Mbona sijawahi ona wanasiasa wakiitisha maandamano au kwenda mahakamani kupigania maslahi ya Wananchi?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,885
Najiuliza tu, Maandamano na kesi zote wanafungua zinahusiana na wao kushika madaraka. Mbona hawaandamani serikali ikifungia wakulima mipaka, mbona hawaendi mahakamani kupinga sheria za kodi etc. Mbona hawaendi mahakamani kupinga makato ya bodi ya mikopo.

Kama wako kwa maslahi ya wananchi si wanaweza anza na hapa. Leo nimemkumbuka Mtikila ndiyo maana nimeandika hili, alikuwa anashinda mahakamani japo alijua si rahisi kuishinda serikali. Kesi zake kama ile ya kudai mgombea binafsi ilifungua sana watu masikio na nafikiri alishinda.

Wanasiasa wangeonyesha kupigania maslahi ya wananchi wangekubalika sana.
 
Najiuliza tu. Maandamano na kesi zote wanafungua zinahusiana na wao kushika madaraka. Mbona hawaandamani serikali ikifungia wakulima mipaka, mbona hawaendi mahakamani kupinga sheria za kodi etc. Mbona hawaendi mahakamani kupinga makato ya bodi ya mikopo.

Maslahi ya wananchi kwa elimu yako ndogo nini? Kwa akili yako katiba bora,uongozi bora,utawala wa sheria na mfumo mzuri wa kuwapata viongozi wazuri si maslahi ya wananchi?
 
Mwanasiasa akienda kudai haki za wakulima na hayo makundi mengine mahakamani, ataambiwa aache kufanya siasa kwenye kila jambo. Na usishangae hata wale anaotaka kuwatetea baadhi yao wakahongwa na watesi wao, ili wawaambie hao wanasiasa wasilete siasa kwenye mambo yao maana serikali ina mpango wa kutatua matatizo yao. Na hayo makundi wakiwa kichwa ngumu wataishia kufanyiziwa kabisa.
 
Najiuliza tu. Maandamano na kesi zote wanafungua zinahusiana na wao kushika madaraka. Mbona hawaandamani serikali ikifungia wakulima mipaka, mbona hawaendi mahakamani kupinga sheria za kodi etc. Mbona hawaendi mahakamani kupinga makato ya bodi ya mikopo.

Kama wako kwa maslahi ya wananchi si wanaweza anza na hapa. Leo nimemkumbuka Mtikila ndiyo maana nimeandika hili, alikuwa anashinda mahakamani japo alijua si rahisi kuishinda serikali. Kesi zake kama ile ya kudai mgombea binafsi ilifungua sana watu masikio na nafikiri alishinda.
Wanasiasa wangeonyesha kupigania maslahi ya wananchi wangekubalika sana.
Na kwanini wakulima Wenyewe wakifungiwa mipaka hawaandamani, maana yake hawaoni tatizo.

Sasa unataka wanasiasa wapiganie kitu ambacho wahisika wenyewe hawaoni tatizo ??

Kuhusu tatizo la sheria za kodi, source huanzia bungeni.

Huko Wanasiasa hasa wa upinzani huwa wanasimama imara na kupinga sheria kandamizi za kodi, lakini huwa zinapitishwa kibabe.

Hata vyama vya wakulima huwa vipo tu havioni tatizo.

Wanaotakiwa kuziheshimu yaani wafanyabiashara wala huwezi kuwaona hata wanapinga, maana yake wameridhika.

Hata viongozi wa sekta binafsi huwa wapo tu na hawaoni tatizo.

Kwahiyo, hapa kuna mawili.

1. Ukiona mwenzio amepatwa na janga simama naye, ukimwacha peke yake atakosa nguvu atadhibitiwa. Na siku wakija kwako pia na wengine wanakaa kimya unakomeshwa.

