Mbona sasa hivi matangazo ya kampuni za BETTING yameshamiri sana?

Eewaa hakunaga matangazo hapo UFM ni mwendo wa uchambuzi tu kuanzia saa 10 jioni hadi 1 usiku..

Au sikiliza Abood Fm kipindi cha michezo asubuhi hukuti mitongozo mingi ya kubet..
Kweli mkuu, ngoja nianze kuifatilia na Abood pia.
 
Kila ukifungulia Redio karibia kila stesheni ni kamari tu, kucheze kubahatisha na mapesa kutolewa, watu wanapokea mamilioni, matv, na mambo kede kede kwa kuchangiana kucheza kamari buku buku kwenye maredio.

Hapo bado kamari za kwenye mitandao ya simu, na kwenye mipira, wazee wa mikeka, na wazee wa makasino, kwezi Tanzania pesa ipo. Mfano kuna redio kila baada ya nusu saa, au lisaa yanatoka mamilioni, sasa unashangaa wanaojichangisha huko hewani mpaka mshindi achukue laki 5 mpaka 10M ni wangapi?

Kuna mmoja akanishangaza kuwa ana line tatu, zote alikua anazichezea kuona ipi itashinda au ipi yenye bahati, kweli tuna pesa.

Kuna mwana JF yoyote aliewahi kushinda kweye hizi za redio za kila baada ya nusu saa atupe mrejesho?

Mwaka flani nilifanya kazi kama customer care agent kampuni flani ya simu, kulikua na kamari flani ya kushindania magari, nadhani lilifanyika miezi kadhaa.

Siku niko kwenye majukumu yangu ya kupokea simu akapiga mteja analalamika kacheza miezi yote hashindi, kuchek kweli kacheza inakaribia 3M, nikamshauri akomae siku yake inakuja, ila nilimuhurumia.

Sasa hivi ni kwenye maredio imeshika kasi, ni mipesa tu inatolewa, alafu tunalalamika tozo.

Ngoja tuendelee kukamuliwa mpaka maji tuite mma.

Tatizo la waTanzania ni wachache sana wanaotumia akili.

Kwenye michezo hii ya kamari kuna mchezo mmoja tu wa kutumia akili ambao ni nusu bahati nasibu na nusu akili. Na ni mchezo ambao ukiamua kutulia kutumia akili vizuri una nafasi kubwa ya kushinda.

Mchezo huo ni wa kutabiri matokeo ya mpira wa miguu.

Basi.

Lakini wajinga ni wale wote wanaocheza michezo ambayo hairuhusu kabisa matumizi ya akili. MIchezo kama slot machine (hii ndo inawafilisi sana waTanzania), au Tatu Mzuka au Bonanza au bahati nasibu za makampuni ya simu na hizo za redioni.

Hizo ni upumbavu mkubwa kucheza.

Ukitaka kucheza michezo ya kubahatisha jifunze kubashiri mechi za mpira wa miguu. Hapo ukiwa unajua kusoma takwimu vizuri mtandaoni una nafasi kubwa ya kushinda.
 
Bingwa wa kamari za casino za mtandaoni nakuja kutolea ufafanuzi jinsi Watanzania wanavyoliwa na makamari ya kubet mpira na namba.
Njoeni kwenye casino mtafurahi
Casino tena? We unazingua! Kubeti mpira ni bora kuliko kubeti chips kwenye Casino. Kwenye mpira ukitulia uhakika wa kula upo. Lakini kwenye Casino ni full kubahatisha.
 
Concept ya kamari zote duniani ni kwamba katika kila watu 1000 mnaoliwa vihela vyenu ni chini ya watu 10 tuuu watakaopata/kushinda. Kwa maneno mengine hii maana yake ni kwamba nyie watu 990 fedha zenu zitatumika kulipa wale watu 10 na kinachobaki choootee ni faida ya mcheza kamari. Sasa serikali haiwezi kuwagusa kwa sababu wewe uliyeshinda say laki tano (za wale wenzako 990) hutapata hiyo laki tano maana itakatwa kodi ya serikali. Pili yule mchezeshaji kamari na yeye atalipa kodi serikalini kulingana na kipato ambacho nyie watu 1000 mmemchangia.. Hii kitu kuna nchi nimesikia kama India ni marufuku kabisa.
Kamari hujenga uraibu. Siku zote mchezaji anajua atashinda na hata asiposhinda leo basi atashinda kesho. Kwa mantiki hii ataendekea kucheza hadi aishiwe fedha. Kwenye makasino waendeshaji wapo radhi kukukopesha ili uendelee kucheza. Hili hufanyika hasa kwa wale ambao hawakosi kucheza kamari sehemu hiyo. Yupo rafiki yangu mmoja yeye apatapo mshahara wake ni moja kwa moja anaanzia kasino. Hatoki hadi ashinde au aishiwe. Nilisikitika sana siku aliyolala na kuamkia huko huko kwenye kasino na hana hata ndururu mfukoni. Kamari ni hatari, hata maandiko mengi yanalaani aina hii ya michezo.
 
Hili lilikuwa ombi la mzee wa Burundi kwa wamiliki wa vyombo vya hbr..ili kuongeza wigo wa mapato...wao wakalichukua kama lilivyo ss kila kipindi kina dro yake mbaya zaid haijulikan inachezeshwaje na kama kuna msimamizi kutoka bodi ya michz ya kubahatisha. WIZI MTUPU..KWA HILI WAZIRI AJIUZULU.
 
Habarini

Niende straight kwenye ujumbe wangu. Hivi kwann media house miaka hii zimekuwa na uhovyo wa vipindi kiasi kwamba kwa sisi tunaojua maudhui mazuri ya vipindi tunaona kama mambo yapo hovyo sana?!

Vipindi vingi vya sasa ni vipindi ambavyo kama sio vina maudhui ya kuhamasisha upotofu wa maadili, basi vina mijadala ambayo haina uhusiano na ujenzi wa taifa bora la Tanzania na hakuna watu wenye weledi nyuma ya mijadala yenyewe kutokana na mifumo ya kuajiri watu wa hovyo katika media kama mapresenter au mahost wa vipindi husika sababu tu ya jina au umaarufu wa muhusika.

Hivi ni nani ambaye anatakiwa kuratibu haya mambo yakae kwenye usawa au ubora wake?! Tazama vipindi vilivyopo mada zake ni upumbavu kama sio upuuzi mtupu hata kusikiliza radio inakuwa ni kazi mtu unaona uweke tu Memory card yako usikilize muziki wako kwenye playlist.

Nyimbo nzuri hazipigwi tena zinazopigwa ni kwa msukumo wa ushabiki tu na sio DJ anayejua muziki na kusaidia mziki mzuri kushika masikio ya watu.

Mapresenter au mahost ni watu wenye matukio ya ajabu katika jamii na hawana staha wala hofu wala hata ufahamu wa standards za jamii.

Kila siku tunazungumzia swala la kumomonyoka kwa maadili na kuwasakizia lawama wazazi na viongozi wa kiimani ila tunasahau Media house kama eneo lenye influence na sumu kali ya haraka sana yenye madhara ya muda mrefu.

Muziki unaopigwa, topic zinazo zungumzwa, mambo yanayoonyeshwa na kupostiwa, wahusika wanaokuwa katika hizi media wanainfluence kubwa sana katika kushape jamii na tabia za kizazi cha sasa na cha baadae.

Nitawapa mfano, kuna kipindi kinaitwa Leo tena cha clouds, wao mada zao zimekaa kiumbea umbea tu hata wale wahusika waliowekwa kama mahost na watangazaji hebu watazame haiba zao na lugha zao na hata mienendo yao, hivi ndivyo tunataka wanawake zetu wawe vile?!

Mimi nakumbuka zamani, akina Suzanne Mungi, Fauzia tabood, Mannuel Elias, Betty Mkwaswa, Auntie Tumaini, Ahmed kipozi, john Ngahyoma, masood masood, Masood kipanya, na wengineo list ni ndefu sana, walikuwa na media personality za adabu na heshima hata leo tukiwaona unaona kama umeona mzazi aliyekulea utotoni mwako kutokana na maudhui mazuri ya vipindi na utulivu wa media wakati huo.

Ilikuwa ni rahisi kusikiliza redio moja siku nzima sababu ya maandalizi ya vipindi kwa utulivu na mada jengefu na zenye kutoa maudhui ya kuiboresha jamii.

Ila sasa aisee, unakuna na akina Gea, juma lokole, loveness Diva, mwijaku, swebe, kingwendu, sijui nani nani hawa watu ukikaa ukawasikiliza aiseee inakufanya uwazie hizi media house zipo under monitoring na censorship ya mamlaka za serikali ambazo zinatakiwa kutazama media inalisha nini akili za raia?!

