Mbona kila jambo awamu hii linapokelewa kwa kuwekewa dosari? CCM tujirekebishe

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
1,281
2,020
Hata uteuzi wa leo tayari dosari zimeonekana. Tayari malalamiko kibao kuwa watu hawapo makini majina yamejirudia.

Haya uteuzi wa Mtednaji wa TANROAD tayari utaratibu umenyoshewa vidole.

Miamala dosari! Bei za mafuta dosari! Mishahara ya watumishi dosari. Safari za Mkuu wa Nchi dosari! Ndege ya tisa kuja dosari, Rais kuwa kimya dosari! Akiongea dosari zinapatikana! Asipomjibu Gwajima dosari! Mlevi MCCM kampiga mtu risasi ba dosari! Neema kumchoma mpenzi moto dosari ya awamu hii! Kuruhusu chanjo kwa hiari dosari! Kwenda kwenda Dar dosari! Kuzuia maandamano dosari! Watu tunaodai Katiba I dosari pia! Mbowe kizuizini dosari! Sasa sijui ni lipi lililo sahihi kwa awamu hii!

Twende kazi - Mie ni MwanaCCM ila ninaapa kuwa MBOWE SIO GAIDI!
 
Back
Top Bottom