Mbona malalamiko ya waislamu hawaitaji CCM kama chanzo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbona malalamiko ya waislamu hawaitaji CCM kama chanzo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Vumbi, Jan 23, 2011.

 1. V

  Vumbi Senior Member

  #1
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nimesoma hoja nyingi amabazo zinadai waislamu tumekandamizwa tangu Tanganyika ipate uhuru. Lakini katika malalamiko hayo sijaona mahali tunailalamikia CCM kwa kutukandamiza kwa zaidi ya miaka 50 bali tunamtuhumu nyerere na wakatoliki. Nyerere amekuwa kiongozi kati ya 1961 na 1984 wastani wa miaka 24 na baada ya 1984 mpaka leo 2011 wamekuwa madarakani viongozi wengine wa CCM takribani maiaka 26 sasa, kama Nyerere alitukandamiza je hawa wengine waliopo kwa miaka 26 wametufanyia nini?. Ndugu zangu waislamu kiini cha matatizo yetu ni CCM kwa ujumla wake bila kujali kiongozi mmoja mmoja na wala sio wakatoliki ambao ni sehemu tu ya raia . Tangu tupate uhuru maeneo ambayo waislamu tupo wengi tumekuwa na wabunge waislamu kupitia CCM je wametufanyia nini? Tangu tupate uhuru tumekuwa na mawaziri waisla japo wachache je wamefanya nini katika majimbo yao?. Ndugu zangu waislamu CCM inatudanganya itatusaidai kutatuma matatizo tuliyonayo ya kiuchumi na kielimu wakati ukiangalia taifa lianagamia kwa umaskini hatuna viwanda, wawekezaji wezi, shule mbovu za kata hata waalimu hazina, hospitali shida, maji shida, ufumuko wa bei n.k je haya matatizo tuliyonayo CCM watayatatua kwa njia ipi wakati tuona wazi inchi inateketea. Kama waislamu tunataka mafanikio lazima tupambane na CCM ambayo ndio kiini cha matatizo na kuwaweka madarakani watu wanyeuwezo wa kutujengea uchumi imara wa taifa letu ambao unaweza kutatua matatizo yanayotukabili sisi waislamu pamoja na watanzania wengine kwa ujumla wao.
  Wenu: Muislamu mwenye uchungu wa maendeleo.
   
 2. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kwa sababu asilimia kubwa ya viongozi wa ccm wa kitaifa, kimkoa na kiwilaya ni waislamu.
   
 3. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #3
  Jan 23, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  Ndugu wana JF, si kawaida yangu kuandika au kujibu thread zenye chembe za udini. Kwa mahali tulipofika inatia wasi wasi kama kweli tunaenzi utamaduni wetu wa kuishi pamoja bila kujali imani,kabila au tulipotoka. Utamaduni huu ulitujengea sana heshima kama binadmu tunaojitambua, kujiheshimu na wenye utu.
  Tunapoongelea mambo mazito kama haya hatupaswi kuongozwa na hisia au tetesi bali ukweli(facts). Facts ni pamoja na kumbukumbu zilizothibitishwa au takwimu(statistic) au data. Bwana Gosbertgooluck kwa vile inaonekana una vigezo hivyo nilivyoainisha, tunakuomba uweke hapa jamvini ili vitusaidie sote katika mjadala. Endapo unaongea kwa hisia basi tunakutaka uombe radhi kwa kupotosha maana halisi ya mijadala. Kwa kuzingatia hili, tuwekee takwimu za viongozi kitaifa, kimkoa au kiwilaya ili tufaidike na maelezo yako.
  Kiongozi Mao tse tung aliwahi kusema, No data no right to speech (kama nimenukuu sahihi).
  Wana JF imefika wakati wale wote wenye mapenzi mema na nchi yetu, tudharau maandishi yanayopelekea kutugawa. Tuna mambo mengi muhimu yanayotuhusu kama wanadamu na watanzania kuliko machache yanayotutofautisha. Umasikini unaotukabili hauchagui dini wala kabila. Wizi tunaofanyiwa na kupandishiwa bei za bidhaa kama umeme hauchagui dini wala kabila. Vitanda tunavyolalia hospitali havichagui dini wala kabila. Shule wanazosoma watoto wetu hazichagui dini wala kabila. Vipi vitu vidogo visivyo na maana vituondoe katika agenda kubwa zinazogusa maisha yetu?
  Je, wanamgambo wa kilebanoni waliopigana kwa miaka 30 kwa udini wamefaidika na nini? Je mapigano ya Nigeria kila uchao yanamsaidia Mnigeria masikini licha ya utajiri wa asili walio nao? Je kule Ireland waprotestant na wakatoliki wamenufaiki vipi na mapigano? Je kule Somalia wanakoishi miaka 19 bila serikali wamenufaika vipi na mapigano ya koo licha ya kuwa wana dini moja?
  Je Bosnia Herzegovina wamevuna nini kwa mtutu wa bunduki.
  Kama kuna vita mbaya duniani, basi ni ya imani.
  Samahanini kwa urefu wa hoja,kama raia mwema ninaona tuendako siko!
  Nawasilisha.
   