Why tunakwenda namna hii?!

Unataka kunambia hakuna watu wenye pure media talents ambao wanaweza itoa hapa hii sekta na kuirejesha kwenye ubora wake halisi?! Naumia sana kuona kama jamii tunakaa kimya tukiyashuhudia haya na hatufanyi lolote.

Stesheni za television muda wote zinapiga muziki. Miziki yenyewe 24/7 ni ya ngono ngono tu hakuna la maana. Hivi unajua masaa 24 ya siku ni silaha kubwa sana ya kinyuklia ya kuharibu taifa kwa kuprogram jamii especially watoto kupitia mambo wanayotazama na kusikia?!

Tunayo power ila tumeamua kuitumia kujiangamiza wenyewe. Power ya media ni kubwa sana aisee. Kuna mengi mazuri na ya kujenga tunaweza yaprogram kwenye media badala ya haya tuliyokazana nayo.

Na ukitaka kujua media zina lengo moja tazama ufananio wa vipindi na maudhui. Halafu tunashangaa kwann watu wanafanya mambo ya hovyo, kwann watoto wanalawitiwa na kunajisiwa, tunashangaa kwann watoto wadogo wanatabia za viburi, kukosa adabu na heshima kwa waliowazidi umri, tunashangaa kwann vijana hawana spirit ya ujenzi wa taifa wanakuwa wa hovyo hovyo, mara kunyoa kiduku mara kuvaa milegezo na Jean's zimechanikachanika kama wametoka kupambana na simba mwenye makucha makali.

Serikali, wanajamii, wanajamii forum, nawasihi tufanye jitihada haya mambo yarejee kuwa sawa. Jamii inaharibiwa sana na vipindi vinavyorushwa kwenye tv na redio kwa sasa.
 
Umesema hoja nzito... Wenye akili tu ndio watakuelewa...

Mimi ningekuwa mwenye mamlaka... Media zilizokosa ubunifu... Mfano zisizo na maudhui zenye kujenga... Wao ni miziki tu masaa 24 nafunga.
 
Gea Habib alishapewa hadi tuzo kwa habari za kijamii na Wizara..Umemuongelea vibaya wrongly..unyanyasaji n.k huwa anazitoa sana hizo habari,so mimi naona hana shida.

Hayo mengine uko sawa.
 
Sikuhz matangazo ya kamari na kubet ndiyo yanatawala kwenye radio stations hadi TBC Taifa wameingia mkenge.Zimebaki radio za dini tu ndizo hazipromote matangazo ya kucheze pesa na kubeti.

Ukiwauliza wanakwambia radio zinaendeshwa kwa matangazo lakini wanasahau kitu kinachoitwa "ethics".Ukiwa Mhariri wa chombo cha habari haijalishi tangazo linalipiwa bilioni ngapi kama linaenda kinyume na maadili+utashi+mila+hulka ya watanzania inatakiwa ulikatae.

Nakumbuka kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwenye siku ya mwisho ya kampeni magazeti ya Tanzania karibia yote yalipambwa kwenye ukurasa wote wa mbele na tangazo la kumnadi mgombea wa CCM lakini magazeti mawili ya Mwananchi na Raia Tanzania yalikataa hilo tangazo japo lilikua na hela nyingi.

Hii ndio tunaiita professionalism
 
Unaingia official page ya clouds Tv au Fm unakuta wamepost meme pale "Ulivoachwa mpenzi wako alikupa sabab Gani"

Au watauliza

"Ni kitu gani ukijiangalia mwilini mwako unasema ma shallah"

Like what the actual f*ck guys??

Me natembelea official page nipate kujua kinaendelea nn uko duniani au watu wanawaza nn nakutana na huo ujinga

Media hazina contents saizi HAKUNA AAA

NB: Hy ni wote clouds,wasaf na ndugu zao wa vigodoro efm na MilardAyo anakalisha wote hao Kwa contents

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamii imeporomoka na inazidi kuporomoka imefikia hatua mtoto wa kiume ni wa kumchunga asiharibikiwe zaidi ya mtoto wa kike... tazama vioo vya jamii sasa yan hopeless!

Cha ajabu thread ya hivi haitembei eti

End of times
 
Wapuuzi sana siku hizi vipindi vimekaa kiumbea umbea, ukahaba na udangaji mixer wanapromote uchawa na watoto wa kiume waliowekwa wote ni machawa kwenye media.
 
Gea Habib alishapewa hadi tuzo kwa habari za kijamii na Wizara..Umemuongelea vibaya wrongly..unyanyasaji n.k huwa anazitoa sana hizo habari,so mimi naona hana shida.

Hayo mengine uko sawa.
Kupewa tuzo sio qualification kuwa mtu ni bora kama inakwenda kinyume na standards za jamii. Kumbuka hata wacheza filamu za ngono hupewa tuzo, je inamaanisha wao nao hawana shida katika jamii?!

Mimi nazungumzia maudhui wanayokuwa wanayajadili katika vipindi vyao muda mwingi. Kupewa tuzo kwasababu ya habari za kijamii mbona kama ni minor issue.
 
Sikuhz matangazo ya kamari na kubet ndiyo yanatawala kwenye radio stations hadi TBC Taifa wameingia mkenge.Zimebaki radio za dini tu ndizo hazipromote matangazo ya kucheze pesa na kubeti.

Ukiwauliza wanakwambia radio zinaendeshwa kwa matangazo lakini wanasahau kitu kinachoitwa "ethics".Ukiwa Mhariri wa chombo cha habari haijalishi tangazo linalipiwa bilioni ngapi kama linaenda kinyume na maadili+utashi+mila+hulka ya watanzania inatakiwa ulikatae.

Nakumbuka kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwenye siku ya mwisho ya kampeni magazeti ya Tanzania karibia yote yalipambwa kwenye ukurasa wote wa mbele na tangazo la kumnadi mgombea wa CCM lakini magazeti mawili ya Mwananchi na Raia Tanzania yalikataa hilo tangazo japo lilikua na hela nyingi.

Hii ndio tunaiita professionalism
Kabisa mkuu. Na shida ya hizi kazi wanapeana sababu ya umaarufu. Mtu kama mwijaku anakuwaje host wa kipindi ukiuliza eti sababu anaongea kama chiriku.

Huu ni upuuzi sana ujue.
 
Habarini

Niende straight kwenye ujumbe wangu. Hivi kwann media house miaka hii zimekuwa na uhovyo wa vipindi kiasi kwamba kwa sisi tunaojua maudhui mazuri ya vipindi tunaona kama mambo yapo hovyo sana?!

Vipindi vingi vya sasa ni vipindi ambavyo kama sio vina maudhui ya kuhamasisha upotofu wa maadili, basi vina mijadala ambayo haina uhusiano na ujenzi wa taifa bora la Tanzania na hakuna watu wenye weledi nyuma ya mijadala yenyewe kutokana na mifumo ya kuajiri watu wa hovyo katika media kama mapresenter au mahost wa vipindi husika sababu tu ya jina au umaarufu wa muhusika.

Hivi ni nani ambaye anatakiwa kuratibu haya mambo yakae kwenye usawa au ubora wake?! Tazama vipindi vilivyopo mada zake ni upumbavu kama sio upuuzi mtupu hata kusikiliza radio inakuwa ni kazi mtu unaona uweke tu Memory card yako usikilize muziki wako kwenye playlist.

Nyimbo nzuri hazipigwi tena zinazopigwa ni kwa msukumo wa ushabiki tu na sio DJ anayejua muziki na kusaidia mziki mzuri kushika masikio ya watu.

Mapresenter au mahost ni watu wenye matukio ya ajabu katika jamii na hawana staha wala hofu wala hata ufahamu wa standards za jamii.

Kila siku tunazungumzia swala la kumomonyoka kwa maadili na kuwasakizia lawama wazazi na viongozi wa kiimani ila tunasahau Media house kama eneo lenye influence na sumu kali ya haraka sana yenye madhara ya muda mrefu.

Muziki unaopigwa, topic zinazo zungumzwa, mambo yanayoonyeshwa na kupostiwa, wahusika wanaokuwa katika hizi media wanainfluence kubwa sana katika kushape jamii na tabia za kizazi cha sasa na cha baadae.

Nitawapa mfano, kuna kipindi kinaitwa Leo tena cha clouds, wao mada zao zimekaa kiumbea umbea tu hata wale wahusika waliowekwa kama mahost na watangazaji hebu watazame haiba zao na lugha zao na hata mienendo yao, hivi ndivyo tunataka wanawake zetu wawe vile?!

