mbona mlimani Tv inawezekana akina dada wetu kuvaa hijab? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mbona mlimani Tv inawezekana akina dada wetu kuvaa hijab?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by muhogomchungu, Jan 26, 2011.

 1. muhogomchungu

  muhogomchungu JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mlimani TV inayomilikiwa na wasomi utakuona akina dada wetu ambao ni watangazaji wakiruhusiwa kuvaa hijab na huku wakiwa Live wanatangaza. hii nimeona ktk taarifa ya habari au hata katika habari nyengine
  lkn baadhi ya tv hawaruhusiwi. na hii kutoruhsu uvaaji wa vazi la lazima kwa akina dada wetu wa kiiislam kunaifanya baadhi ya akdada wenye imani ya kweli na dini yao wanashindwa kujiunga na tv hizo huku wakiwa na sifa zao za utangazaji . kwa mfano niliwahi kusoma ktk moja ya gazeti kwamba Sakina dotto alikata kujiunga na Itv baada ya kukuataliwa kuvaa hijab akiwa Online.na wapo wengi tu ambao kwao hijab ni lazima lakina wanasifa zote za kutangaza.
  Huku tukiwa tunapigania haki za wanawake Tanzania, yaani wawe huru bila ya kuvunja sheria, vyombo vya habri vikiwa mbele kutetea uhuru wa wanawake,yaani uhuru wa wanawake na kutowanyanyaswa .
  Mbona mlimani tv inawezekana na huku Itv, star tv,Tbc haiwezekani? au mlimani tv ni ya waislam?
   
 2. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Sioni udhia katika kutumia vazi la hijaab, kwani ni vazi lenye kutunza utu wa mwanamke.
   
 3. Madikizela

  Madikizela JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2009
  Messages: 320
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  PELEKA HII HOJA MAHAKMA YA KADHI!!!:car:
   
 4. M

  Mkare JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh! Inahusu... Kwani ni lazima kujibu jamani? Kama mtu amepost hoja yake unaona huwezi kuchangia si utambae tu kimya kimya wangu...! Haipendezi bana, tukue
   
 5. semango

  semango JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  katoa wazo lake tena lawezekana ni la kiutu uzima kabisa
   
 6. d

  dorisvety Member

  #6
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  inawezekana kwa akina dada kuvaa hijab na kuonekana kwenye tv wakitangaza, wasiwasi wangu ni huu uvaaji wa juba, je nao itakuwaje? nao waruhusiwe?
   
 7. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  niwajuavyo hawa watataka mpaka kuvaa kininja watangazapo
   
 8. haibreus

  haibreus JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 296
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Penye ukweli daima watu hutia jazba!wapeni watu uhuru wao!!hakuna wapumbavu siku hizi!
   
 9. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Nadhani jibu la swali lako unalo.

   
 10. K

  Kivia JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  K├╣vaa hijabu hakupunguzi chochote kwa mwanamke. Ni bora TV ZOTE WAIGE MFANO HUO[mwanamke ni stara]
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  :behindsofa:
   
 12. P

  Pokola JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Chagua moja, udini au kazi!! Huku ulaya hayo madude wanavua, wanakaguliwa ikibidi. Unaleta udini hapa?
   
 13. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #13
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Msilazimishe mambo wewe nenda panapokufaa!!! Kama Sakina aliktaa tena kimya kimya hiyo ndio busara :suspicious:!!
   
 14. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #14
  Jan 26, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  mkuu, mbona wapo wengi tu!
   
 15. K

  Kivia JF-Expert Member

  #15
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Vazila hijabu linapendeza, wadau wa jf acheni ushabiki. Hili ni vazi kongwe toka enzi za mitume. Ndo maana hata masister wa kikatoliki huvaa vazi hilo safi na kuwaacha waamini wao wakivaa vimini, vijisuruali na vitop ambazo ni mila za kizungu. VAZI LA Hijabu linapendeza saana kinadada/mama livaeni mpendeze
   
 16. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #16
  Jan 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nani alikuambia ukivaa hijab ndo umetunza utu? huo ni utamaduni wa mashariki ya kati!
   
 17. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #17
  Jan 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Nani alikuambia linapendeza, hebu fikiria na joto lote la Dar mtu uko tu umejitwika manguo kibao, Yaani ni majasho kwa kwenda mbele, Hebu na nyie wanaume mjaribu kuvaa hizo hijabu muone wanawake wanavyopata shida! Asikuambie mtu hijab kwa dar ni mateso makubwa, Labda kwa watu wanaoishi ulaya mf, Urusi, wakati wa winter hata mie naweza kuvaa na kujifunika mwili mzima nikabakisha macho tu.
   
 18. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #18
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Kila kazi ina masharti yake, ukiikubali kazi maana yake unayakubali masharti yake.
  Unamtumikia kafiri ili upate mradi wako.
  ndiyo maana kuna waislamu kibao wanafanya kazi Tanzania Breweries na Konyagi japo pombe kwao ni haramu.
   
 19. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #19
  Jan 26, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nao waruhusiwe tu, manake watu wanasema mwanamke stara, wakati stara ni mtazamo tu wa mtu. Nani alikuambia ukivaa nguo yako vizuri bila shungi hauwi na stara? Achane kukandamiza wanawake eti kisingizio wanapendeza, mbona nyie wanaume hamvai?
   
 20. muhogomchungu

  muhogomchungu JF-Expert Member

  #20
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hawa wanawake wakiristo waliokoka wanaovaa hijab vipi? Mashariki ya kati?
   
Loading...