kisanganyakiswata
JF-Expert Member
- Jan 28, 2014
- 1,294
- 543
Uislam mzuri sana umejali mnoo haki za wanawakeHuko ndio kwenyewe kwa kumkandamiza, mpaka katika jina, hana haki ya kuitwa ubini wa wake, anaitwa kwa ubini wa mume wake.
(1) Kama alikuwa anaitwa Marry Joseph Kigu, na Mumewe anaitwa Clement Mapunda, akiolewa tu anakuwa ni Marry Clement Mapunda.
Utambulisho wake wote, unapotea. Lakini katika uislamu anabaki na ubini ule ule wa baba yake, akiitwa Asha Haji Mtopea, atabakia hivyo hivyo, Asha Haji Mtopea.
(2) Katika uislamu, mali anayomiliki mwanamke ni yake mwenyewe, ikiwa jina la nyumba atakayoijenga, au amenunua nyumba, shamba itabaki jina lake la Asha Haji Mtopea, hakuna jina la mume, Wala jina la ukoo wa mume, unaoingia Katika hati ya nyumba, kadi ya gari, cheti chake Cha elimu ya juu, kama ataongeza elimu, kwenye cheti chake Cha ndoa, kwenye passport, na utambulisho mwingine wowote ule.
(3) Katika uislamu, mwanamke hata awe na kazi, awe tajiri, awe na uwezo wa kiuchumi, hawajibiki kutunza familia, anayewajibika ni mwanamme. Mwanamme anawajibika, makazi, chakula, kusomesha watoto, kulipia matibabu nk.
(4) Katika uislamu,mtoto amepewa amri ya kumuheshimu, Mama yake, mara tatu zaidi ya baba yake. Na mtoto, pepo yake iko chini ya unyao wa mama ake.
(5) Katika uislamu, mtoto akizaliwa nje ya ndoa, kwa baba upande wa baba hauna haki(sio halali), lakini kwa mama ni halali, mtoto akiwa mkubwa, na akiacha mali, Mama ndio anarithi, baba hapati kitu, kwa mtoto wa nje ya ndoa .Nk