Mimi nakumbuka zamani, akina Suzanne Mungi, Fauzia tabood, Mannuel Elias, Betty Mkwaswa, Auntie Tumaini, Ahmed kipozi, john Ngahyoma, masood masood, Masood kipanya, na wengineo list ni ndefu sana, walikuwa na media personality za adabu na heshima hata leo tukiwaona unaona kama umeona mzazi aliyekulea utotoni mwako kutokana na maudhui mazuri ya vipindi na utulivu wa media wakati huo.

Ilikuwa ni rahisi kusikiliza redio moja siku nzima sababu ya maandalizi ya vipindi kwa utulivu na mada jengefu na zenye kutoa maudhui ya kuiboresha jamii.

Ila sasa aisee, unakuna na akina Gea, juma lokole, loveness Diva, mwijaku, swebe, kingwendu, sijui nani nani hawa watu ukikaa ukawasikiliza aiseee inakufanya uwazie hizi media house zipo under monitoring na censorship ya mamlaka za serikali ambazo zinatakiwa kutazama media inalisha nini akili za raia?!

Why tunakwenda namna hii?!

Unataka kunambia hakuna watu wenye pure media talents ambao wanaweza itoa hapa hii sekta na kuirejesha kwenye ubora wake halisi?! Naumia sana kuona kama jamii tunakaa kimya tukiyashuhudia haya na hatufanyi lolote.

Stesheni za television muda wote zinapiga muziki. Miziki yenyewe 24/7 ni ya ngono ngono tu hakuna la maana. Hivi unajua masaa 24 ya siku ni silaha kubwa sana ya kinyuklia ya kuharibu taifa kwa kuprogram jamii especially watoto kupitia mambo wanayotazama na kusikia?!

Tunayo power ila tumeamua kuitumia kujiangamiza wenyewe. Power ya media ni kubwa sana aisee. Kuna mengi mazuri na ya kujenga tunaweza yaprogram kwenye media badala ya haya tuliyokazana nayo.

Na ukitaka kujua media zina lengo moja tazama ufananio wa vipindi na maudhui. Halafu tunashangaa kwann watu wanafanya mambo ya hovyo, kwann watoto wanalawitiwa na kunajisiwa, tunashangaa kwann watoto wadogo wanatabia za viburi, kukosa adabu na heshima kwa waliowazidi umri, tunashangaa kwann vijana hawana spirit ya ujenzi wa taifa wanakuwa wa hovyo hovyo, mara kunyoa kiduku mara kuvaa milegezo na Jean's zimechanikachanika kama wametoka kupambana na simba mwenye makucha makali.

Serikali, wanajamii, wanajamii forum, nawasihi tufanye jitihada haya mambo yarejee kuwa sawa. Jamii inaharibiwa sana na vipindi vinavyorushwa kwenye tv na redio kwa sasa.
Starehe pekee inayoteka akili za watu ni ngono, na ili watu wavune lazina wapitie "...pale ambapo sisi sote wakubwa na wadogo twapapenda... in Mwinyi's voice"
 
Unaingia official page ya clouds Tv au Fm unakuta wamepost meme pale "Ulivoachwa mpenzi wako alikupa sabab Gani"

Au watauliza

"Ni kitu gani ukijiangalia mwilini mwako unasema ma shallah"

Like what the actual f*ck guys??

Me natembelea official page nipate kujua kinaendelea nn uko duniani au watu wanawaza nn nakutana na huo ujinga

Media hazina contents saizi HAKUNA AAA

NB: Hy ni wote clouds,wasaf na ndugu zao wa vigodoro efm na MilardAyo anakalisha wote hao Kwa contents

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni changamoto sana ujue. Yaani unakuta official page ya media house kubwa ila inaendeshwa kama ni page inayosimamiwa na katoto ka sekondari.
 
Jamii imeporomoka na inazidi kuporomoka imefikia hatua mtoto wa kiume ni wa kumchunga asiharibikiwe zaidi ya mtoto wa kike... tazama vioo vya jamii sasa yan hopeless!

Cha ajabu thread ya hivi haitembei eti

End of times
Uzuri watasoma na wataona wasipochangia it means wameshaona ukomo wao wa kufikiria ulipofikia ndugu yangu. Usitegemee watu waliojaza ujinga mwingi kichwani wakiona nyuzi za busara wataongea lolote, hiyo sio platform yao ila wakisoma wanaelewa na kujifunza.
 
Back
Top Bottom