 4. Ncha ya Upanga

  Ncha ya Upanga Member

  #4
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vumbi, nadhani unahitaji kumsoma Dkt. John C. Sivalon, katika kitabu chake alichokiita "KANISA KATOLIKI NA SIASA YA TANZANIA BARA -1953 HADI 1985", kitajibu maswali yako mengi tu.
   
 5. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,041
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  CUF......ndo chama mbadala wa hoja yako.......
   
 6. m

  mzambia JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  upupup mtupuuuu
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  There's one and only one reason.....................


  BAKWATA ni tawi la CCM
   
 8. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maelezo ya nguruvi3 yanajitosheleza,wale vibaragashia wanaopotosha kwa maslahi ya ccm kama hawajaelewa labda wanaishi tanzania nisiyoijua
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Unazungumzia 'chanzo' au 'ugomvi na'? Waisilamu wana ugomvi na CCM na serikali yake -- kwa kuuendeleza 'mfumo-Kristo' uliopo bila kujali masilahi ya Waisilamu.
   
 10. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,498
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 180
  natamani kukugongea thanks sema nipo kwenye mobile.
   
 11. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,356
  Trophy Points: 280

  wakati wa mkapa waislm walikuwa wanaisea vibaya ccm kila siku for obvious reason...mkapa ni mkiristo!! sasa hivi rais ni muislam mwenzao hawaisemi,wanaitetea,wanaisemea kila inapokosolewa,.these sheikhs are not only uneducated they r devilish too in their matamko...
   
 12. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Data zipo nyingi mno. Ngoja nikusanye ambazo ni more relevant. Wakati nakusanya endelea kutafakari thread ya 'Nyabhingi'. Inaweza ikakupasha moto kidogo.
   
 13. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mkuu unauliza mk....u wakati mkia unauona?
   
 14. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,088
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  watanganyika tuwe makini sana, tukiendekeza udini tutagawanyika then hakutakua na umoja tena.hao wachochezi wanafanya hivyo kwa maslahi yao binafsi.
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Huo ndiyo ukweli!
   
 16. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Haswaaa!
   
 17. akajasembamba

  akajasembamba Senior Member

  #17
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kabisa ni maajabu wakati wa Mkapa hawa waarabu weusi walikuwa ni CUF ngangari kaja JK wamegeuka ni CCM akiondoka JK na akaja Mkristo watarudi CUF! angalia umaarufu wa CUF ulivyopungua sasa TZ bara,
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Huu mwendo wanaouanzisha huu ni wa meli inayokwenda kuzama. Ngoja tusubiri tuone hatima yake
   
 19. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #19
  Jan 23, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Duh si mchezo
   
 20. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #20
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Asante kwa mchango wako mkuu tumekusoma, kuna thread humu ililetwa na Topical inasema Tamko la waislamu full text umeiona? Isome na uitafakari ndio ujue hawa Waislamu na CCm ndio wanaochochea huu udini. Mimi mwenyewe sipendi kabisa ishhu za udini kabisa kwa sababu zinapikwa na watu ambao wanasikilizwa na jamii (viongozi wa Kiislam na wa kiserekali akiwemo raisi) lakini huku mtaani mambo shwari tunaishi vizuri bila shida yoyote, mimi naona kuna haja ya kila mwenye nia njema na nchi yetu akemee na apinge udini kwa nguvu zote, hivi tutapambana na ishu ngapi umasikini, ufisadi,ujinga,maradhi,n.k
   
Loading...