mpasta
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 919
- 2,004
Hivi karibuni kila redio unayosikiliza hasa hizi za FM KITAA ukiitoa TBC basi lazima ukutane na matangazo ya kupigia debe kamari mpaka inakera. Kwenye simu nako kila wakati zinatumwa meseji za kuhamasisha watu wajiunge na ubashiri...
Hivi kama Taifa tumeshajiandaa na madhara yanayokuja na yajayo kutokana na BETTING???

. Tunajua uhalifu kiasi gani utaongezeka, familia ngapi zitavunjika, matatizo mangapi ya afya ya akili inayotokana na msongo wa mawazo yatatokea???N.K...Ndio uatakuta sasa kazini Baba zima na midevu yake ana MIKEKA yake ya KUBET, Vyuo vikuu ndio useme Madenti wana BETT kwa kutumia Bumu hawa si ndio watakuja kuugua "Gambling Disorder" kesho na kesho kutwa wamekuwa MAWAZIRI wetu wa nchi pesa za bajeti ya wizara wanaenda KUBETT kwenye MACASSINO

Asubuhi nilikuwa nasoma PAPER moja ya Utafiti imetoka tarehe 24/01/2022 yenye kichwa cha habari "GAMBLING RELATED SUICIDES IN EAST AFRICAN COMMUNITY", humo nimekuta wenzetu KENYA kujiua kutokana na madhara ya BETTING wanaongoza, wakifuatiwa na UGANDA kisha ndio sisi TZ, tena mbaya zaidi hao waliojiua wengi wao walikuwa wana elimu ya Chuo Kikuu na wameajiriwa.
Chambilecho "Mwenzako akinyolewa wewe tia maji", sheria ya michezo ya kubahatisha inasema wazi

"Mtu yeyote atakaye ruhusu mtoto chini ya miaka 18 kushiriki, kuingia au kukaa karibu na eneo la Mchezo wa Kubahatisha, anahesabika kafanya kosa na anastahili kulipia faini ya shilingi 500,000/- au kifungo kisichopungua miezi mitatu au vyote kwa pamoja”
Nani anafuatilia utekelezaji huo?Mbona huku mitaani tunawaona watoto wa Sekondari chini ya umri wa miaka 18 wapo kwenye Slot mashine za MCHINA??.
Nguvu ya kukusanya kodi ya michezo ya Kubet bora iendane na nguvu za kudhibiti madhara vinginevyo tutakuja kubwa na Taifa la ajabu sana, sasa vijana mtaani BETTING ndio imekuwa chanzo cha mapato hapo ndio Shida inapoanzia....