Mbona sasa hivi matangazo ya kampuni za BETTING yameshamiri sana?

Kupewa tuzo sio qualification kuwa mtu ni bora kama inakwenda kinyume na standards za jamii. Kumbuka hata wacheza filamu za ngono hupewa tuzo, je inamaanisha wao nao hawana shida katika jamii?!

Mimi nazungumzia maudhui wanayokuwa wanayajadili katika vipindi vyao muda mwingi. Kupewa tuzo kwasababu ya habari za kijamii mbona kama ni minor issue.
Kwahiyo Wizara itoe tuzo kwa mwanahabari mtu anayefanya mambo kinyume na standards za jamii?..This is Bongo but hilo haliwezekani.

Geah Habib sio Mbovu kama ulivyomsema hapa.

I'm out.
 
Kwahiyo Wizara itoe tuzo kwa mwanahabari mtu anayefanya mambo kinyume na standards za jamii?..This is Bongo but hilo haliwezekani.

Geah Habib sio Mbovu kama ulivyomsema hapa.

I'm out.
Hakuna cha am out, rudi hapa tumalizane kwanza.

Ipo hivi. Mfano kuna mtu ni mwizi anaiba na kuua watu ila anatoa sana misaada kwa masikini na kusaidia miradi ya maendeleo utampa tuzo ya raia bora tu kwasababu anakufurahisha kwa yale anayofanya ili aonekane kuwa ana mazuri ila akakuficha kuhusu haiba yake ya matendo nyuma ya pazia au kizani?!

Point yangu sijamlenga huyu mtangazaji m'moja wapo wengi na huwa wanatangaza wakiwa kundi. So nimemtaja kama mshirika.
 
Yaani hadi zile redio zilizoheshimika ukifungua tu waatangaza makamari yao ati kuna mil 10 leo inakusubiri bonyeza 4 nenda....weka 1000 tu na mijinga inaweka.....

Nendeni mkabeti kama Mancity win n und unaona matokeo, haya mambo ya kuwa wajinga. Eti halloo uko wapi umeonaa salioo ndio kama hujui mjini shule wao ndio wanaanza tangaza lak 2 zimeingia umeziona ndioo, fasta wanakata asije kuharubu.

Amkeni hakuna slope ya maisha kwa buku hasa mnaopewa hela ya chakula na waume zenu mnabetia mkome nasema mtalaaniwa. Kila rediioo zimekuwa kero ndio maaana utitri wa redio kila siku.

Observations is also allowed
 
Kama redio moja leo iko huku ....amearibu kabisa ati wahi haraka kuna mil 900 mwezi huu zinakusubiri weweww yaan moto unakusubiiri ami jiandae
900M
MNALIPWS NGAPI MSHAHARA AISEE
 
Habari wakuu.

Hali ya sasa katika redio stesheni za hapa Tanzania imekua ya kukera sana, kutwa kucha ni matangazo ya kamari redioni pia redio stesheni zimekua zinachezesha kamari (wenyewe wanaita bahati nasibu).

Mfano: Mchongo pesa.

Hakuna tena "radha" ya kufatilia vipindi vya redio.

Wizara ya Habari chini ya serikali ya Samia Suluhu imehalalisha wananchi wake kucheza kamari kutwa kucha ili kujipatia kipato cha njia ya kubahatisha.

Hizi kamari zinachochea watu kutowaza namna ya kujiongezea kipato wamekaa kutegemea kubahatika na hiyo michezo kila siku.

Serikali ikaamua kuhalalisha kamari nchini kwa kupunguza kodi kutoka asilimia 20% hadi 10% ilihali vitu vya msingi wameongeza kodi kandamizi kwa wananchi wake mfano TOZO za miamala, kodi ya jengo kila ununuapo LUKU hata kama ni mpangaji utailipa tu inderect.

Serikali ya Samia Suluhu kwanini mmebariki haya mambo ya kipuuzi yaendelee kushamiri nchini?

Haya hizo kodi kandamizi mnazokusanya hatuoni cha maana mnachofanya zaidi ya kununuliana mavieiti kila kukicha!
 
Kila ukifungulia Redio karibia kila stesheni ni kamari tu, kucheze kubahatisha na mapesa kutolewa, watu wanapokea mamilioni, matv, na mambo kede kede kwa kuchangiana kucheza kamari buku buku kwenye maredio.

Hapo bado kamari za kwenye mitandao ya simu, na kwenye mipira, wazee wa mikeka, na wazee wa makasino, kwezi Tanzania pesa ipo. Mfano kuna redio kila baada ya nusu saa, au lisaa yanatoka mamilioni, sasa unashangaa wanaojichangisha huko hewani mpaka mshindi achukue laki 5 mpaka 10M ni wangapi?

Kuna mmoja akanishangaza kuwa ana line tatu, zote alikua anazichezea kuona ipi itashinda au ipi yenye bahati, kweli tuna pesa.

Kuna mwana JF yoyote aliewahi kushinda kweye hizi za redio za kila baada ya nusu saa atupe mrejesho?

Mwaka flani nilifanya kazi kama customer care agent kampuni flani ya simu, kulikua na kamari flani ya kushindania magari, nadhani lilifanyika miezi kadhaa.

Siku niko kwenye majukumu yangu ya kupokea simu akapiga mteja analalamika kacheza miezi yote hashindi, kuchek kweli kacheza inakaribia 3M, nikamshauri akomae siku yake inakuja, ila nilimuhurumia.

Sasa hivi ni kwenye maredio imeshika kasi, ni mipesa tu inatolewa, alafu tunalalamika tozo.

Ngoja tuendelee kukamuliwa mpaka maji tuite mma.
Na vipindi vyao vimekosa maana/maudhui yaani kila dakika wanapigia chapuo kamali zao, kuna hao rfa hadi watangazaji wanataka kulia kisa pakua mkwanja. **** chota mihela, na hawa voda na makamali yao meeeeeeeeeeeeeengi,, sina nia ya kuharibu biashara za watu lakin hiz kamali hazina maana kwa nchi yetu. Serikali hili nalo mkalitazame
 
Wa

Ngoja wapigwe
Kufikia 2018 nilikuwa nimetumia tsh13, 700, 000 kwa ajili ya betting na pesa niliyokula ni 6,573,000 na kuanzia 2019 hadi 2022 nimetumia 370,000 na nimekula 4000.kimsingi kamali ni umasikin
 
Back
Top Bottom