hannibali
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 468
- 427
Habari za muda huu wanaJF na poleni na majukumu ya kutafuta tonge. Niende moja kwa moja kwenye mada husika.
Hivi kwanini Mwarabu amemdharau sana mwanamke? Imenifanya nifikirie kwa undani zaidi baada ya jana kuona footage ikimuonesha Mwarabu akimtoa mwanamke kwenye mgahawa ambao eti inasemekana ni sehemu ya jamii ya kiume. Sasa the way alivyokuwa anamtoa utafikiri kama si kiumbe cha kawaida, ilinipasa kujiuliza mara mbili mbili.
Ivi wanawake si mama zetu kabisa na wamechangia kwa namna moja ama nyingine katika malezi yetu. Sasa kwanini anatengwa kama mtu kutoka sayari nyingine? Hii kitu ipo katika jamii nyingi za Kiarabu na sio hicho tu kuna vitu vingi ambavyo mwanamke anakatazwa kufanya kama vile:
• Haruhusiwi kuendesha magari
• Haruhusiwi kufanya kazi za jeshi na intelijensia
• Wanawake hawawezi kufungua akaunti benki bila ruhusa maalumu kutoka kwa mwanaume.
• Wanawake wanalazimika kuwa na ridhaa ya kiongozi wa kiume mfano katika familia ili kupata pasi ya kusafiria au kuondoka nchini.
• Kwenye maeneo mengine ya maisha mfano masomo, kazi na hata kwenye kupata baadhi ya huduma za kiafya mwanamke hapati kipaumbele sawa na mwanaume
Tatizo ni nini hasa mpaka kukawa na tabaka kubwa namna hii kati ya mwanamke na mwanaume? Ni mfumo au kitu gani? Mwanamke ana nini ambacho ni cha ajabu kiasi hicho? Au wanaona kama ni kiumbe hakistahili kuwepo?
Wanazengo wanaoelewa zaidi leo tuje kuwekana sawa hapa.