kupigania maslahi ya wananchi wangekubalika sana.