2. Huwezi kukaa tu kama maiti, hujihusishi na chochote lakini unataka vitu vizuri. Utasikia Lissu pambania katiba mpya, ajira,
Soko la wakulima et al utafikiri hayo mambo ni kwaajili yake tu na watoto wake.
 
Mitaa iko mingi Tanzania subiri hapohapo watapita kukutangazia.
 
Maslahi ya wananchi kwa elimu yako ndogo nini? Kwa akili yako katiba bora,uongozi bora,utawala wa sheria na mfumo mzuri wa kuwapata viongozi wazuri si maslahi ya wananchi?
Mara nyingi wakitetea hayo mambo huwa ni pale yanapokwamisha njia yao ya kushika madaraka.
 
Na kwanini wakulima Wenyewe wakifungiwa mipaka hawaandamani, maana yake hawaoni tatizo.

Sasa unataka wanasiasa wapiganie kitu ambacho wahisika wenyewe hawaoni tatizo ??

Kuhusu tatizo la sheria za kodi, source huanzia bungeni.

Huko Wanasiasa hasa wa upinzani huwa wanasimama imara na kupinga sheria kandamizi za kodi, lakini huwa zinapitishwa kibabe.

Hata vyama vya wakulima huwa vipo tu havioni tatizo.

Wanaotakiwa kuziheshimu yaani wafanyabiashara wala huwezi kuwaona hata wanapinga, maana yake wameridhika.

Hata viongozi wa sekta binafsi huwa wapo tu na hawaoni tatizo.

Kwahiyo, hapa kuna mawili.

1. Ukiona mwenzio amepatwa na janga simama naye, ukimwacha peke yake atakosa nguvu atadhibitiwa. Na siku wakija kwako pia na wengine wanakaa kimya unakomeshwa.

2. Huwezi kukaa tu kama maiti, hujihusishi na chochote lakini unataka vitu vizuri. Utasikia Lissu pambania katiba mpya, ajira,
Soko la wakulima et al utafikiri hayo mambo ni kwaajili yake tu na watoto wake.
Umeongea vizuri. Lakini hapo kwenye point ya pili huoni hilo linasababisha na wao waachwe peke yao yakiwakuta kama kuibiwa kura nk. Hao wakulima na wafanyabiashara unakuta hawajui hata waanzie wapi kudai haki zao, wanasiasa wanajua pa kuanzia. Wanasiasa wakianza kuwapigania wananchi, wananchi hawatawaacha yakiwakuta.
 
Mara nyingi wakitetea hayo mambo huwa ni pale yanapokwamisha njia yao ya kushika madaraka.
Halafu kitu usichokijua ni kwamba wanasiasa lengo lao ni moja.

Nitakupa mfano: Magufuli hana tatizo kabisa na Tundu Lissu ndio maana alikuwa tayari kumpa xheo akae kimya, ila tatizo kubwa la Tundu Lissu kwa Magufuli ni kupita mitaani anawaamsha waliolala.

Hapo ndio utakosana na CCM, kama Wewe ushakuwa mjanja wanakupa vinono utafune, ukianza kupita pita mitaani unawaamsha waliolala hapo ndio utakosana na watawala.

Kama mtu anadhulumiwa na yeye mwenyewe haoni tatizo, ukianza kumuelimisha hapo utakosana na watawala.

Mfano mwingine.

Mtawala anakutesa, Mzungu au mwanasiasa fulani anakutetea uondokane na hiyo adha, yule yule anayejutesa anakuja kukwambia huyo anatekutetea anakudanganya, siyi mtu mzuri kwako.

Sasa hapo ni akili yako ndio inatakiwa kutumika.
 
Wananchi ndio hutetea masilahi ya wanasiasa,jamaa wameaminisha kuwa matatizo yooote ufumbuzi wake ni upinzani kuingia madarakani.
 
Haya fanyeni hima muandamane kupinga watoto wenu kushindwa kuendelea na masomo kwa uhaba wa madawati wakati serikali yenu pendwa inanunua madege kwa cash na hayafanya kazi yapo parking kama urembo.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom