Mbona matajiri hawavai vizuri, hawapendi kula bata na wakati hela wanazo?

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,622
2,835
Habari wana Jamii Forums.

Katika Jamii tumetofautiana vipato wapo wenye vipato vikubwa,vidogo na vya kati.

Hawa wenye vipato vikubwa huwa ndo tunawaita "Matajiri". Lakini kinachonishangaza kwa Watu Hawa ni kwamba nashindwa kuelewa Hela zao wanazitumiaje kwasababu hawavai nguo nzuri na Hawapendi kabisa kula bata. Licha ya kuwa hela wanazo wanashindwaje kula bata na kuparty.

For instance tuchukulie mfano Bill Gates anasema huwa anatumia muda wake mwingi kusoma vitabu! Shida yote ya nini wakati Hela unazo si ukule bata mpaka bata zikome.

Mwingine ni Mark Zuckerburg the Facebook Owner huyu yeye vinguo anavyovaa Kama vya Kariakoo mtumbani.Hela unazo why don't you dress.

Hiyo nafasi akipata mwingine ataitumia ipasavyo.

Kingine eti wanapenda vitu vya bei ndogo Sana. Nilishangaa kumuona Tajiri mmoja amekwenda kununua nguo alipofika dukani akauliza "mashati shilingi ngapi"muuza duka akamjibu yapo ya 20000,30000 na 40000 Ila eti yule Tajiri akachagua la 20000 tena akaomba muuza duka ampunguzie bei hadi akalinunua kwa 15000.

Hii imekaaje Inakuaje hawavai sana mabling na kula bata hawali.
 
Inategemea NTU na NTU. Kuna matajiri wengi tu wanatupia vidudu vya nguvu tu. Yuko yule Bezos wa Amazon ambaye kamzidi Bill Gates na mkewe wanatupia vidudu vya haja tu. Sasa hivi wameachana baada ya kuanikwa hadharani kuhusu mchepuko wake.

Wapo mabilionea wengi wengi tu wanaovaa vizuri sana kama Oprah, Michael Jordan etc.
 
Back
Top Bottom