Mbona Reginald Mengi yupo kimya juu ya utawala wa Magufuli? Anamkubali au hamkubali?

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Feb 18, 2016
1,261
1,222
Reginal-Mengi.jpg

Reginald Mengi ni mfanyabiashara mkubwa sana hapa nchini. ndiye mwenyekiti mtendaji na mmiliki wa makampuni ya IPP yanayomiliki ITV, RADIO ONE, GAZETI LA NIPASHE na mambo mengi hapa nchini. alishawahi kulalamikia watawala wakuu wa nchi kama ifuatavyo?

1. Enzi za MKAPA: alilalamikia sana kukosa hoteli ya KILIMANJARO ambayo alipewa mfanyabiashara kutoka Uarabuni. Mengi alidai kuna rushwa ktk utawala wa enzi hizo na ndiyo maana aliikosa hiyo fursa.

2. Enzi za KIKWETE: alilalamikia kuwa fursa za kibiashara wanapewa wachache wanaojua kutoa rushwa. akawataja akina Manji na wengine kuwa ni MAFISADI PAPA. aliilaumu serikali ya Kikwete kwa kulea rushwa na upendeleo.

Sasa yuko JPM, sijaona maoni ya mzee Mengi. hii inaashiria nini? hamkubali JPM pengine anamwona mbabaishaji au yeye Mengi ndo msanii au anampa muda ndo atoe yake ya moyoni?
 
Bado anavuta pumzi kwanza. Mbona ni mapema mno hasa kulalamikia maslahi binafsi. Isitoshe kanyimwa nini hadi alalamike?
 
Bado anavuta pumzi kwanza. Mbona ni mapema mno hasa kulalamikia maslahi binafsi. Isitoshe kanyimwa nini hadi alalamike?
walau hata kumsifia? huna ana hisia za kusema wazi ndiyo maana nashangaa juu ya ukimya wake
 
Reginald Mengi ni mfanyabiashara mkubwa sana hapa nchini. ndiye mwenyekiti mtendaji na mmiliki wa makampuni ya IPP yanayomiliki ITV, RADIO ONE, GAZETI LA NIPASHE na mambo mengi hapa nchini. alishawahi kulalamikia watawala wakuu wa nchi kama ifuatavyo?

1. Enzi za MKAPA: alilalamikia sana kukosa hoteli ya KILIMANJARO ambayo alipewa mfanyabiashara kutoka Uarabuni. Mengi alidai kuna rushwa ktk utawala wa enzi hizo na ndiyo maana aliikosa hiyo fursa.

2. Enzi za KIKWETE: alilalamikia kuwa fursa za kibiashara wanapewa wachache wanaojua kutoa rushwa. akawataja akina Manji na wengine kuwa ni MAFISADI PAPA. aliilaumu serikali ya Kikwete kwa kulea rushwa na upendeleo.

Sasa yuko JPM, sijaona maoni ya mzee Mengi. hii inashiria nini? hamkubali JPM pengine anamwona mbabaishaji AU yeye Mengi ndo msanii AU anampa muda ndo atoe yake ya moyoni?
Kwani yeye ni nani mpaka aseme hayo?
 
Hizi zinaitwa chokochoko, Magufuli ndio kwanza ana miezi sita hata bajeti yake haijaanza kutumika anatumia ya Kikwete halafu mnataka watu waanze kusema mnayosema nyie. Muacheni mzee mengi aendelee na biashara zake wakati ukifika atasema
 
Mengi hana tofauti na wewe kama mwananchi wa Tanzania tofauti labda kumiliki kwake vyombo vya habari ambavyo anajua kuvitumia kumtangaza binafsi, si lazima anachokiona Mengi kwenye utawala kiwe ama kisiwe sahihi kwako au kwetu
Kwa kifupi sioni umuhimu wa hoja yako
 
Back
Top Bottom