Mbona malenga wetu wako kimya na hii hali ya siasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbona malenga wetu wako kimya na hii hali ya siasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Aug 11, 2011.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Kila mtu yuko kimya na hiki ndicho kipindi cha kupata maneno na maoni ya malenga wetu juu ya hali ya kisiasa tnzania.

  Itakuwa si vibaya kila tukapata walau beto moja inayo reflect hali halisi tulikotoka, tulipo na kuendako

  amazingly we might learn something. Maana tushachoka na who knows this might be our refuge.


  Kuna shairi moja sijui liliandikwa na nani (nadhani dudumizi) laitwa Mkopaji na mkopwaji...hii ina beti inayosema:

  MKOPAJI (serikali ya Tanzania)....imeenda kukopa pesa kwa wahisani....


  Hodi bwana nimekuja, nina shida na tatizi
  Nijilie kutaka haja, arobaini ghawazi
  Tazileta kwa pamoja, siku mbili hizi hizi
  Tafadhali nikopeshe, haondoe haja yangu
   
 2. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hilo shairi sidhani kama liliandikwa na dudu baya lakini nitafurahi kusoma majibu toka kwa wahisani (MKOPWAJI)
   
 3. E

  Engineermsuya Member

  #3
  Aug 12, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mhhh

  makubwa haya wajameni
   
 4. E

  Eddie JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwenye Mali: Nimekwisha kusikia, tuliza yako nafusi
  Haja Nitakutimizia, InshaAllah kitu hukosi
  Shida yako si rupia?, nitakupa kwa furusi!
  Njoo Jumamosi nami nashauri moyo.
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Jamani muangalie vina kwani hiyo nayo ni fani sio kukurupukia.

  Hongereni mmejaribu lakini
   
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  Lakini majibu hayo toka kwa wahisani yaonekana kuwa serikali yetu huwa hawapewi pesa moja kwa moja mpaka viji terms & conditions viwe met...anyway MKOPAJI karudi jumamosi kama ulivyoahidi na anasema:

  Hodi bwana nawasili,kwa ile yetu miadi
  unihesabie mali, arobaini nakidi
  Muamshe Jalali, usifanye itikadi
  Tafadhali nikopeshe, haondoe haja yangu
   
 7. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  apparently bwana mkubwa juzi kauliza hii habari ya mkopaji na mkopwaji inaendelea vipi

  watu wamempelekea copy

  makes you miss Mudhihir na Kitwana Kondo bungeni enzi zao
   
 8. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,689
  Trophy Points: 280
  Majibu mazuri ila hilo neno Inshallah halikuwa na umuhimu kuwepo hapo
   
 9. E

  Eddie JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Moyo wangu siamini, kukuhesabia mali,
  Shuruti leta mdhamini, alie msema kweli,
  Shilingi arobaini, kulipa huna dalili,
  Njoo Jumapili nami nashauri moyo.
   
 10. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  Ukiskia uhuni ndo huu

  Mwanzo umesema nije jumamosi leo wanrusha mara ohh lete mdhamini mara off sijui nini...sasa na mimi nasema:

  Shahidi wangu ni Juma, ni huyu nimemleta
  Muaminishe Karima, thawabu utajazipata
  Zihesabu ndarahima, kwangu hakuna matata
  Tafadhi nikopeshe , haondoe haja yangu
   
 11. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,059
  Likes Received: 6,506
  Trophy Points: 280
  asanteni sana mahenga wetu.
   
 12. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  sasa mbona huyo mkopwaji hanipi jibu langu maana kataka referee nimempa kila kukicha naambiwa njoo juma mosi....ndio maana serikali huamua kukopa kwa wa China
   
 13. Eric Cartman

  Eric Cartman JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,816
  Likes Received: 1,353
  Trophy Points: 280
  bado tu somo ujalipata kaka ndio maana wenzako wakasema 'dezo karaha' labda uanze kuishi within your means sasa.
   
 14. E

  Eddie JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna uhuni wala nini kuna kitu kinaitwa due diligence, lazima kifanyike ili kutoa "furusi" sio kukurupuka tu......


  Najua Juma Swahibu, bali sizitoi katu!,
  Tafuta waarabu, wawili au watatu,
  Nakhofu kunighiribu, kutoa tu peke yetu,
  Njoo Jumapili, nami nashauri moyo.
   
 15. E

  Eddie JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Hakuna uhuni wala nini kuna kitu kinaitwa due diligence, lazima kifanyike ili kutoa "furusi" sio kukurupuka tu......


  Najua Juma Swahibu, bali sizitoi katu!,
  Tafuta waarabu, wawili au watatu,
  Nakhofu kunighiribu, kutoa tu peke yetu,
  Njoo Jumapili, nami nashauri moyo.
   
 16. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #16
  Aug 16, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Nimekupata lakini siku ya kwanza uliniuliza na ukasema mwenye kuwa shinda yangu ushaifaham kuwa ni rupia na mimi nakakujibu swadakta na baadae ukasea utanjaalia fulusi na kuniahidi nije Jumamosi huku wewe washauri moyo...nikakuachia wiki nzima na jumamosi nikaja ukata taka haya mambo yenu ya due diligence na ukamtaka na shahidi nimemeleta bwana Juma sasa leo unamtakaa wataka WAARABU sasa kama si kunyanyasana nin nini huku? unataka nimlete Kepteni Maliki au Sahib Ugundo?

  Lakini usitie shaka na nasema hivi:

  Waarabu uliowataka, Hawa nimekuletea
  Nihesabie haraka, hizo ishirini rupia
  Mwenzio ninateseka, kwenda na kurejea
  Tafadhali nikopeshe, haondoe haja yangu
   
 17. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #17
  Aug 16, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kweli mmetuburudisha maana vina na viarifa vimekaa sawa hongereni sana
   
 18. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  namsubri kesho sijui ataniyeyusha na lipi jipya
   
 19. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Dolari sio tatizo, kwangu zimejaa tele
  Takupa uende nazo, kaondoe yako ndwele
  Ukienda cheza nazo, malipo ya pale pale
  Mkataba taandika, wenye kauli ya mwisho
   
 20. E

  Eddie JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waarabu hawafai, lete hati niione,
  Nitakapo kudai, usilete mengine,
  Nakuona ulaghai, hatima tusigombane
  Njoo Jumatatu, nami nashauri moyo
   
Loading...