Mbona Muhongo Hakuitwa Mezani Kuomba Msamaha mbele ya Mungu na Watanzania Wote Halafu Aanze Upya?

Mgibeon

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
11,254
21,276
Inasikitisha Sana, mtu ambaye umemtuhumu kua Ni mwizi eti Leo unamwambia Njoo Nyumbani, Uombe Msamaha na urudishe ulichoiba halafu tuanze upya! Inapatana na Akili Kweli?

Hawa wameshababisha sio hasara ya pesa Tu, wamesababisha hasara kubwa ambayo haiwezi kulipwa na pesa. Ikitokea mtu akakwapua simu yako pale Ubungo kwenye foleni Halafu watu wakamkimbiza na kumpata Hua wanamwambia "Haya twende ukaombe Msamaha na umrudishie mwenyewe simu yake?

Ukiwaza Sana kiundani unaweza kuona Ni jinsi gani tunachezewa Akili, Ajabu Ni kwamba hawa hawa CCM ndio wametufikisha hapa, halafu hawa hawa wanajifanya kushangaa Sana (Refer to Mshangao wa Job Ndugai Jana). Mimi nadhani haya yote yanafanyika kujitaftia jina Tu kwa Watanzania wenye uelewa mdogo.

Eti Acacia Haijasajiliwa! Kodi na document zote za kuingiza vifaa na mitambo, document zote za kutoa dhahabu na malighafi zake zilikua zinapitaje pitaje kama hapakua na usajili na hapo bado hatujazungumzia mikataba yenyewe ingawa ni ya wizi ila Walipokua wanasaini hawakujua wanaingia mkataba na nani? Kuna maswali mengi Sana ya kujiuliza ambayo mwisho wake sio mzuri Sana kwa afya ya CCM.

Huyu huyu tunayemuita Mwizi bado anaendelea na uchimbaji.. Huyu huyu tunayemuita Mwizi tumempa nafasi ya Kuja kuomba msamaha na kuanza upya, mbona haikua hivyo kwa Prof, Muhongo? Ni kipimo gani kinatumika kumsamehe Acacia na kipimo kipi kinatumika kutokumsamehe Prof Muhongo?

Hatuwatetei wezi, Ila hatuoni Nia thabiti ya kupambana na kuthibiti wizi huu.. Haya mnataka kulipwa fidia ya mchanga wa hizo container elfu 44 na kitu, vipi mmeshapiga hesabu zimeshasafirishwa contena ngapi za pure gold na zenyewe tulipwe?

"Acheni Unafiki"- H.Bashe, Mb.Nzega.
 
Back
Top Bottom