Mbona Manji hapati watetezi?

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Manji kama ilivyo kwa Mbowe na Sumaye ni mwanasiasa,ni diwani wa kata ya Mbagala kupitia CCM. Ameingia matatani na PSPF kuhusiana na mkataba wa pango ambapo mahakama kuu imemkuta na hatia ya kukaa bila kulipa pango kama ilivyo kwa Mbowe. Mbunge wa Mbarali pia alikutwa na ardhi kubwa ambapo zaidi ya ekari 1800 ilipokwa na kurudishwa kwa wananchi,sasa Sumaye ekari 33 mjini, manispaa ya kinondoni,jiji la Dar Es Salaam bila kuliendeleza imekuwa nongwa. Je ndani ya jiji ekari 33 kuziacha pori wakati watu hawana makazi ni sawa?

Mbona wengine walivyopokwa tumeshangilia? Ila Mbowe na Sumaye imekuwa nongwa?
 
Ingawa fisadi ni fisadi kokote aliko iwe ccm au chadema ......

Lakini watanzania kuna mambo tunakuwa tunalialia sana Tanzania ina eneo la 75% ambalo halijawai kutumika......

Yaani unakuja dar unataka upate hapo hapo shamba,Kiwanja,ujenge Nyumba nzuri uishi maisha mazuri wakati ukute umekuja Dar kama mtu Wa Milioni 3 hivi na wengine umewakuta.....

Unasahau familia ya baba Wa taifa wana nyumba moja tu Dar wakati wamekuna dar miaka zaidi ya 60 iliyopita na kwanini ukoo wao mkubwa bado wanaishi butiama?.....
 
Kwani wanaomtetea ni nani? si ukawa....kwao kila anayenasibiana nao basi anageuka Mtakatifu...Manji wanaona anastahili.
 
Hivi ekari 33 ni shamba nalo la kusema ni ufisadi?........

Babu yangu anazo ekari 200 lakini mje mjaribu kumgusa ndio tutaeshimiana ......

Yaani mtu amemiliki shamba toka nchi haijapata Uhuru alafu vijana mliozaliwa juzi mnakuja kuleta siasa kwenye mambo kama haya......

Kwa taarifa yako kama una shamba wewe ni fala tu eneo ambalo alitumiki Tanzania ni kama 75% alafu unalia lia na ekari 33.......
Dogo,Dar ni Jiji...hakuna mashamba...tangia mwaka 1999 vijiji vilifutwa Dar...yeye alitakiwa akate viwanja kwa ubia na halmashauri...kiburi kilimuingia,huko kwenu simanjiro wewe miliki hata ekari 1000, bei yenyewe kwa heka sh.50,000/= endeleeni kufuga ngedere tu. By the way, Mke wa Sumaye mwaka jana, March wakiwa bado CCM walipokonywa mamia ya ekari huko Kibaha. endelea kupuliza moto.
 
Mkuu mwaka jana mke wa huyu sumaye alipokwa mamia ya ekari huko Kibaha,walishangili kisa alikuwa CCM sasa kahamia Chadema eti anaonewa.
 
Wameshajivika uwezo wa kusamehe na kuhukumu, sasa sijui wao ni nani.
 
Hivi ekari 33 ni shamba nalo la kusema ni ufisadi?........

Babu yangu anazo ekari 200 lakini mje mjaribu kumgusa ndio tutaeshimiana ......

Yaani mtu amemiliki shamba toka nchi haijapata Uhuru alafu vijana mliozaliwa juzi mnakuja kuleta siasa kwenye mambo kama haya......

Kwa taarifa yako kama una shamba wewe ni fala tu eneo ambalo alitumiki Tanzania ni kama 75% alafu unalia lia na ekari 33.......
Tutalitwaa tu hilo shamba la baba yako na ukileta fyoko fyoko utakiona hatujaribiwi
 
Wameshajivika uwezo wa kusamehe na kuhukumu, sasa sijui wao ni nani.
Asante sana fyatu. Kwao mwanasiasa anaweza kutukanwa matusi mazito sana akiwa bado yupo CCM lakini akihamia kwao tayari ni malaika mpya kundini. Ni watu wa kuwasamehe tu.
 
Ha ha ha...wanajiita 'makamanda'...ila kwa sasa wengi wamegeuka wapiga ramli.
 
Hivi ekari 33 ni shamba nalo la kusema ni ufisadi?........

Babu yangu anazo ekari 200 lakini mje mjaribu kumgusa ndio tutaeshimiana ......

Yaani mtu amemiliki shamba toka nchi haijapata Uhuru alafu vijana mliozaliwa juzi mnakuja kuleta siasa kwenye mambo kama haya......

Kwa taarifa yako kama una shamba wewe ni fala tu eneo ambalo alitumiki Tanzania ni kama 75% alafu unalia lia na ekari 33.......
Kama babu yako anazo 200 basi toa 33 mmpatie MTU wenu
 
Hahaha hatari kweli kweli, wao wanasubiri jambo lifanyike halafu mbio mbio wanaleta mada humu za kupinga, lengo lao haswa ni kujifariji.
Hata kipindi Msajili kamrudisha Lipumba CUF,wenyewe walikimbilia kwenye media kutoa ramli zao ili kujenga dhana ya kuonewa.
 
Hata sisi tunashamgaa kwann alipokuwa ccm na kupigiwa kelele sana na cdm hakunyang'anywa lkn amehamia cdm tu amenyang'anywa?
 
Dogo,Dar ni Jiji...hakuna mashamba...tangia mwaka 1999 vijiji vilifutwa Dar...yeye alitakiwa akate viwanja kwa ubia na halmashauri...kiburi kilimuingia,huko kwenu simanjiro wewe miliki hata ekari 1000, bei yenyewe kwa heka sh.50,000/= endeleeni kufuga ngedere tu. By the way, Mke wa Sumaye mwaka jana, March wakiwa bado CCM walipokonywa mamia ya ekari huko Kibaha. endelea kupuliza moto.
jiji pekee lenye shamba katikati ya mji ni arusha, kama anataka kulima mjini akatafute shamba arusha.
 
Hata sisi tunashamgaa kwann alipokuwa ccm na kupigiwa kelele sana na cdm hakunyang'anywa lkn amehamia cdm tu amenyang'anywa?
hata manji mwana ccm anarudisha nyumba ya pspf, hakuna double standard
 
Back
Top Bottom